Tafuta

Vatican News
Washonaji katika kipindi cha virus vya covid-19 jijini Accra nchini Ghana.Katika ujumbe wa Pasaka wa Maaskofu nchini humo wanahimiza waamini kutunza imani na matumaini kwa Mungu Baba. Washonaji katika kipindi cha virus vya covid-19 jijini Accra nchini Ghana.Katika ujumbe wa Pasaka wa Maaskofu nchini humo wanahimiza waamini kutunza imani na matumaini kwa Mungu Baba. 

Ghana #coronavirus.Ujumbe wa Pasaka:Tutunze imani na matumaini kwa Mungu!

Maaskofu nchini Ghana katika ujumbe wao wa Pasaka 2020 katika mazingira ya virusi vya corona,wanawaalika waamini watunze imani kwa Mungu na kutazama wakati ujao kwa matumaini.Onyo pia ni kuacha tabia za kuchukua fursa ya hali hii katika kutaka kupata pesa zaidi,kwa kuongeza bei za bidhaa za chakula na vifaa vya afya nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kutunza imani na kutazama wakati endelevu kwa matumaini, ndiyo ujumbe wa kuwatia moyo wa Baraza la Maaskofu nchini Ghana (Gcbc). Lengo la ujumbe wao kwa waamini ni kwa ajili ya maadhimisho ya Siku Kuu  ya Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyeteswa, akafa na kufufuka katika wafu. Pasaka ambayo kwa namna ya pekee mwaka inaangukia katika janga la virusi vya corona vilivyo kwisha shambulia na vinavyoendelea kuwakumba nchi nyingi za Afrika na duniani kote kwa ujumla kwa kusababisha vifo na mabadiliko ya maisha ya watu wote duniani.

Lakini mbele ya kuwa na hofu na wasi wasi mkubwa wa dharura ya kiafya, ambayo inazuia waamini kushiriki kimwili katika maadhimisho ya Pasaka ili kuzuia maambukizi zaidi  ya virusi vya corona, maaskofu nchini Ghana wanatoa ushauri kwa waamnini kuwa na imani kuu  kwa Mungu ambaye anaweza kuondoa mzizi huo kabisa wa ugonjwa.  Kupitia tovuti ya Baraza la maaskofu  wa Ghana (Gcbc) wanatoa  hata wito wa“kusali ili ufufuko wa Kristo uweze kufanya kila kitu kuwa kipya kwetu sisi”.

Hata kama maambukizi ya  Covid -19 imewaambukiza  zaidi ya milioni moja na nusu ya watu, duniani na fifo vya watu karibia 100elfu, nchini Ghana imefikia maambukizi ya watu 287, kwa maana hiyo, Baraza la Maaskofu wa Ghana( Gcbc) wanawaalika waamini “ kutazama wakati ujao kwa matuimaini na imani” kwa sababu “ hampaswi kuwa na mashaka ya uwezo wa Mungu ambaye anaweza kutusaidia kushinda janga la sasa. Lazima kuendelea kutunza imani yetu na konyesha matumaini katika Mungu Baba ambaye alitoa Mwanaye ili kuokoa ulimwengu”. Wamehimiza.

Hata hivyo maaskofu pia  wanatoa tamko  wakiomba kuwa na “umoja na ushirikianao ili kuweza kukabiliana na janga hili kama familia moja ya kibinadamu na katika kuendelea kuchukua hatua zote zilizotolewa za kiafya ambazo ni msingi wa kuzuia usambaaji wa ugonjwa huu”. “Ikiwa kuna jambo fulani ambalo tumefundishwa na covid-19,   wanaandika maaskofu ni ule wito wa umoja yaani upamoja ambao hauna ubaguzi wa rangi, dini, jinsia, kabilia au kijamii” kwa maana hiyo, maaskofu, wanahimiza sera zote za kisasa, wawe na umoja katika kufanya kazi kwa umoja na roho ya ushirikiano na kama wazalendo bila kuingiza siasa katika janga hili kwa maana “virusi vya corona, havina rangi na wala wadau”. Aidha zaidi, kwa kila mtu, awe mwamini  au la, kwa  kipindi hiki ni  muafaka kuweza kutambua thamani ya udugu na kudumisha mahusiano ya dhati na wengine”.

Hatimaye  maaaskofu kwa kutathimini hali halisi nchini Ghana mahali ambapo katika muktadha wa janga umesababisha tayari kuongezeka kwa bei za bidhaa za chakula na vifaa vya kiafya, Kanisa mahalia linatoa onyo: "Lazima tuache tabia za kuchukua fursa ya hali hii kupata pesa zaidi, au fursa za kuddhulumu wengine kwa bei  za juu; siyo wakati muafaka wa kupata faida ya fedha nyingi na kumbe ni wakati wa kusaidia mahitaji na mateso ya wengine". Aidha wameongeza kuandikia: "Hasa  zaidi katika  wakati huu wa mateso, Mungu anatualika tujiangalia ndani ya maisha yetu ili kukwepa dhambi, ambayo ni virusi vya hatari zaidi katika mwili na roho”.

11 April 2020, 12:36