Tafuta

Vatican News
 NIGER#coronavirus makanisa yatafunguliwa kwa sikukuu ya Kupaa kwa Bwana NIGER#coronavirus makanisa yatafunguliwa kwa sikukuu ya Kupaa kwa Bwana  (ANSA)

NIGER#coronavirus:makanisa yatafunguliwa katika sikukuu ya Kupaa kwa Bwana!

Siku iliyochaguliwa kufunguliwa kwa makanisa ili kuendelea na liturujia nchini Niger itakuwa tarehe 21 Mei sambamba na sherehe za siku kuu ya Kupaa kwa Bwana.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baada ya kufungwa makanisa kwa sababu ya dharura ya virusi vya Corona, hata Nchini Niger wameazimia kufungu makania yao tarehe 21 Mei 2020 ili waendelee na maadhimisho ya kiliturujia kuwaruhusu waamini wasali na kutafakari ibada zao. Ni kwa mujibu wa maaskofu wa nchi hiyo mara baada ya kukabiliana na mapadre na Baraza la maaskofu wa Burkina-Niger. Tarehe hiyo iliyochaguliwa ni sambamba na sherehe za siku kuu ya Kupaa kwa Kristo.

“Kurudi tena katika makanisa yetu kwa ajili ya liturujia yatazingatia kwa kiwango kikubwa cha hatua na sheria zilizowekwa  na mamlaka za kiafya katika nchi yetu”, kwa mujibu wa ujumbe wa maaskofu uliotangazwa tarehe 16 Mei 2020- . Aidha wanabainisha hasa katika kuzingatia kunawa mara kwa mara mikono vizuri kwa maji na sababuni, kufanya usafi katika maeneo ya ibada,  kuweka umbali  wa kukaa moja na mwingine karibu, kuzuia kupeana mikono na mambo mengine.

Katika kuhitimisha ujumbe uliotiwa sahihi ya Askofu wa Niamey, Laurent Lompo, wanamwomba Mungu aweze kuokoa ulimwengu na janga la covid-19. Hadi kufikia Jumapili 17 Mei 2020 nchini Niger walikuwa wanahesabu kesi za maambukizi ya covid-19 889 na vifo 51.

18 May 2020, 13:58