Tafuta

Vatican News
Vijana ni matumani ya Kanisa ambapo Kanisa la Tanzania linachanua miito ya Kikuhani. Vijana ni matumani ya Kanisa ambapo Kanisa la Tanzania linachanua miito ya Kikuhani. 

TANZANIA:Ufunguzi wa Seminari Kuu mpya Kahama,Tanzania!

Nchini Tanzania imepata neema ya miito ya kikuhani lakini inahitajika kuwa na jengo la kuwezesha waseminari mahali pa kuendelea na masomo yao ya juu.Mchango mahalia wa nchi hautoshi,kwa sababu hiyo Baraza la Maaskofu kupitia Rais wa Baraza la Maasko,Askofu Mkuu Nyaisonga,anatoa wito kwa wafadhili wengine wenye ukarimu ili kutimiza lengo hili.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican

Kanisa nchi Tanzania linatarajiwa kuwa na neema ya kupata Seminari Kuu mpya. Hiyo itaitwa Seminari Kuu ya Nazareth inayotarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu katika Jimbo Katoliki la Kahama. Ni mpango  uliofikiriwa kwa muda na Baraza la Maaskofu ili kukabiliana na ongezeko la miito ya kikuhani nchini humo.

Tangu kuwekwa wakfu wa daraja la kikuhani kwa  mapadre wa kwanza 4 wa asili kunako mwaka 1917, miito  nchini Tanzania imeonekana kuongezeka na ambayo hata hivyo imekuwa ikiongezeka katika miaka ya hivi karibuni na kupelekea kujaa sana kwa majengo ya seminari kuu tano zilizopo nchini humo kama ifiatavyo: ya Mama Yetu wa Malaika iliyopo Kibosho mkoani Kilimanjaro, ya Mtakatifu Agostino, iliyopo Peramiho, mkoa wa Ruvuma, ya Matakatifu Antony wa Padua iliyopo Ntungamo mkoani Kagera, ya Mtakatifu Paolo huko Kipalapala mkoani Tabora na Seminari Kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Segerea Mkoa wa Dar -Salaam.

Hata hiyo kwa mujibu wa taarifa ni kwamba tayari Seminari sasa hivi zimekwisha fanya usajili wa idadi kubwa zaidi kuliko uwezo wao. Kwa namna ya pekee la wanafalsafa wa Kibosho na Ntungamo  ambao wana idadi kubwa zaidi ya waseminari 140 na wakati  wengine 250  wanapaswa kuanza masomo yao ya juu mwaka ujao wa kimasomo 2020-2021, walakini  mia yao wako hatari ya kutokubaliwa kwenye kozi hizo. Kutokana na hilo ndipo kuna ulazima wa kuharakisha muda wa kujenga Seminari Kuu mpya huko Kahama.

Mchango mahalia wa nchi hiyo hata hivyo, hautoshi, kwa sababu hiyo Baraza la Maaskofu kupitia Rais wa Baraza hilo Askofu Mkuu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga, ametoa wito kwa wafadhili wengine wenye ukarimu ili kutimiza lengo hili.

Hivi sasa nchini Tanzania kuna makuhani wazaliwa  zaidi ya elfu mbili, ambao pamoja na wamisionari wa nje wanatoa huduma  karibu kwa waamini milioni 14, sawa na theluthi moja ya idadi ya watu, zaidi ya asilimia 40 ya Wakristo na karibu Waislamu asilimia 35%.

08 May 2020, 16:13