Tafuta

Vatican News
Kabla ya kuingia kanisani , lazima kusanifisha mikono Kabla ya kuingia kanisani , lazima kusanifisha mikono  (ANSA)

Kurudia maadhimisho ya Ekaristi kwa watu wa Mungu barani Afrika!

Baadhi ya nchi katika bara la Afrika wameanza kufungua makanisa yao kwa ajili ya maadhimisho ya liturujia za Ekaristi kwa uwepo wa waamini.Ni mfano wa matumaini katika Kanisa la Niger na Pwani ya Pembe.Shauku ya kuzidisha misa katika kipindi hiki cha janga ni kubwa ili kuwezesha kuzuia mkusanyiko mkubwa ambao unaweza kusababisha maambukizi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Nchi nyingi barani Afrika, zimerudia kufungua makanisa kwa ajili ya kuadhimisha liturujia zao na watu wa Mungu mara baada ya kukaa karantini kwa siku kutokana na janga la virusi vya corona. Ni ishara ya matumaini, katika bara la Afrika mahali ambapo katika kipindi cha Pasaka watu wengi wamekosa ule muungano, sherehe na chereko, ambacho huwa ni kipindi muhimu cha kuandaa ubatizo kwa watoto na zaidi wakatekumeni. Katika ufunguzi huu, ni ishara ya wazi kwamba waaamini wanayo shauku kubwa ya kukutana tena na kuandaa kwa haraka kusheherekea kwa pamoja mafumbo ya Ekaristi.

Furaha ya waamini nchini Niger japokuwa na mashambulizi ya kigaidi

Hata hivyo katika Nchi ya Niger, mahali ambapo asilimia kubwa ya raia ni  waislam, jumuiya ndogo katoliki, imekuwa na furaha kubwa kwa mara nyingine   kusali tena kwa pamoja baada ya karantini, iliyoweka hata mguu wake katika makanisa. Kwa mujibu wa Padre Vito Girotto, mmisionari katika mji mkuu Niamey nchini Niger, amebainisha juu ya utambuzi wa kina wa watu wake ambao wamejeruhiwa tangu awali na mashambulizi ya kigaidi katika mikono ya Boko Haramu na kwa sasa  hata ubaya mkubwa wa virusi vya corona!

Hata katika kipindi cha karantini visa vya mashambulizi haikusita

Cha kusikitisha ni kwamba hata katika kipindi hiki cha karantini, mashambulizi ya kigaidi hayakukoma kwa mfano katika kijiji kimoja cha  Bomoanga, mahali alipotekwa nyara Padre mmisionari Luigi Maccalli ambaye bado yupo kwenye mikono ya magaidi hao, kulikuwa na msalaba uliowekwa katika kilima na mapadre wenzake wa kidini. Hivi karibuni msalaba huo uling’olewa. Na ndiyo sababu kwamba ufunguzi wa makanisa kwa mara nyingine tena ni ishara ya matumaini na karibu ukombozi. Afrika anasema Mmisionari huyo, ishala za liturujia ni muhimu sana. Na jambo linalosikitisha sana kwa upande wa waamini ni lile la kutosalimiana na kupeana amani wakati wa maadhimisho ya misa. Kwa kwa namna hiyo wakati wa kupeana amani, wao waliangalia tabernakulo kwa kitambo na baadaye kuendelea na misa. Lakini hata hivyo hisia ni nzuri sana ya kurudia katika maadhimisho ya misa kwa maana inawasaidia kuvumilia kila aina ya matatizo.

Pwani ya Pembe misa zimeongezeka mara mbili

Na furaha pia imekuwapo sana katika ufunguzi wa makanisa nchini  Pwani ya Pembe. Karantini kutokana na janga la virusi, ilikuwa umetupilia mbali kwikwi za jumuiya katoliki mahali ambapo walikuwa wanasubiri kwa hamu sana uwezekano wa kurudi  kuishi maadhimisho ya ekaristi. Kwa mujibu wa Padre Leopoldo Molena, ambaye yupo katika maeneo hayo kama mmisionari wa siku nyingi amesema,  jumuiya  yao ina nguvu sana kwa maana hiyo kipindi cha kurudi kanisani kimerudisha matumaini na maono chanya ya wakati wendelevu. Kwa kufuata itifaki za usalama wa kuzuia maambukizi, katika makanisa hawawezi kuingia waamini zaidi ya miambili. Nchini Pwani ya Pembe au kama ilivyo Afrika nzima, kwa kawaida misa zinajaa umati mkubwa sana. Kwa maana hiyo wameamua kuongeza misa nying ili watu waweze kuwa wachache katika makanisa kwa kuruhusu uwepo wanafasi kulingana na kanuni zilizowekwa kwa ajili ya kuzuia maambukizi zaidi ya corona. Na kwa kufanya hivyo mahali ambapo walikuwa wanaadhimisho ya  misa mbili kwa sasa wameweka maadhimisho ya misa tano!

26 May 2020, 14:35