Tafuta

Vatican News
Janga la virusi vya corona bado ni tatizo barani Amerika ya Kusini Janga la virusi vya corona bado ni tatizo barani Amerika ya Kusini 

Amerika Kusini:Mtazamo nchini Paraguay,Bolivia na Brazil!

Baraza la maaskofu nchini Paraguay na serikali wafanya mkutano kukabiliana na hatua ya tatu ya kuzuia janga la virusi vya corona.Ufunguo wa kujua familia,ndiyo kozi ya mafunzo kuhusu ndoa,familia na maisha kwa miezi mitatu kupitia mtandaoni.Utafiti kwa waseminari nchini Brazil juu ya maisha yao katika mkatadha wa janga ambao umegusa kila sehemu ya nidhamu,maisha ya sala, ya miito,chakula,maombolezo, mafunzo,uhusiano.

Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Fursa ya kujadiliana juu ya kazi iliyotendeka katika harakati za kuzuian usambaaji wa virus inchini Paraguay na itifaki zilizowekwa na Kanisa kwa mantiki ya hatua ya tatu ya karantini, ndiyo zimekuwa mada msingi katika mkutano wao katika Seminario kuu  ya jiji kati ya Rais wa Baraza la Maaskofu nchini humo, viongozi wa Kanisa na wawakilishi wa serikali tawala. Kipindi cha tatu cha karantini nchini Paraguay kimeanza Jumatatu 15 Juni na kinatazamia kufunguliwa kwa hatua ya shughuli nyingine na kutathimini kila baada ya siku 21, kwa uwezekano wa kutazama mikakati iliyokwishfanywa a na Waziri wa Afya. Lengo bado linabaki la kuzuia athari za covid-19 katika sekta mbalimbali za kijami. Itifaki zilizwekwa na  Kanisa zimebainisha zitaendelea kufayiwa kazi na kutathimini taratibu ikiwa hatua hizi zikifanikiwa.

Bolivia:ufunguo wa kujia familia,ndiyo kozi ya mafunzo kuhusu ndoa,familia na maisha

Imefunguliwa kujiandikisha mtandaoni kozi ya miezi mitatu, inayohusu mada ya “ funguo za kujua familia”, kozi iliyoandaliwa na Kitengo cha Familia cha Umoja wa Kikanisa cha Baraza la Maaskofu nchini Bolivia na Tume ya Jimbo kuu kwa ajili ya Uchungaji wa Familia Takatifu. Lengo la kozi hiyo ni kutaka kuwasaidia  washiriki nafasi ya mafunzo katika nidhamu kuhusu ndoa, familia na maisha, ambayo inawezesha kujipyaisha kwa familia zao na kuwatia moyo katika kuhudumia familia katika mantiki mbalimbali za uinjilishaji mahali wanapofanya kazi. Kozi hiyo itaanza tarehe 24 Juni  kupitia majukwa ya Zoo kila Jumatano saa 1.00 jioni ambayo inawalenga wadau wote wa Uchungaji wa Familia, washauri wa familia, walimu, wazazi na raia kwa ujumla. Katika miezi hii mitatu ya mafunzo, washiriki watatatufa namna ya kukaribia hali halisi ya maisha ya familia kwa njia ya mafunzo mbali mbali kama vile taalimungu, elimu ya maisha na saikolojia. Vile vile watakuwa na hatua mantiki tatu za kukabiliana: Kanisa na familia; Maisha a Familia; na Uhusiani kifamilia.

Brazil:utafiti kuhusu mafunzo ya kikuhani katika kipindi cha janga

Ni jinsi gani ya kubaki kidete katika mafunzo ambayo ni changamoto na muingiliano wa kukabiliana na mchakato wa mafunzo. Ni swali ambalo liamefanywa kwa waseminari ambao wameshiriki sehemu za mashindano katika utafiti ulioandaliwa kwa ajili ya kujua ngazi ya mafunzo ya makuhani wakati wa kipindi cha janga la virusi vya corona ambapo matokeo yametangazwa kwenye Tovuti ya Maaskofu nchini Brazil. Kwa mujibu wa walioanzisha wazo hili Msaikolojia na Padre Douglas Alves Fontes, Gambera wa Seminari ya Mtakatifu José Jimbo Kuu Niterói nchini Brazil wamebainisha kwamba, kwa kupokea majibu wamependekeza kutafakari juu ya utume wa mafunzo kwa kipindi cha janga na baadaye watatazama changamoto za mafunzo ya makuhani yanayoendelea katika nyakati ngumu kwa wote.

Awali ya yote wametoa shukrani kwa waseminari wote ambao wameamua kujibu, kariba elfu mbili na ambao wanaendelea kuwasindikiza na kujenga safari hiyo yenye maana. Utafiti umejikita hasa juu ya maisha yao katika muktadha wa janga ambao umegusa kila sehemu ya nidhamu, ya maisha ya sala, ya miito, ya chakula , maombolezo , mafunzo, uhusiano  na majibu ambayo yamefika karibia asilimia 50 ya waseminari waliopo nchini Brazil, hasa wale ambao ni sehemu ya majimbo ya kanda ya Kusini mashariki. Sehemu kubwa ya mahojiano yalifanyika kwenye nyumba za familia zao wakati wa janga; japokuwa  asilimia hii 42.6% walijibu kwamba walikuwa wanakabiliwa na migogoro ya kifamilia wakati huu. Ikiwa kwa walio wengi, katika janga hili wamekuwa na wasiwasi mkubwa, waseminari wengi walijibu kuwa hali yao ya kihisia ni ya kawaida kwa sasa; aidha karibu  asilimia 35.7%, walijibu  kwamba wamekuwa na uzito mkubwa wa upweke. Karibu theluthi ya jumla ya waliohojiwa walisema kujiunga kwenye mtandao hasa kwa kutumia mitandao ya kijamii kuondokana na hali hii ya upweke na kutengwa.

Suala muhimu katika uchunguzi lilikuwa uzingatiaji kwa waseminari wengi walikubali kuonesha kutafakari juu ya wito wao katika kipindi hiki. Theluthi moja yao, hata hivyo, waliendelea kutegemea utafutaji wa kiroho kwa njia ya mtandao. Kwa swali juu ya shida kuu walizokutana wakati huu, majibu yalikuwa ni mengi kama vile ugumu wa kudumisha utaratibu wa sala; shida kutokana na ukosefu wa mawasiliano ya kijamii; shida zinazohusiana na utunzaji wa usafi wa kiroho; ukosefu wa kiongozi wa kiroho; ugumu wa kuhudhuria Misa  kwa njia ya mtandao. Miongoni mwa masuala ya mwisho yaliyofanyiwa kazi na uchunguzi huo, kwa maana hiyo unaibuka muktadha wa waseminari kuwa na  ukomavu wa kibinadamu hata kiroho; faida nyingine iliyoonyeshwa na kutengwa kwa sababu ya ugonjwa wa virusi vya corona  ni uwezekano wa uhusiano wa kina zaidi, katika kukuza dhamiri binafsi, ili kufikia maarifa ya kuridhisha ya udhaifu wa mtu binafsi, ambao daima upo katika utu wa mtu, kwa mtazamo wa uwezo wa kujituma na maisha ya kuwajibika. Kwa sasa, nchini Brazil ndiyo moja ya Nchi ambayo pamoja na India zinatoa wasiwasi mkubwa zaidi katika maambukizi ya virusi vya corona.

18 June 2020, 13:36