Tafuta

Vatican News
Pasaka katika kipindi cha janga la corona tusheherekee kama Kanisa la nyumbani kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Vienna nchini Austria Pasaka katika kipindi cha janga la corona tusheherekee kama Kanisa la nyumbani kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Vienna nchini Austria 

Austria#coronavirus Kard,Schönborn:Tusherekee Pasaka kama kanisa la nyumbani!

Tendo la kutotembelewa na wazazi,bibi na babu au marafiki ni muhimu kwa kulinda maisha mwaka huu ambapo liturujia zote za Juma kuu na Pasaka vinafanyika bila waamini makanisani.Waamini wanaadhimisha Pasaka kama Kanisa la nyumbani.Wakumbuke maneno ya Yesu asemaye:“wawili au watatu waunganapo kwa jina langu mimi nipo kati yao”.Ni kwa mujibu wa Kardinali Christoph Schönborn,wa jimbo la Vienna.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mwaka huu wakristo wengi wanapaswa waadhimishe lirurujia na ibada za Pasaka kama Kanisa la nyumbani, ikiwa na maana ni wale ambao wanaishi ndani ya nyumba peke yao. Tendo la  kutotembelewa na wazazi, bibi na babu, au marafiki ni muhimu kwa sababu ya kulinda maisha. Ndiyo wito uliotolewa na Kardinali Christoph Schönborn, Askofu kuu wa Vienna na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Austria ambaye amefafanua kuwa vizuizi vya sasa vilivyowekwa kwa umma ili  kubaki ndani ni jambo kubwa na wakati huo huo lenye  maana ya sadaka. “ Ikiwa tutajidhibiti sasa, ni busara  na kwa ajili ya kujilinda na kwaajili ya kulinda jirani. Ni kwa njia hiyo tu, tunaweza kweli kuishi pamoja kikamilifu ile imani yetu”,  amesema Kardinali Schönborn.

Kwa sasa inastahili kufuata sheria zilizowekwa kwa umma na kwamba maparokia na makuhani waadhimishe vipindi hivi bila kuwa na waamini na hivyo makanisa yakiwa bila waamini . Waamini wafuatilie ibada zote ka njia ya vyombo vya habari na mitandao yote iliyopo kushiriki ibada hizi kuu takatifu ya ukombozi wa Bwana.

 “Tunaweza kufanya hivyo hata kulingana na kile ambacho Yesu mwenyewe alisema: palipo na wawili au watatu walioungana kwa jina langu, mimi niko akati yao”, ameeleza Kardinali. Hata hivyo Katikati ya mwezi wa tatu, Baraza la Maaskofu nchini Austria waliunda Tume kuu yenye kazi ya kukabiliana na masuala yote muhimu yanayohusiana na dharura kufuatana na maambukizi ya virusi vya corona. Kikundi cha kazi hiyo Kardinali Schönborn, pia yumo pamoja na Askofu Mkuu Franz Lackner, wa jimbo kuuu  Salisburg, Askofu  Manfred Scheuer, wa Jimbo la  Linz na Askofu Wilhelm Krautwaschl, wa jimbo la  Graz.

Tume hiyo ilifanya kikao chake tarehe 8 Aprili 2020 kwa njia ya video na mwisho wa mkutano huo, askofu mmojawapo wa Austria alithibitisha juu ya kuwasiliana na serikali kima mara ili kujifunza namna ya itakavyokuwa kuanza shughulizi. “ kwa sasa, maaskofu wako wanafanyia kazi juu ya mango ambao unapaswa baadaye kuhakikisha kazi taratibu”.

Hatimaye Askofu Mkuu wa Vienna alitoa shukurani kubwa kwa nidhamu na uvumilivi uliooneshwa kwa siku hizi za vizuizi kwa upande wa raia  ni matumaini yake kuwa uvumilivu wa lazima utasaidia zaidi kuweza kurudia hali ya kawaida kwa wote. Na kama Kanisa, ni matashi yao kuwa baada ya Pasaka, wanapata uwazi zaidi ni namna gani ya kuweza kukuabiliana na wakati ujao.

11 April 2020, 09:09