Tafuta

2020.06.19 Amani nchini Korea 2020.06.19 Amani nchini Korea 

Korea-WCC:Jitihada za kiekumene za amani katika fursa ya miaka 70 tangu vita vya Korea!

Jitihada za kiekumene kwa ajili ya amani katika mwaka wa 70 tangu kuanza vita vya Korea ndiyo kauli mbiu itakayoongoza mkutano kwa njia ya mtandao tarehe 22 Juni 2020.Fursa ya Mkutano huo imeandaliwa na Baraza la Makanisa ulimwengu WCC.Ni tukio linalotaka kuhamasisha ujumbe wa amani na mapatano katika Pensula hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ujumbe wa amani wa kiekumene katika kumbu kumbu ya miaka 70 tangu kuanza kwa vita ya Korea utawakilishwa katika mkutano kupitia majukwa ya  mitandao na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC), tarehe 22 Juni 2020 saa 7.00 nchana. Ujumbe wao utaongozwa na mada “jitihada za kiekumene kwa ajili ya amani katika mwaka wa 70 tangu kuanza vita vya Korea”. Shirikisho la Makanisa nchini Korea na Baraza la Makanisa ulimwenguni vinatafuta kuhamasisha ujumbe wa amani na mapatano kwa ajili ya peninsula ya Korea, kwa namna ya pekee ya Nchi ambazo walioshiriki vita vya Korea, kwenye mazingira ya kikanisa na isiyo. Aidha wanaunga mkono Kampeni  ya sala ya ulimwengu 2020 kwa ajili ya Korea, kuhamasisha ushirikiano wa kiekumene katika kuhamasisha msimamo wa amani ya kudumu ya Nchi.

Siku 70 za sala:Tunaomba,Amani sasa,Maliza Vita

Katika mwaka huu kwa hakika  wa miaka 70 tangu kuanza kwa vita vya Korea, Baraza la Makanisa ulimwenguni (WCC) pamoja na Baraza la kiekumene Kitaifa la Makanisa nchini Korea (NCCK), wamezindua hata siku 70 za sala kwa ajili ya amani katika Peninsula ya Korea, kuanzia tarehe 1 Machi hadi 15 Agosti 2020 duniani kote kwa kauli mbiu: “We Pray, Peace Now, End the War!”, yaani “Tunaomba, Amani sasa, Maliza Vita” kwa ajili ya kumaliza rasmi kwa Vita vya Kikorea na ubadilishwaji wa Mkataba wa Kijeshi wa mwaka  1953 kuwa makubaliano ya amani.

Kila mmoja anaweza kujongea kupitia tovuti ya Wcc

Katika tukio la mkutano kwa njia ya mtandao kuhusu “jitihada za kiekumene kwa ajili ya amani katika mwaka wa 70 tangu kuanza vita vya Korea” kati ya wale watakaozungumza ni pamoja na Katibu Mkuu wa mpito wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni WCC, Mchungaji Ioan Sauca, Makamu Mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni  Profesa Isabel Apawo Phiri, Katibu Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Makanisa nchini Korea, mchungaji  Hong Jung Lee, msimamizi wa Tume ya Makanisa kwa ajili ya Masuala ya Kimataifa wa WCC, mchungaji Frank Chikane, na Rais wa Baraza la Kitaifa la Makanisa (USA), Mchungaji  John Dorhauer. Kwa ana yeyote anayetaka kushiriki, tukio hili litatangazwa moja kwa moja katika Youtube ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC) na kupitia Tovuti yake: www.oikoumene.org/live

19 June 2020, 15:52