Tafuta

Vatican News
Maaskofu wa Ulaya na Afrika kwa pamoja kujali ubinadamu wa watu wake. Maaskofu wa Ulaya na Afrika kwa pamoja kujali ubinadamu wa watu wake.  (©Nastya Tepikina - stock.adobe.com)

Mizizi ya Afrika na Ulaya inawaunganisha kulinda utu na hadhi ya mwanadamu!

Maaskofu wa Afrika na Ulaya wamekuwa na ushirikiano mzuri na wenye dhamana,unaozingatia watu na zaidi katika kutetea na kulinda utu na hadhi ya mwanadamu.Haya yanajionesha katika maombi yao ya pamoja katika matazamio ya mkutano wa 6 wa viongozi wakuu wa kisiasa wa mabara haya mawili,uliopangwa kufanyika Oktoba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika matazamio ya Mkutano wa 6 wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Ule wa Afrika unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (Comece) na wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (Secam ) wametoa mchango wa mawazo yao pamoja kwa viongozi hawa. Kwa mujibu wa viongozi wa dini hawa wanaongozwa na misingi kwamba Afrika na Ulaya, ni mabara mawili yanayofungamanishwa na mizizi ya pamoja, na ukaribu wa kijiografia na wakati huo huo hata wasiwasi mkubwa kutokana na matokeo ya janga la virusi vya corona au covid-19. Wasi wasi huu ni juu ya familia na juu ya jumuiya zote kwa namna ya pekee zile ambazo wanajikuta katika hali ngumu sana ya udhaifu na kuathirika katika mabara yote mawili.

Ulaya na Afrika ni injini ya kukuza ushirikiano

Marais wa Comece Kardinali  Jean-Claude Hollerich na Philippe Nakellentuba Ouédrago wa Secam, kwa pamoja kutoka makao yao makuu ya Bruxelles na Accra, licha ya kupongeza juhudi za maandalizi ya wahusika wa sera za kisiasa za Ulaya  na Afrika, wamehimiza na wanawapa moyo wa kuelekeza kazi zao maandalizi juu ya misinga ya  hadhi  ya binadamu, uwajibikaji na mshikamano, kuzingatia uchaguzi au upendeleo kwa maskini, juu ya utunzaji wa kazi ya uumbaji na utafutaji wa ustawi wa wote. Maaskofu hao wanabainisha kuwa “Tunaamini kabisa kuwa Afrika na Ulaya zinaweza kuwa injini za kurekebisha tena ushirikiano wa kimataifa”, pia ufafanuzi wa Kardinali Hollerich juu ya jukumu la Ulaya katika  kushiriki amani na ustawi na majirani zao.

Kardinali Jean-Claude Hollerich (Comece)

Uwajibikaji wa pamoja kwa Ulaya na Afrika

Hati yao iliyopewa mada “ Katika siku zake haki itasitasiwi na kwa wingi wa amani”, kipengele kilichochukuliwa kutoka Zaburi 72 katika Biblia, unatoa mfululizo wa mapendekezo maalum ya kisiasa kwa lengo la kutazama mahusiano ya kisiasa na kiuchumi ambayo upelekea haki na ushirikiano na kuwajibika ambao anao uwezo wa  kuweka watu kuwa kitovu. Katika hilo ndipo ombi la maaskofu wa Afrika na Ulaya wanaomba ushirikiano kwa ajili ya maendeleo fungamani ya wanadamu, ekolojia fungamani, usalama wa binadamu na amani na kwa watu walio katika mzunguko.

Wasiwasi kwa jamuiya zilizo dhaifu na kuathirika

Kanisa Katoliki kwa sehemu zote mbili za  mabara zinashirikishana wasiwasi hasa kwa  ajili ya wale watu, familia na jamuiya ambazo, tayari katika hali ya mazingira magumu na udhaifu na  sasa kwa sababu ya Covid 19 zinajikuta hata zaidi katika hali ya umaskini uliokithiri na njaa, tatizo kubwa la ukosefu upatikanaji wa haki, huduma msingi za kijamii, ufisadi, vurugu, shambulio la kigaidi na mateso ya jamuiya ndogo dhaifu za kidini, pamoja na unyonyaji wa maliasili na uharibifu wa mazingira . Kati ya maombi, hayo Kardinali Ouédrago amegusia kuhusu kufutwa kwa deni ya nchi za Afrika, kwa maana ya  anathibitisha ni kuwaruhusu kufufua uchumi wao.

Kardinali Philippe Nakellentuba Ouédrago -Secam

Kanisa la Afrika ni taa hata baada ya miaka 25

Katika tamko la pamoja, makardinali hao wawili pia wanakumbuka tumaini liliotolewa katika Wosia wa kitume baada ya Sinodi ya Kanisa la Afrika (Eclesiae in Africa” wa Mtakatifu Yohane Paulo II na kwamba  hata baada ya miaka 25 wosia huo “bado unatujaza leo kwa kututia moyo na bidii ya kuchangia katika kukabiliana na  changamoto hizi”. Kwa maana hiyo katika hitimisho la makardinali hawa Hollerich na Ouédrago wanasema “Tunaamini kwamba  misingi na maadili ya hadhi ya binadamu, mshikamano, viwe  chaguo na upendeleo kwa maskini, mwelekeo wa mali za ulimwengu, uhamasishaji  wa maendeleo ya kibinadamu, usimamizi wa jukumu la kila kitu katika kazi ya uumbaji pamoja na utafataji wa ustawi wa wema viwe ndiyo mwongozo muhimu na mwelekeo katika kufafanua majibu husika na hatua za kisiasa”.

10 June 2020, 15:10