Tafuta

Vatican News
wasanii maarufu wa muziki na hata walio wadogo wanatafuta kuhamasisha watu katika kipindi hiki cha lockdow.Ndivyo hata kikundi cha vijana katoliki Australia wanafanya kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wasanii maarufu wa muziki na hata walio wadogo wanatafuta kuhamasisha watu katika kipindi hiki cha lockdow.Ndivyo hata kikundi cha vijana katoliki Australia wanafanya kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook 

Australia#coronavirus Tamasha la vijana wanamuziki kupitia Facebook:imani,furaha na matumaini katika nyumba!

Nchini Aistralia katika kipindi hili cha janga la virusi vya corona,vijana wanamuziki katoliki wameandaa tamaasha la kusifu kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa wao wa facebook ili kudumisha imani,furaha na matumaini kwa watu wanaolazimika kukaa kajumbani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni wiki tatu sasa wanamuziki vijana katoliki waitwao Parramatta, huko Australia kila siku ya Jumatano wako  mubashara katika ukurasa wa Facebook huku wakifanya tamasha la muziki kwa dakika 30, tamasha walilolipatia jina  “Worship Wednesday” kwa ajili ya kudumisha imani, furaha na matumaini” kwa watu ambao wamelazimika kukaa nyumbani (lockdown)  kutokana na janga la virusi vya corona.

 “Il Worship Wednesday” imekuwa moja ya mambo ya kwanza tuliyowaza wakati sheria ya vizuizi vya kutoka nje kutokana na Covid-19 ilipoingia”, anasema James Camden, Mkurugenzi wa Vijana katoliki-Parramatta, kwa mujibu wa Gazeti la Cathnews, chombo cha mawasiliano cha huduma ya Baraza la Maaskofu wa Australia. Aidha “vipindi hivi vya muziki na tafakari vimewawezesha kutangaza sifa kwa Bwana na imani yao hata kwa njia ya mitandao. Ni fursa ya kufanya iweze kukua imani, hata kuweza kuwafanya wanamuziki mahalia  kuwa na ile misingi ya imani katika jumuiya zao za maparokia na ambazo kwa ukarimu wanaendelea kutoa talanta zao katika kipindi hiki kigumu”.

Katika Tamasha la kueneza sifa  kwa Bwana  kila Jumatano, wameichagua ili kuwapa moyo waamini walio wengi wasisimame katikati ya wikimì, na ili kuwa pamoja,  kutafakari kwa pamoja na binafsi watu wote ambao wako nyumbani. Kwa njia hii anasisitiza ni vema kupokea kwa ukarimu siku hiyo iliyochaguliwa ya “Worship Wednesday”.

Tamasha hizi zinaandaliwa na Vijana katoliki waitwao Parramatta  na zaidi ya kufanya muziki wao kuwa mzuri hii ni fursa kwao hata ya kusali, kwa hiyo wanatafuta namna ya kuwa na uwiano sawa. Si kwamba wako  katika studio zenye taa  na vipaza sauti vya kitaalam, la! Wao kila mmoja akiwa amekaa kwenye subule nyumbani kwao. Lengo ni kutaka kuunda uzoefu wa imani ambao unaweza kumwilisha kiroho kwa wiki nzima  ya tafakari kwa mujibu wa Camden, mkurugenzi wa wanamuziki vijana katoliki nchini Australia.

22 April 2020, 11:48