Tafuta

Vatican News
Patriakoìi Bartholomew I ameandika ujumbe wake kwa waamini wa Kiorthodox ambao wamenza Juma Kuu Takatifu tarehe 12 Aprili 2020 baada ya wakristo wa Magharibi Patriakoìi Bartholomew I ameandika ujumbe wake kwa waamini wa Kiorthodox ambao wamenza Juma Kuu Takatifu tarehe 12 Aprili 2020 baada ya wakristo wa Magharibi 

Pasaka 2020:Ujumbe wa Patriaki Bartholomew I:tutaondokana na jaribio tukiwa na utambuzi wa zawadi ya maisha!

Katika fursa ya kuingia Juma Kuu Takatifu katika dunia ya Kanisa la Kiorthodox,Patriaki Bartholomew ametoa ujumbe wake akiwahakikishia kuwa wataondokana na majaribu wakiwa na ufahamu zaidi wa zawadi ya maisha.Lirutujia za kipindi cha Pasaka kwa upande wa waorthodox wa nchi za Mashariki ni baada ya wiki moja ya zile za makanisa ya Magharibi kwa mujibu wa kalenda ya kijuliani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican  

Jaribio hili litakwisha; janga hili litatoweka na majareha yatapona. Ninaomba ili sisi sote tuweza kuondokana na janga hili tukiwa tumeweza kugundua yale yote  yaliyo ya msingi katika mambo yote na kuweza kusifu na kuthamanisha thamani ya zawadi za Mungu kama ile ya afya na maisha, sadaka na kukataa haki binafsi kwa ajili ya upendo wa mwingine. Ndiyo matashi mema kutoka makao makuu ya Fanar, jijini Istanbul, kwa  wa Patriaki wa Kiekumene Bartholomew I wa Costantinopoli, akiulekeza ulimwengu wa kiorthodox ambao umeanza Wiki Kuu Takatifu.  

Juma Kuu kwa waorthodox

Waorthodox na makanisa ya Mashariki wameanza Juma Kuu Takatifu katika Dominika ya Matawi, tarehe12 Aprili 2020, ambapo ni siku saba baada ya ulimwengu wa wakristo wa Magharibi, kwa mujibu wa kalenda ya kijuliani. Patriaki Bartholomew I amesema “tunaingia katika Wiki Kuu Takatifu kwa unyenyekevu, baada ya kuhitimisha kipindi cha Kwaresima kilicho tofauti  kulingana na utamaduni wa kawaida. “Janga la virusi vya corona vimebadilisha maisha yetu ya kila siku. Makanisa yamefungwa kwa waamini wetu. Haiwezekani kupokea ekristi takatifu. Hatuoni nyuso za kaka na dada zetu katika Kanisa. Tumenyimwa cheche za uvumba”. Yote hayo ameongeza kusema, “kwa hakia kuna maana yake”. Patraki kama alivyo kuwa tayari amekwisha eleza wakati wa mwanzo wa dharura ya virusi vya corana, amepyaisha wito wake kwa kuwaalika kufuata kanuni za ulinzi na kujitenga kwa mujibu wa maamuzi ya serikali ambayo imetangaza hata kwa Wiki kuu Takatifu na katika liturujia zote kwamba hapatakuwapo na mksanyiko.  “Tubaki katika nyumba zetu kwa ajili ya kulinda na kupanua sheria hii hata katika Wiki Kuu Takatifu. Ni kwa ajili ya kulinda wote bila kutafuta sababu”.

Ikiwa wanahisi kujeruhiwa na patriaki ana huzuni

Katika ujumbe wa Patriaki, Bartholomew ameasema: “Ndugu wapendwa na wana, muwe na uhakika kuwa ikiwa mnahisi kujeruhiwa na makanisa yamefungwa, hata Patriaki wenu ana huzuni na wasiwasi. Licha ya hayo anawahakikishia kuwa hakuna njia nyingine. Katika kipindi hiki kigumu cha janga, madaktari na wanasayansi wamependekeza kufuata hatua za lazima zilizowekwa na Mataifa yote. Kwa maana hiyo  hata wao wanatakiwa kuchangia katika kulindana ndugu wote walio karibu, amesisitiza. Na zaidi “ni muhimu kusali kwa Mungu wa upendo, tabibu wa roho na wa miili yetu”, ili aweze kuwapa nguvu wagonjwa katika mateso yao na kuwasaidia kazi ngumu ya madkatari, wauguzi na wote ambao wanatoa sadaka binafsi ili kukabiliana na kipindi hiki kikubwa cha matatizo.

Janga la corona limeonesha hata nguvu na thamani ya upendo

Kipeo hiki kisichoelezeka kimeonesha nguvu na thamani ya upendo. Na mshikamano ambao ndiyo awali ya yote unabubujika kwa  ajili ya maisha ya ubinadamu na ambao unaonyesha mhuri wa neema ya Mungu Amefafanua Patriaki. Aidha amesema “Hatua hizi za kisheria zilizowekwa hazizuii imani; hazipunguzi hata kidogo kitovu cha hekalu au huduma zake takatifu katika maisha ya waamini”. Hatua hizi za vizuizi vya muda siyo maamuzi dhidi ya Kanisa. Hautazami kitovu cha utambulisho wa waamini, bali utambulisho wao tu wa kuwa binadamu anayeishi katika dunia. Kwa maana hiyo Patriaki Bartholomew kwa kuhitimisha amehimiza kwamba wataendelea kufuata kanuni hizo maalum zilizotolewa. Na kuwaalikwa waamini wawashe mwanga wa Pasaka katika mioyo yao ili waweze kugeuka kuwa mwanga wa dunia nzima.

12 April 2020, 15:04