Tafuta

Vatican News
2020.04.25 Askofu John Oballa Owaa katikati,kushoto kwake askofu Kivuva na kulia  kwake ni askofu Rotich wa Kenya. 2020.04.25 Askofu John Oballa Owaa katikati,kushoto kwake askofu Kivuva na kulia kwake ni askofu Rotich wa Kenya. 

Kenya#wito wa maaskofu kwa serikali:kusaidia watu waliokumbwa na mafuriko!

Tume ya Haki na amani ya Baraza la Maaskofu nchini Kenya kupitia Rais wake Askofu John Oballa Owaa,imetoa wito kwa Serikali kutenga rasilimali muhimu ili kusaidia idadi ya watu ambao wamekumbwa na mafuriko kwenye maeneo ya Kisumu Magharibi mwa nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni waathirika 28 na makumi waliopotea kufutia na mafuriko ambayo yamekumba ndani ya wiki hii katika kanda ya Magharibi ya Kenya. Hali ngumu inatazama mji wa Kisumu na pembeni mwa Ziwa Victoria, mahali ambapo kuna hatari hasa ya mabwawa kuporomoka wakati mvua kubwa zikiendelea kunyesha bila kukoma.

Mbele ya janga hili la asili, Tume ya Haki na amani ya Baraza la Maaskofu nchini Kenya imetoa wito kwa Serikali ili kutenga rasilimali muhimu katika kusaidia idadi ya watu. Kutokana na hili pia maaskofu wametoa wito kwa wananchi wenyewe, ili wawe na mshikamano na wale walioathiriwa zaidi na mafuriko, pamoja na wasio na makazi, kwa sasabu  tayari walikuwa katika shida kutokana na janga la virusi vya corona.

Kwa mujibu wa Askofu John Oballa Owaa, Rais wa Tume ya Maaskofu ya Haki na amani anasema ni lazima na  haraka kutengwa rasimilia inayotosha ili kuingilia kati mahitaji ya dharura ya watu. Na wakati huo huo,kufuatia na Janga la Covid-19 pia maaskofu wanawasihi waamini wote kuheshimu maelekezo yaliyotolewa na mamlaka ili kuepuka kupoteza maisha ya binadamu na mali, ikiwa ni pamoja na usalama wa jumuiya hasa inayoanzia na hao.

Zaidi katika mji wa Kisumu,maeneo yaliyokubwa na mafuriko ni Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet, Bungoma na Homabay.  Zaidi ya familia 400 zimerundikana kwa pamoja kwani mafuriko yametapanya nyumba nyingi, na kufanya barabara kuwa ngumu  kwa namna hiyo shughuli za uokoaji ni ngumu pia!

25 April 2020, 15:22