Tafuta

Vatican News
Pasaka ya Kiorthodox: Katika ujumbe wa Pasaka kutoka kwa Patriaki Kirill wa Moscow Urusi anawaalika waamini wabaki kidete katika imani na kusali kwa kina wakiwa nyumbani. Pasaka ya Kiorthodox: Katika ujumbe wa Pasaka kutoka kwa Patriaki Kirill wa Moscow Urusi anawaalika waamini wabaki kidete katika imani na kusali kwa kina wakiwa nyumbani.  (AFP or licensors)

Urusi:Ujumbe wa Pasaka wa Patriaki Kirill:ujarisiri na kubaki kidete katika imani!

Katika ujumbe wa Pasaka kwa upande wa Kanisa la Kiorthodox kutoka kwa Patriaki Kirill wa Urusi anasema Mfufuka atawaimarisha na kuwapa ujasiri wa kubaki kidete katika imani.Terehe 19 Aprili sambamba na Siku kuu ya huruma ya Mungu kwa wakristo wakatoliki,Kanisa la Kiorthodox linaadhimisha siku kuu ya ufufuko wa Bwana.Patriaki ameandika kuwa katika ufufuko wa Kristo unajionesha utimilifu wa upendo wa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika ujumbe wa Pasaka ambayo ni sikukuu kubwa kati ya sikuu zote za Kanisa la Kiorthodox, Patriaki Kirill waMoscow nchini Urusi unaanza kwa kusema “Tufurahi kwa upya kwa ajili ya utukufu wa Ufufuko wa Bwana". Anawakumbusha kwamba katika ufufuko wa Kristo unajionesha utimilifu wa upendo wa Mungu  na kwamba  Bwana ameshinda mauti. Terehe 19 Aprili 2020 sambamba na Siku kuu ya Huruma ya Mungu kwa wakiristo Wakatoliki, Kanisa la Kiorthodoxla katika nchi za Mashariki na nyinginezo linaadhimisha Siku Kuu ya Ufufuko wa Bwana.  Kwa maana hiyo wiki moja baada ya Pasaka kwa Wakristo wa makanisa ya Mashariki kufuatana na kalenda ya kijuliani.

Patriaki Kirill katika ujumbe wake wa Pasaka anabainisha kuwa mwaka huu, watu wa Mungu duniani wanaishi kipindi cha majaribu kwa namna ya pekee kilicho sababishwa na virusi vya corona “lakini kama wakristo wa kiorthodox, hatupaswi kujisalimisha na kukata tamaa katika hali hizi ngumu, kama ilivyo hata hofu”, anaandika Patriaki na kuongeza kuwa “Tumeitwa kutunza amani ya ndani na kukumbuka maneno ya Mwokozi, yaliyotamkwa katika usiku wa mkesha wa Mateso yake ya ukombozi: "mtakuwa na dhiki katika ulimwenguni, lakini kuwa na imani: Mimi nimeshinda ulimwengu!

Patriaki Kirill anasisitiza kuwa "ni kwa neema ya Ufufuko wa Kristo, tunapata uhuru wa kweli” na anawaalika waamini wasigeuke kuwa “ watumwa wa ubatili wa ulimwengu huu ì, kwa kuangukia mbele ya hofu zinazopita na kusahau tunu msingi ya kiroho na wito wa kweli wa mkristo katika kuhudumia Bwana”. “Dini iliyo safi bila madoa mbele ya Mungu wetu Baba ni ile ambayo inatokana na upendo, uvumilivu katika udhaifu wa wengine, kusaidia watu wengine katika majaribu kwa mfano ulio onyeshwa kwetu na Injili ya Mchungaji mwema.  Ameongeza  kuandika Patriaki wa Moscow na Urusi yote.

Aidha Patriaki Kirill amesisitiza kuwa "hakuna vizuizi vya nje vinaweza kusambaratisha umoja wetu,  kwa sababu sisi sote ni wajumbe  wa mwili mmoja katika Kristo, kwa dhati  ni imani inayosaidia kutupatia nguvu za kuishi na kushinda, kwa msaada wa Mungu katika magonjwa yote na majaribu".

Hatimaye, Patriaki anaomba wote kuzidisha nguvu ya sala ya pamoja. "Bwana atupatie neema ya kubaki thabiti katika kushiriki maisha ya liturujia ya Kanisa, licha ya matatizo yote yaliyopo” na  matashi yake Patriaki ni kwamba “ Sakramenti ya Ekaristi iendelee kuadhimishwa” na kwamba  "waamini wanaweza kupata kutoka katika  Kisima cha kweli cha maisha ule Mwili na Damu ya Kristo" na kwamba “wagonjwa wapate kupona”. “Tunaamini kuwa Bwana mfufuka hatatuacha, atatupatia nguvu na ujasiri wa lazima ili kubaki thabiti katika imani ili kuendelea katika mchakato wa safari ya kwenda mbinguni na kufikia maisha ya milele”. Amehitimisha ujumbe wake

18 April 2020, 18:06