Tafuta

Vatican News
2020.04.23 Wakati asili, wanyama na ndege  wanafurahia, binadamu anaangaika na kuwa na hofu.Ni wakati sasa kuwa na maelewano kwa sababu kila kitu kimetolewa na Mungu kwa wema wake.Chaguo ni letu sote pamoja 2020.04.23 Wakati asili, wanyama na ndege wanafurahia, binadamu anaangaika na kuwa na hofu.Ni wakati sasa kuwa na maelewano kwa sababu kila kitu kimetolewa na Mungu kwa wema wake.Chaguo ni letu sote pamoja 

Patriaki Bartholomew I:Inahitajika kuwa na maelewano kati yetu,kujipyaisha na kusaidiana!

Katika siku ya kimataifa ya kuenzi Mama Dunia,katika ujumbe wa Patriaki Bartholomew I anasisitiza kuwa na maelewano ndani mwetu,kujigundua kwa upya na kusaidiana mmoja na mwingine,itakuwa ni fursa tena ya kupata maisha na kushinda wakati huu huku tukiingia kwa mara nyingne tena katika uhusiano mpya na Dunia na ulimwengu wote,kwa sababu kila kitu kimetolewa na Mungu kwa wema wake.Chaguo ni letu pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Janga la virusi vya corona limefanya ubinadamu  wote ugutuke na kutambua udhaifu wake wakati kwa wakristo katika nyakati hizi ni kama kipindi cha majilio, ni saa zenye  giza katika matarajio ya kuona  dunia iliyo mpya. Ndivyo Patrikaki wa Kiekumene Bartholomew I ameandika na kutoa sahihi yake katika ujumbe kwenye tukio la  maadhimisho ya miaka 50 ya Siku ya kuienzi Dunia Mama inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 22 Aprili ya kila mwaka.

Siku hii ilianzishwa na wanafunzi wa Marekani kunako mwaka 1970. Sherehe hizi za kimataifa zinazoadhimishwa karibu katika nchi 193  kwa upande wa nchi ya Italia ilikuwa imechagua mada ya kuongoza siku hii ya Wosia wa Papa Francisko wa Laudato Si, ambao kwa mwaka huu umefkisha miaka mitano  tangu kutangazwa kwake. Yote hayo yamebadilishwa kutokana na janga la virusi vya corona! Japokuwa inabakia siku ilivyo na ambayo inatazama kwa hakika mada nyeti ya joto kali linaliokumbwasayari hii. Katika harakati za mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira kwa ujumla Vatican imekuwa mstari wa mbele katika jitihada kubwa kwa hamasisho la kila wakati kutoka kwa  Papa Francisko. Na si kwa bahati mbaya hata katekesi ya tarehe 22 Aprili 2020  ambayo imeangukia katika  tukio la Siku ya  kuenzi Mama Dunia ameungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha siku hii

Hata Patriaki Bartholomew I ameonesha dhamiri kuu ya kiekolojia ambayo imepelekwa mbele kwa namna ya pekee katika jitihada za hali ya  juu ya ekolojia ya kibinadamu na ambayo ipo hata katika Hati ya kwanza ya Mafundisho jamii ya Upatriaki iliyotangazwa hivi karibuni. Katika hati hiyo yapo mambo ambayo yanakwenda pamoja na Papa Francisko na ambapo zaidi inakumbkwa  mwaka 2017 walitia sahihi ya pamoja katika Siku ya Sala kwa ajili ya kuombea Viumbe ambayo uadhimishwa kila mwaka tarehe Mosi Septemba.

Katika ujumbe wa Patriaki Bartholomew I anakumbusha zile jitihada za miaka mitatu za Upatriaki wa Costantinople kuhusu mada msingi za kiekolojia na kusisitiza kuwa Papa Fracisko ameungana na jitihada hizo tangu miaka mitano iliyopita kwa Wosia wake wa Kitume  wa Laudato Si. Patriaki anasisitiza kwamba kutokana maelewano hayo ya Papa Francisko wakiwa wameshikana mikono kama ndugu wanapaza sauti katika ubinadamu wote “ili kusimama na kupokea kilio cha uchungu kinachotokana na asili iliyo jeruhiwa, katika nyumba hii ya pamoja, mahali ambapo tumekuwa na mivutano na  siyo wahudumu wa amani na wanauchumi wake wazuri”.

Katika ujumbe wake, Patriaki aidha ananyoshea kidole chake kwa  “kiburi cha mwanadamu  ambaye hajafanya kazi kwa ajili ya ustawi wa wote, bali kafanya kwa kutosheleza ubinafsi wake mwenyewe, kusahau haki, upendo kwa pande zote,  kusaidia zaidi maskini na wasio na fursa yoyote, kuheshimiana na kiu ya uwepo wa Mungu ”. Kadhalika katika ujumbe huo unabainisha kuwa janga la ugonjwa wa virusi vya corona, umefanya kutambua udhaifu wa kibinadamu. Dunia ya leo hii inajikuta katika hali ya kubiliana na njia mbili. “Je tutakuwa na uwezo wa kukuza uhusiano wetu kijamii ulio pyaishwa, tutatambua kuwa watu wa amani, kuheshimiana na kupenda nyumba ambayo Mungu alitupatia kuilinda? Ni mawasli ya kutafakari.

Kwa mujibu wa  Patriaki Bartholomew I, “ kipindi cha maneno kimekwisha, sasa ni  kujikita katika matendo ya dhati ambayo yanaweza kuanza, kwa sababu asili na wanyama wako katika furaha ya mapumziko, wakati mwanadamu kwenye kipindi hiki anayumbishwa na kuwa na wasiwasi”. Kwa kuhitimisha ujumbe wake Patriaki anasema “kwa kupata maelewano ndani mwetu, kujigundua kwa upya  na kusaidiana mmoja na mwingine, tutapata fursa ya kupata tena maisha yetu na kushinda wakati huu na kuingia tena kwenye uhusiano mpya na Dunia na ulimwengu wote, kwa sababu kila kitu kimetolewa na Mungu kwa wema wake. Chaguo ni letu sote kwa pamoja".

23 April 2020, 12:24