Tafuta

Hata kama janga limeleta athari nyingi hasi, lakini Neno la Mungu lazima litangazwe kwa kila kona ya dunia. Hata kama janga limeleta athari nyingi hasi, lakini Neno la Mungu lazima litangazwe kwa kila kona ya dunia. 

Pwani ya Pembe#coronavirus:Katika janga mshikamano na ushuhuda viendelee!

Utume ni amri ya Kristo,yaani mapenzi ya Kristo anavyotaka kwenda kila kona ya dunia na kuwa wafuasi wake.Ni kwenda kuwaelekea wengine hata kama leo hii janga la corona linaleta vikwazo.Kwa maana hiyo ni kutafuta au kubuni mbinu za kuweza kuendeleza utume huo ambao pia ulikabidhiwa kwa Shirika la Kipapa la Matendo ya kimisionari ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kipindi ambacho tunakipitia ni kipindi kigumu sana kwa mantiki zote za maisha ya binadamu na Kanisa haliwezi kukwepa matokeo hayo, lakini utume wake unaendelea kwa mujibu wa Padre Jean Joel Gossou, Mkurugenzi wa Kitaifa wa masuala ya Matendo ya Kimisionari nchini Pwani ya Pembe, katika mazungumzo na Shirika la habari za Kimisionari Fides, kuhusiana na athari za janga la covid-19 na shughuli za utume katika nchi hiyo.

Padre Gossou amesema utume ni amri ya Kristo, yaani mapenzi ya Kristo anavyotaka kwenda kila kona ya dunia na kuwa wafuasi wake. Ni kwenda kuwaelekea wengine hata kama leo hii katika janga la virusi vya corona kuna vikwazo. Kwa muktadha huo ni kutafuta au kubuni mbinu za kuweza kuendeleza utume huo ambao pia ulikabidhiwa kwa Shirika la Kipapa la Matendo ya kimisionari ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kitaifa anasema, utume leo hii unaendelezwa shukrani kwa akili za watu kupitia njia za mawasiliano kama vile radio, TV, mitandao ya kijamii au ujumbe mbali mbali hasa wa kutuma vifungu vya Kibiblia. Kwa wakristo wanawatumia ujumbe wa  kuwatia moyo, kutunza zile cheche za moto wa uamsho wa kimisionari. Kwa kuongeza amethibitisha kwamba Covid-19 haipaswi isimamishe utume hata kama vikwazo vya kusafiri kutoka sehemu kwenda nyingie vipo. Hiyo kwa hakika inawezekana kuendelea na utume kwa kutoa ushuhuda  wa upendo wa Kristo kila mahalia tunapokuwapo.

Pili, Padre Gossou amebainisha kwamba tunaposhuhudia, tunakuwa mashuhuda wa upendo, wa mshikamano, wa hisani, katika mazingira ya maisha na kwa maana hiyo huo ndiyo utume unaoendelea. Ndiyo hali halisi katika nyakati hizi za mgogoro wa kiafya ambapo ishara za mshikamano zinazidi kuongezeka kwa mantiki nyingi. Padre Gossou amesisitza kuwa "licha ya janga la virusi vya Corona, utume unaendelea zaidi hata kwa maombi ambayo ndiyo sehemu msingi wa maisha ya utume wa Shirika la Kipapa  la Matendo ya Kimisionari na Kanisa la ulimwengu". 

20 May 2020, 12:48