Tafuta

Vatican News
Kukaa upekwe unasaidia mtu kujiumbia undani ile nafasi yake ya ukimya wenye nguvu zaidi na kufanya tafakari nzuri ambayo inakaribia na Mungu na maombi ya kuweza kupata kile ambacho kinaombwa. Kukaa upekwe unasaidia mtu kujiumbia undani ile nafasi yake ya ukimya wenye nguvu zaidi na kufanya tafakari nzuri ambayo inakaribia na Mungu na maombi ya kuweza kupata kile ambacho kinaombwa. 

Omnis Terra#Virus vya corona vimewakuta wakristo wamejiandaa?

Upweke ambao umelazimishwa kutokana na virusi vya Corona anasema Askofu Mkuu mstaafu wa Thomas Menamparampil wa Jimbo la Guwahati,India, unafanya kuwa na tafakari kubwa.Umelazimishwa kwa nguvu zote kusimama na kutathimini maisha ya kila siku na kugundua baadhi ya mambo yasiyo na mshiko wala tija katika maisha yetu,mfano kutafuta faida za haraka haraka,wasiwasi kupita kiasi,mitindo ya kisasa,hukumu za haraka na ubatili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Virusi vya corona vimewakuta wakristo wengi katika mabara tofauti bila kujiandaa kikamilifu, wakiwa wanahangaikia namna ya kuishi na migogoro tofauti, mingine ikiwa ya asili na mingine ya kujisababishia pia wakiwa wamefumbwa na mapendekezo nusu ukweli na kutumiwa bila utambuzi katika dunia hii. Tumekuwa kama watoto wadogo, wanaopeperushwa na mawimbi ambayo yanapiga huku na kule na upepo wa kuvuma. Hali halisi hii ya dharura imepelekea mambo mengi ya kijimii na yenye thamani ambayo watu wengi walikuwa wakitegemea na kuegemewa yamesahauliwa. Na kumbe kujitenga kwa ajili ya kufunga, au kukaa katika ukimya na kutafakari na sala ndiyo sasa vimeonekana kwa wengi katika hali hii kuwa ni vyenye maana na kufikiria maana yao ya kuishi.

Mafungo ya kiroho yamekuwa ni muhimu kwa karne zote

Ndivyo wanathibitisha katika Tovuti ya  Omnis Terra kwa tafakari kutoka kwa Askofu Mkuu mstaafu wa Shrika la wa Salesian Askofu Thomas Menamparampil wa Jimbo la  Guwahati, nchini India na muhusika mtaafu wa Ofisi ya Ujinilishaji wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia. Askofu Mkuu mstaafu  Menamparampil anadhibitisha kuwa kwa kile kiitwacho janga la  kijamii- covid-19 limepekeka baraka isiyo tarajiwa, huku akikimbusha  kwa namna ambavyo katika dunia kwa mfano mafungo ya kiroho daima yamekuwa yenye thamani kubwa na chanya katika tamaduni ya kikristo kwa karne zote japokuwa wengi kutotambua sehemu hii muhimu katika maisha. Anatoa mfano kwamba Wamonaki wa nyakati za zamani walikuwa wakifanya mafungo ya kiroho milimani, Waeremiti walikuwa wanafanya mafungo yao katika mapango, na Watafakari, walikuwa wanafanya mafungo katika misitu. Hawa walikuwa ni walinzi wa mazingira kila mahali walipokwenda, walikuwa wanalinda uoto wa asili na kuheshimu kazi ya uumbaji. Walikuwa wanaamini kuwa kukaa upekwe unasaidia mtu kujiumbia undani ile nafsi yake ya ukimya wenye nguvu zaidi na kufanya tafakari nzuri ambayo inakaribia na Mungu na maombi ya kuweza kupata kile ambacho kinaombwa na kutafuta.

Upweke wa kulazimishwa kutokana na virusi vya corona

Upweke ambao umelazaimishwa kutokana na virusi vya Corona anasema Askofu Mkuu Menamparampil unafanya utafakari sana. Umelazimishwa kwa nguvu zote kusimama na kutathimini maisha ya kila siku na kugundua baadhi ya mambo ambayo ni ya kijuu juu na yasiyo na mshiko wala tija katika maisha yetu, kwa mfano, ile tabia ya baadhi kutafuta faida za haraka haraka, wasiwasi kupita kiasi, watu na miundo na mitindo ya kisasa, hukumu za haraka, ubatili, ugomvi usio kuwa na maana, ukosefu wa huruma na hisia mbaya kwa wengine, vyote hivyo na mengine mengi kwa wakati huu havina nafasi kwa maana duniani katika dunia ya sasa ni kutafuta kile ambacho kinajenga kwa ajili ya wema wa wengine na sisi binafsi.

Katika dharura hii tumeatambua kuwa wote tunategemeana na ni wahitaji

Hali kadhalika Askofu Mkuu Menamparampil amesema  msiba au janga hili la corona limesababisha mabadiliko ya haraka ya mitazamo kwani kumekuwa na mlipuko wa ukarimu kutoka vyanzo visivyotarajiwa. Ghafla tumegundua kuwa tunaweza kuwa wakarimu, tunaweza kuwa wapatikanaji, wawajibikaji, wa kujitolea kwa hara bila kujibakiza, na kushirikiana, kusali kwa ajili ya wengine, kuwa na huruma, kutoa msaada wa haraka ... tumetambua ya kwamba tunahitajiana, tunategemeana na wote tuko katika mtumbi mmoja ambapo tunaweza hasa kuzama pamoja au kusalimika kwa pamoja. Hakuna anayejiokoa mwenyewe bila mwingine.

08 April 2020, 09:57