Tafuta

Kardinali Béchara Boutros Raï, Patriaki wa Antiokia ya Kimaroniti nchini Lebanon Kardinali Béchara Boutros Raï, Patriaki wa Antiokia ya Kimaroniti nchini Lebanon  

LEBANON:Patriaki Bechara Raï apokutana na Rais Aoun!

Akikutana katika ofisi ya Rais wa nchi ya Lebanon ofisini kwake tarehe 30 Aprili 2030,Patriaki wa Antiochia ya kimaroniti,Kardinali Béchara Boutros Raï,ametoa wito wa kuwa na mazungumzo kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini humo inayoendelea na ghasia na maandamano kutokana na mgogoro wa kiuchumi nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Patriaki wa Antiochia ya kimaroniti, Kardinali Béchara Boutros Raï, ametoa wito wa kuwa na mazungumzo kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Libanon ambapo tarehe 30 Aprili 2020 amepokelewa katika ofisi ya kiongozi wa Nchi hiyo Rais Michel Aoun. Katika nchi hiyo kiukweli, mandamano  yanaendelea kwa miezi hivi, dhidi ya kuanguka kwa thamani ya kifedha  na kuongezeka kwa gharama za maisha.  Tangu maandamano hayo yaanze yamekwisha sababaisha hata vifo na majeruhi wengi. Katika kipindi cha siku nne zilizopita, mapigano yamejitokeza hasa huko Tripoli na Saida, mahali ambapo waandamanaji walishambulia hata matawi kadhaa ya Benki Kuu.

Mbele ya mambo yote hayo, Patriaki Raï ameshauri kuwa na utulivu na mazungumzo. Patriaki amesema, "Hatukubali kuona kile tukionacho, yaani mashambulizi ya mali za watu binafsi na umma, huku akitaja maneno ya  mwelekeo wa safari kuwa:Tunaunga mkono hitaji la serikali kwa sababu nchi haiwezi kuishi kwa utulivu bila taasisi". Kwa  njia hiyo amesitiza na kusema:“Ninawaalika kila mtu amsikilize mmoja na mwingine kwa madhumuni ya kutetea nchi nzima na siyo masilahi ya mtu binafsi”.

Mgogoro wa kisiasa nchini Lebanon ulianza kunako Oktoba 2019 wakati mzozo maarufu ambao haujawahi kutokea wa watu ulipoibuka  na zaidi kiini ni  mgogoro wa kiuchumi na kifedha. Maandamano ya watu yalisababisha kuanguka kwa serikali ya Saad Hariri wiki chache baadaye. Kuanzia tarehe 21 Januari 2020, waziri mkuu mpya ni Hassan Diab ambaye ameweka katika ajenda yake  kufanya mapambano dhidi ya ufisadi.

30 April 2020, 17:04