Tafuta

Vatican News
2020.05.07 Padre Manuel Barrios Prieto,Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu  barani Ulaya (Comece). 2020.05.07 Padre Manuel Barrios Prieto,Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Ulaya (Comece). 

ULAYA#coronavirus-Comece:ufunguzi wa makanisa kwa upya urejeshwe haraka!

Mmomonyoko wa aina yoyote ya haki msingi katika muktadha wa sasa wa dharura pamoja na ile ya uhuru wa dini,haipaswi iwe sheria mpya ya kawaida,kinyume chake haki hizi lazima zirejeshwe kikamilifu kwa haraka iwezekanavyo.Amethibitisha hayo mwakilishi wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya ya Ulaya kwa kuzingatia hali ya sasa ya vikwazo na ambayo ameitaja kama mchezo wa uhuru wa kidini.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika mantiki ya mapambano dhidi ya virusi vya corona au Covid-19, kuna mchezo wa uhuru wa kidini kwa mujibu wa Padre Barrios Prieto, Katibu Mkuu wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya za Nchi za Ulaya (COMECE) katika taarifa yake iliyotangzwa tarehe 6 Mei 2020 katika tovuti ya ya Shirikisho hilo Comece. Katika wakati ambao Nchi nyingi za Ulaya zimeanza hatua ya II ya janga la ugonjwa wa virusi vya corona, kudorora kwa baadhi ya hatua za usalama wa kiafya na ufunguzi kwa mara nyingine wa huduma nyingine, bado inabaki kutokuwa na uhakika katika masuala ya kurudisha maadhimisho la liturujia za Kanisa kwa ajili ya waamini. Kwa maana hiyo Padre Prieto amethibitisha kuwa ufunguzi wa Makanisa katika kuheshimu kanuni na busara za kiafya, lazima itekelezwe na viongozi wa umma kwa njia iliyo wazi na isiyo ya ubishi, kwa heshima kamili na mazungumzo na taasisi za Kanisa “kwa sababu uhuru wa dini, pamoja na uhuru wa ibada ni haki  msingi na hitaji la kweli kwa watu wengi.

Majadiliano kati ya Kanisa na jumuiya kitaifa ni muhimu

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa COMECE anabainisha kuwa katika dharura ya sasa, majadiliano kati ya Makanisa na za Jumuiya na kitaifa ni muhimu, kama ilivyo daima.Kwa namna hiyo ni masikitiko yake Padre Prieto kiukweli kwamba njia kuu ya hatua za kudhibiti janga hili, lililochapishwa hivi karibuni na Tume ya Jumuiya ya Ulaya, haikuwa na kumbukumbu yoyote iliyo wazi kabisa kuhusu shughuli za kidini. Na hiyo imemkatisha tamaa kwa sababu ya kutozingatia nafasi msingi wa dini katika jamii ya Ulaya, amesema. Dini kwa hekema amesema, mkuu huyo wa Comece kuwa "siyo suala kirahisi la mtu binafsi, lakini pia lina ukuu wake maalum wa umma na wa pamoja, kama ilivyoelezewa bayana hata katika misingi ya mikataba yote ya haki za binadamu".

Kufurahia haki msingi wa uhuru wa dini kwa jamii ni demokrasia

Kwa kuzingatia hili, amebainisha kuwa mbinu za fujo ya watendaji wengine walei dhidi ya jukumu la dini kwenye uwanja wa umma imesikitisha, kwa sababu inaweza kuwa ilichangia na kukandamizwa kwake katika muktadha wa shida ya sasa. Kwa upande mwingine, amesema, Baraza la Ulaya lenyewe linaendelea na maoni kwamba kufurahia haki msingi wa uhuru wa dini ni kumbukumbu kwa jamii za demokrasia za kisasa. Na kila wakati Baraza hili linawaalika viongozi ili kuhakikisha kuwa zizuizi vyovyote vilivyowekwa wazi na sheria kwa kufuata dhamana husika ya kikatiba na sawa sawa na malengo yaliyotekelezwa. Hatimaye mwakilishi wa  COMECE ameisitiza kwamba "mmomonyoko wa aina yoyote ya haki msingi katika muktadha wa sasa wa dharura, pamoja na ile ya uhuru wa dini, haupaswi kamwe kuwa sheria mpya ya kawaida, kinyume chake: haki hizi lazima zirejeshwe kikamilifu kwa haraka iwezekanavyo".

07 May 2020, 10:36