Tafuta

Vatican News
Waamini  wa kibudha wakiwa katika hekalu la kibudha wanasali huko Seoul nchini Korea Kusini wakati wa janga la virusi vya corona Waamini wa kibudha wakiwa katika hekalu la kibudha wanasali huko Seoul nchini Korea Kusini wakati wa janga la virusi vya corona 

Korea Kusini:Ask.Lee Ki-heon:majeraha ni wazi ni wakati wa maridhiano!

Rais wa Tume ya Maaskofu katoliki wa kwa ajili ya mapatano ya watu nchini Korea ya Kusini ametuma ujumbe wake kwamba majeraha ya nchi bado yamefunguka na hivyo ni wakati wa kufanya maridhiano ya kweli. Ameandika huo kwa ajili ya sala ya umoja wa kitaifa ambayo kila mwaka wanaadhimisha tarehe 25 Juni siku ambayo miaka 70 iliyopita ulikuwa ndiyo mwanzo wa mgogoro kati ya Korea zote mbili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kumbu kumbu ya mwaka wa 70 tangu kuanza vita vya Korea zote mbili Askofu Peter Lee Ki-heon anasema kwamba vita hivyo bado viko wazi na kwa maana hiyo ni wakati wa kufanya maridhiano. Kwa kuongozwa na Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Waefeso 2,16 isemayo “Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”, ndiyo umeongoza ujumbe wa Askofu Lee Ki-heon, Rais wa Tume ya Maaskofu katoliki wa Korea ya Kusini kwa ajili ya mapatano ya watu wa nchi hiyo. Ametuma ujumbe huo kwa ajili ya sala ya umoja wa kitaifa ambayo kila mwaka wanaadhimisha tarehe 25 Juni siku ambayo miaka 70 iliyopita ulikuwa ndiyo mwanzo wa mgogoro kati ya Korea zote mbili.

Uchungu na vita bado viko wazi

Uchungu wa vita bado uko hai na hasa migongano ambayo imetapakaa na watu wengi wameona matukio ya kutisha ambayo yamerithishwa kwa njia ya simulizi, ya kizazi hadi kikizazi. Kwa mujibu wa askofu, anasema kwa miaka sabini iliyopitia  sasa imefikia wakati wa kushinda chuki za mawazo ambayo yameleta kinzani kwa sehemu zote na kuzuia sehemu hizo mbili kukua na kuendelea kwa uhuru. Askofu Lee Ki-heon amekumbuka hatua kadhaa za kujaribu kufikia amani ya kweli. “Hatua hizo zimefanyika bila kuwa na mafanikio”. Matumaini yalikuwapo wakati wa jibu la“ Tamko la Panmunjom” mnamo Aprili 2018, wakati Rais wa Korea ya Kusini  Bwana Moon Jae-in na Kiongozi wa Korea Kaskazini Bwana Kim Jong-un, walipokutana na kuahidi jitihada hizo kwa kutia sahihi, wakiazimia ndani ya mwisho wa mwaka huo kuwa na mkataba wa amani ili kufunga moja kwa moja vita na kufikia kwa dhati kusitisha nyuklia katika peninsula.

Mkutano  wa Panmunjom ulikuwa wa matumaini 

Ulikuwa ni mkutano wa shauku kubwa na ambao uliongeza matumaini kwa ajili ya mwanzo mpya amebainisha Askofu.  Lakini Mkutano huo mkuu haujazaa matunda. Kwa mujibu wa Askofu Lee Ki-heon anasema, ukosefu wa matunda hayo unaweza kuwa umesababishwa kwa wale ambao wanajinufaisha mbele ya nchi yao. Katika ujumbe huo, pia unabainisha matatizo ya nchi ambayo ni moja katika dunia iliyogawanyika sehemu mbili mahali ambapo vita havijaisha na kuendelea kuona wazalendo wake wanaishi katika vikwazo vya nguvu kwa mantiki ya kidemokrasia.

Kuna haja ya dharura ya amani 

Kutokana na kutoisha vikwazo hivyo ndipo kuna haja ya dharura ya amani hata kama siyo kazi rahisi kwa sababu ya mivutano ya wenye nguvu zaidi. Wahusika wakuu katika ujenzi wa safari ya pamoja, lazima iwe kwa watu wa Korea. Lazima kufanya kazi pamoja na kushirikishana” amesisitiza. Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya mapatano aidha amezungumzia hali halisi ya Kanisa ambalo ndilo hasa sababu ya migawanyiko na zaidi imelazimika kutotimiza hatua zenye kuleta maoni hasa Korea ya Kaskazini. Kutokana na hilo  Askofu anashauri kuongeza  msaada na mitindo mipya ya kubadilishana na Korea kusini ili kusaidia Kanisa la Korea Kaskazini.  Askofu amesema "Tumesali sana kwa ajili ya mapatano kwa kujikita hasa nia za kila siku saa tatu usiku. Lakini tunapaswa kuwa na uwezo wa kusamehe na kushinda vikwazo na lazima tujitahihidi kuongeza nguvu. Kuanzia kwenye maparokia yetu na tunaalikwa kugeuka kuwa mitume wa amani”.

Janga la virusi vya corona nchini Korea Kusini

Akizungumzia juu ya Janga  la homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona, Askofu  Lee Ki-heon anakumbuka kwamba Korea Kusini imejitahidi kwa ngazi ya ulimwenguni katika uwezekano wa  kupunguza kikamilifu kuenea kwa virusi hivyo. “Itakuwa muhimu kwamba Kaskazini inaweza kutegemea maarifa, juu ya programu na zana zinazopatikana lakini pia kutoka Seoul”.  Kwa kuzingatia kwamba kwa  miaka mingi ambayo imepita, familia nyingi zilizotengwa kwa sababu ya vita hazitaweza kukutana tena kwa sabababu zinaendelea kuzeeka na fursa ni chache za kuweza kukumbatiana, hivyo  tuna jukumu la kuzidisha fursa hizi" amesisitiza Askofu Lee Ki-heon.

01 June 2020, 12:02