Tafuta

Vatican News
2020.05.19. Askofu Mkuu Coleridge, wa Jimbo Kuu Katoliki la Brisbane,Australia. 2020.05.19. Askofu Mkuu Coleridge, wa Jimbo Kuu Katoliki la Brisbane,Australia. 

AUSTRALIA#Ripoti ya kuhamasisha uwajibikaji katika utawala wa Kanisa katoliki !

Maaskofu Katoliki nchini Australia wamewasilisha Ripoti kuhusu kuhamasisha uwajibikaji katika utawala wa Kanisa Katoliki.Tume ya Shirikisho na Tume ya Uchunguzi ya mahojiano katika kutoa majibu ya taasisi kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto,ina mapendekezo 86 ambayo yanapaswa yawe muhimu kwa utawala ulio bora wa Kanisa nchini Australia.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Maaskofu katoliki nchini Australia wamesilisha ripoti  yao kuhusu uhamashaji wa uwajibikaji katika utawala wa Kanisa katoliki la Australia, ripoti hiyo wameiwakilisha kabla ya mkutano wao wanaotarajia kuufanya mwaka huu. Kufuatia na pendekezo kutoka kwa Tume ya Shirikisho na Tume ya Uchunguzi ya mahojiano katika kutoa majibu ya taasisi kuhusiana na  unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, ina mapendekezo 86 ambayo yanapaswa yawe  muhimu kwa utawala ulio bora wa Kanisa huko nchini Australia. Katika ripoti imegawanyika katika vifungu kadhaa kama vile: ufadhili, utawala, mikutano, majadiliano, mang’amuzi na uongozi  pia inatoa maoni madhubuti juu ya jinsi gani  ya kuimarisha jukumu la walei na kuhakikisha wajibu wao vya kutosha, iwe kwa ngazi ya kiparokia na hata ya kijimbo.

Wajumbe wa timu ambayo ilifanya kazi katika mpango wa uhakiki wanastahili kupongezwa kwa kazi kubwa ambayo wamefanya na itakayo kuwa na matokeo na chachu kwa maisha na utume wa Kanisa, kama alivyothibitisha Rais wa Baraza la Maaskofu Australia (Acbc), Askofu Mkuu Mark Coleridge. Kwa kuongezea Asjìkofu Mkuu ameeleza kwamba, maaskofu kwa sasa watashauri, watachambua na kuijadili  ripoti hiyo katika ngazi ya kijimbo au katika mkutano wao, mwezi Novemba mwaka huu kabla ya kuchapisha na kujibu mapendekezo.

Hata hivyo pia amebainisha kuwa ripoti hiyo itatoa mchango mkubwa katika mijadala wakati wa Mkutano wao wa kitaifa kwa jumuiya nzima katoliki ya Australiakatika sehemu zake mbali mbali na itaitwa kujadili na kutafakari juu ya hatma ya utume wa Uinjilishaji wa Kanisa nchini humo  na kwenye njia itakayochukuliwa mbele ya changamoto zake mpya. Mkutano wao ulikuwa ufanyike mjini Adelaide kuanzia tarehe 4 -11 Okotaba 2020, lakini kutokana na dharuru ya virusi vya covid-19, Tume imeharisha kuhaisha hadi  2021,mahali ambapo walikuwa wanatazamia kufanya mkutano wao wa pili jijini Sydney, kuanzia 28 Juni- 3 Julai.

19 May 2020, 12:35