Tafuta

Vatican News
Marais wa Comece na Cec wanatoa shukrani kwa madaktari na wahudumu wote wakati huo huo wakiombwa watu wote wa Ulaya kuendelea na mshikamano. Marais wa Comece na Cec wanatoa shukrani kwa madaktari na wahudumu wote wakati huo huo wakiombwa watu wote wa Ulaya kuendelea na mshikamano.  (AFP or licensors)

EUROPE #Coronavirus:wito wa Comece na Cec:Tubaki tumeungana!

Marais wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na Mabaraza ya Makanisa wanasema katika ujumbe wao wa pamoja kuwa sasa ni kipindi cha kuonesha umoja huo na ambao usidhibitiwe na vikwazo wala hofu,badala yake ni kuwa na mshikamano katika kupambana na janga la covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa sasa ni kipindi cha kuungana na wote kuonyesha jitihada za pamoja katika mpango wa Ulaya na thamani ya pamoja ya Ulaya ya mshikamano ambapo umoja huo  usiwekewe vizingiti, hofu na utaifa. Ndiyo wito wa nguvu katika kuwataka uwajibikaji wa kushirikishana ambao umetolewa tarehe 2 Aprili 2020  kwa Bara la Ulaya kutoka wa Marais wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (COMECE) na Baraza la Makanisa Ulaya  CEC,  kufuatia na muktadha wa janga la Covid-19.

Kusaidia mifumo ya kiafya iliyo midhaifu duniani

Kwa mujibu wa Vyombo hivi vya kidini yaani Cec na Comece  kupitia marais wake wanasema  kielelezo cha dhati cha mshikamano kinaweza kuwa cha kweli  kushirikishana na kuwa na uzito wa kutunza wazee, kubadili zana za kiafya kwa haraka, lakini pia hata kuchukua hatua za ubunifu ambazo zinaweza kusaidia kutoa hisia mbaya za kijamii, kiuchumi na kifedha kama vile  kupitia vyama vya ushirika vya kimataifa na usaidizi wa kibinadamu katika kuongeza nguvu za kusaidia mifumo ya kiafya iliyo mibovu katika kanda  zenye kuhitaji zaidi duniani.

Ukaribu na shukrani kutoka kwa marais wa Comece na Cec

Tamko hili limetolewa na Kardinali Jean-Claude Hollerich SJ, na mchungaji Christian Krieger ambao wanaonesha pia ukaribu sana kwa sala katika Makanisa yote ya Ulaya ambayo yako yanateseka na janga hili na kwa ajili ya waathirika wengi, lakini pia wanatoa shukrani kubwa kwa madkatari, wauguzi, watu wa kujitolea na watoaji huduma zote; vyombo vya kisheria na utekelezaji, watu wanaojihusisha na haki ambayo inasaidia sana leo hii jirani ili  aweze kujuliwa hali na kupewa joto la upendo kwa watu wote waliokumbwa  katika usaidizi wa kichungaji.

Viongozi wa dini wanatia moyo watu wote  

Marais wa Comece na Cec aidha wanatambua na kutoa shukrani kwa kuanzisha mambo mengi binafsi na ya pamoja ambayo yanaendelea kuonesha mitindo mbali mbali ya mshikamano na namna mpya ya kushirikishana kwa kutoa zaidi mambo ya lazima kijamii na kuwatia moyo wanasisasa wa Jumuiya ya Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuendelea kutenda kwa njia iliyoamuliwa, iliyo wazi, yenye huruma na ya kidemokrasia.

02 April 2020, 13:12