Tafuta

Vatican News
Dr. Getrude Pangalile Rwakatare, Mchungaji, Mwanasiasa na Mwana harakati katika maendeleo ya elimu nchini Tanzania amefariki dunia tarehe 20 Aprili 2020. Dr. Getrude Pangalile Rwakatare, Mchungaji, Mwanasiasa na Mwana harakati katika maendeleo ya elimu nchini Tanzania amefariki dunia tarehe 20 Aprili 2020.  (AFP or licensors)

Dr. Getrude P. Rwakatare amefariki dunia! Mwanamke wa shoka!

Dr. Gertrude Pangalile Rwakatare alikuwa ni Mchungaji mkuu wa Kanisa la Mlima wa moto, huko Mikocheni B, Dar es Salaam. Alikuwa ni mwanasiasa na mwanachama wa Chama cha Mapinduzi, CCM na Mbunge wa viti maalum huko Mvomero kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2015 na baadaye aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge. Alizaliwa tarehe 31 Desemba 1950. RIP!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Maana ya Kikristo ya Kifo imefunuliwa katika mwanga wa Fumbo la Pasaka, yaani: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu, ambaye ndani yake mna tumaini na chemchemi ya maisha na uzima wa milele. Kwa Mkristo siku ya kifo huanzisha, mwisho wa maisha yake ya Kisakramenti: Nangojea ufufuko wa wafu na uzima wa ulimwengu ujao! Watanzania wengi wameguswa na kusitikishwa na kifo cha Mchungaji Dr. Gertrude Pangalile Rwakatare kilichotokea Jijini Dar es Salaam, tarehe 20 Aprili 2020 kwa shinikizo la damu, kadiri ya taarifa kutoka kwa mwanaye Mutta Rwakatare aliyenukuliwa na vyombo mbali mbali vya habari.

Dr. Gertrude Pangalile Rwakatare alikuwa ni Mchungaji mkuu wa Kanisa la Mlima wa moto, huko Mikocheni B, Dar es Salaam. Alikuwa ni mwanasiasa na mwanachama wa Chama cha Mapinduzi, CCM na Mbunge wa viti maalum huko Mvomero kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2015 na baadaye aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge. Itakumbukwa kwamba, Dr. Gertrude Pangalile Rwakatare Alizaliwa tarehe 31 Desemba 1950. Kwa ufupi kabisa, kunako mwaka 1987 Dr. Rwakatare akaanzisha mtandao wa Shule za St. Mary kuanzia shule za awali, sekondari hadi Chuo. Alichangia sana kuinua sekta ya elimu nchini Tanzania. Kunako mwaka 1995 akaanzisha Kanisa la Mlima wa Moto, huko Mikocheni B ambalo limekuwa na waamini wengi hasa katika Jiji la Dar es Salaam. Kunako mwaka 2006 akaanzisha Kituo Kikubwa cha Watoto Yatima kilichokuwa na uwezo wa kuwapokea na kuwalea watoto 700. Kituo hiki kinajulikana kama “Bright Future”.

Dr. Rwakatare

 

20 April 2020, 13:27