Tafuta

Vatican News
Watu wengi wa hali ya duni nchini Uingereza wamekufa kwa ajili ya maambukizi ya virusi vya corona.Askofu Paul McAleenansisi amesema wote wanalo jukumu la kukabiliana na  suala la ukosefu wa usawa katika jamii  yao. Watu wengi wa hali ya duni nchini Uingereza wamekufa kwa ajili ya maambukizi ya virusi vya corona.Askofu Paul McAleenansisi amesema wote wanalo jukumu la kukabiliana na suala la ukosefu wa usawa katika jamii yao.  (ANSA)

Uingereza#Coronavirus:Dharura ya mpango wa matendo ya dhati dhidi ya ukosefu wa usawa!

Maaskofu nchini Uingereza wanabainisha kuwa wote wana jukumu la kukabiliana na suala la kizamani la ukosefu wa usawa katika jamii yao ambayo katika mgogoro wa kiafya umefunua uwazi hali halisi ya watu wadhaifu kiuchumi.Wanathibitisha hayo mara baada ya takwimu za vifo vingi vya watu kutokana na virusi vya Corona nchini humo kuwakumba watu wa makabila madogo kwa mujibu wa Chama Katoliki kwa ajili ya haki ya makabila (CARJ).

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mpango mkubwa wa hatua ya dhati unahitajika wa dharura ambao uruhusu mabadiliko ya kweli katika jamii ya Uingereza kuweza kudhibiti ukosefu wa usawa wa kijamii ulioibuka sana katika mzozo wa ugonjwa huu wa mapafu ya virusi vya corona. Ni wito wa  Chama Katoliki kwa ajili ya haki ya makabila (CARJ) nchini humo ambao wameomba kwa sauti kubwa. Wamesisitiza hayo mara baada ya matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni wa Ofisi ya Takwimu ya Uingereza ambayo iligundua na kuonyesha idadi kubwa ya vifo kutokana na virusi vya corona vimewakumba watu wa makabila madogo madogo ikilinganishwa na sehemu yao kwa jumla ya idadi ya watu wote. Ni matokeo ambayo yalimsukuma Mtendaji kufungua uchunguzi na Chama cha Wafanyakazi kwa upande wao kuanzisha uchunguzi wao.

Watu wa makabila madogo nchini Ungereza wako hatarini

Kwa mujibu wa Chama hicho CARJ, takwimu zilizokusanywa zinaonesha  mambo kadhaa yanahusiana kwa karibu, ambayo  kwao wanasema hakuna  hata moja linaweza kupuuzwa. Haya ni pamoja na umaskini, aina ya kazi inayofanywa na hali ya makazi ambayo imechangia kufanya makakabila madogo nchini Uingereza yawe hatarini zaidi kuliko raia wengine. Jambo muhimu la kutoa maelezo ni uwepo mkubwa wa wafanyakazi kutoka katika jumuiya hizi kwenye sekta zinazofikiriwa kuwa muhimu, lakini mara nyingi hulipwa mshahara kidogo. Na hizo sektea ni kama vile kutunza watu, usafirishaji barabarani, biashara, kusafisha na utunzaji wa afya. Kwa kuongezea, Chama hiki Carj kinabainisha, ingawa walikuwa wazi zaidi kupata maambukizi, aina za watu hawa hawakupewa kipaumbele cha kuchukuliwa vipimo.

Hitaji la kuwa mpango wa matendo ya dhati ya muda mfupi na mrefu

Kutokana na hali hiyo ndipo kuna hitaji lilionyeshwa na wakala wa maaskofu wa Uingereza na Walles ili  kuwa na mpango wa hatua za matendo ya dhati wa muda mfupi na mrefu. Mpango wa muda mfupi, maana yake ni suala linalotakiwa kupata msaada wa dharura ambao jumuiya hizi zinahitaji. Kwa upande wa muda mrefu, maana yake kipaumbele lazima kutolewe katika mapambano dhidi ya ukosefu wa usawa ambapo katika makundi haya ndiyo waathirika, kwa mfano katika: malipo, elimu, nyumba na ajira. Lakini ili kuboresha hali ya kijamii na kiuchumi ya raia hawa kiuukweli Chama hiki Katoliki cha masuala ya makabila madogo nchini Uingereza  (Carj) kimesisitiza juu ya utekelezaji wa mpango huu wa hatua ambayo lazima ifuatiliwe mara kwa mara na wataalam na matokeo yachapishwe mara kwa mara.

Tuna jukumu la kukabiliana na ukosefu wa usawa

Matumaini ni kwamba Mtendaji ataweza kushughulikia kwa uzito maswala haya.  Na hata ni matumaini yaliyoungwa mkono na Askofu Paul McAleenan, msaidizi wa Jimbo Katoliki la Westminster ambaye pia ni mwenyekiti wa Ofisi ya Sera za Uhamiaji wa Baraza la  Maaskofu wa Uingereza na Walles(CBCEW). Katika kuunga mkono amesema “ sisi sote tuna jukumu la kukabiliana na  suala la zamani la ukosefu wa usawa katika jamii yetu ambayo katika mgogoro wa kiafya imefunua  uwazi wa hali halisi”.

22 May 2020, 11:14