Tafuta

Vatican News
Serikali nchini Ufilippino imetangaza mpango wa kuondoa watu wasio kuwa makazi ya kudumu jijini Manila ili warudi mashambani. Serikali nchini Ufilippino imetangaza mpango wa kuondoa watu wasio kuwa makazi ya kudumu jijini Manila ili warudi mashambani.  (AFP or licensors)

Ufilippino#Coronavirus:Mpango wa kurudisha watu shambani bila uwekezaji mkubwa!

Serikali imetoa uamuzi wa kurudisha watu wanaoishi pembezoni mwa jiji la Manila warudi mashambani baada ya janga la dharura,lakini ni mpango ambao hauna uwekezaji,kiasi kwamba mazingira ya umasikini yatawafanya warudi tena jijini,kwa maono ya Askofu Msaidizi wa Manila na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Kuu la Manila.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Dharura ya Coronavirus imesukuma serikali ya Ufilipino kuondoa mradi wa zamani wa maendeleo ili kuhimiza kurudi katika mashamba kwa kuwaondoa watu katika mitaa mibaya iliyojengwa nje ya mji mkuu Manila. Umasikini wa mashambani nchini Ufilipino ndiyo kweli sababu kuu ya uhamiaji wa ndani kutoka vijijini kwenda katika miji mikubwa kama mji mkuu huo, ambapo hata hivyo inaunda hali mpya mpya za kufurika kwa watu. Hii ni hali ambayo imejionesha zaidi wakati huu wa janga la virusi.

Kwa maana hiyo Rais wa Nchi Bwana Rodrigo Duterte ametangaza “Balik Probinsya, Bagong Pag-asa Program”, yaani Mpango wa kurudi katika wilaya mahalia”. Mpango huo umekubaliwa kwa shingo upande kutokana kwa maono ya Askofu Broderick Pabillo Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Manila na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo hilo ambaye anakumbuka jinsi mipango mingi kama hiyo imeshindwa hapo awali kutokana na  kukosekana kwa kazi watu wengi waliotumwa kurudi mashambani, na walirudi tena  jijini.

Askofu Pabillo aliyeinukuliwa na shirika la habari  la maaskofu Cbcpnews) “Sasa wanaahidi kuwapa mafunzo ya kitaalam na kuanza kuwapa mtaji ili kuwasaidia kukaa na hii ni matokeo chanya, lakini haitoshi. Kwa mujibu wa  amebainisha kuwa ili mradi huo mpya ufanye kazi, serikali na biashara lazima ziwekeze pakubwa  kwa  kutoa ajira na huduma katika maeneo ya vijijini. Janga amsisitiza lihamasishe wito kwa Serikali ili waweke umakini sana katika sekta ya kilio  ambayo hadi sasa ilikuwa imesahalika .“Kutengwa na kukaa ndani kwa mara nyingine  kumedhihirisha jinsi wakulima na wavuvi ni muhimu katika uchumi wa Ufilipino na maisha yetu”.

19 May 2020, 12:20