Tafuta

Vatican News
Baraza Katoliki kitaifa la watu wa asili na visiwa vya Torres nchini Australia  wanashauri jumuiya zao kutumia muda huu wa karantini kutafakari ujumbe wa Mtakatifu Yohane Paulo II wa mwaka 1986 Baraza Katoliki kitaifa la watu wa asili na visiwa vya Torres nchini Australia wanashauri jumuiya zao kutumia muda huu wa karantini kutafakari ujumbe wa Mtakatifu Yohane Paulo II wa mwaka 1986 

Australia#coronavirus:karantini iwe fursa ya tafakari ya Mt. Yohane Paulo II!

Baraza la ushauri Katoliki la Watu wa asilia na Visiwa vya Torres wametoa ushauri wa kwa jumuiya zao ili kupokea fursa ya kipindi cha upweke kijamii kutokana na virusi vya corona wakiongozwa kiroho na maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II aliyowaeleza alipofanya ziara nchini huko kunako 1986.Shughuli zilizo katika Halmashauri ni mchakato wa safari ya sakramenti,utunzaji wa kichungaji,msaada kwa maskini,wagonjwa na wafungwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa kupokea kipindi cha upweke kijamii kufuatia na dharurua ya kiafya kutokana na virus vya corona  ni muhimu kujikita kwa upya kuongozwa na maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II aliyowambia watu wa asili na wa visiwa vya Wilaya ya Torre nchini Australia kunako mwaka 1986. Na hii i kwa sababu, wakati ule ujumbe ulisikia kama wa kimapunduzi, lakini kwa wakati huu, ujumbe huo unatoa matumaini, nguvu na utambuzi wa kuwa taifa moja dhidi ya tishio la hatari ya pamoja. Ni mwaliko kutoka kwa Baraza Katoliki kitaifa la Watu wa Asili na visiwa vya Torres wakitoa ushauri jumuiya zao.

Katika ujumbe wa 1986, Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa wamewaalika wakatoliki wa asiache  kuelekeza tabia yao ya upatanisho ili kuweza kutoa mchango wa kukuza taifa. Ni kwa njia hiyo tu mtaweza kuboresha mchango wa ndugu kaka na dada katika taifa hili. Ninyi ni sehemu ya Australia na Australia ni sehemu yenu. Kanisa lenyewe la Australia halitakuwa Kanisa timilifu kwa mujibu wa mapenzi ya Yesu ikiwa hamtaweza kutoa mchango wa maisha yake na ikiwa mchango huo hautapokelewa kwa furaha na wengine”.

Mchango huo kwa mujibu wa Mtakatifu Yohane Paulo II , unapelekea ule  mhuri wa Roho Mtakatifu, kwani anasema: Wakati wote wa kipindi cha Roho wa Mungu amekuwa nanyi. Kuota kwenu ndoto ni namna yenu ya  kugusa fumbo la Roho wa Mungu katika ninyi na katika kazi ya uumbaji. Mnapaswa kuendelea kuongeza bidii ya kumfikia Mungu na kudumu katika tabia ya maisha yenu.” Katika kipindi hiki cha dharura ya Corona, Baraza katoliki la kitaifa la watu wa asilia na watu wa Visiwa  vya Torres wanapeleka mbele huduma kwa watu wenye kuhitaji zaidi wakijaribu kutoa mafundisho muhimu binafsi kwa ajili ya namna ya kujitunza na usafi hata kuwasaidia wazee kwa njia ya mawasiliano ya Skype.

Aidha wamejikita katika huduma ya kuweka orodha anauazi za barua pepe ambayo itasaidia kutoa sasisho na habari muhimu kuhusu dharura ya Covid-19. Katika suala hili, ujumbe unasema  “Tunajaribu kusaidia jamuiya zetu kwa kushirikisha habari muhimu ili  kukabiliana na janga hili. Sisi sio wataalamu wa madaktari, lakini tunashauri kila mtu kufuata mwongozo uliowekwa na serikali na mamlaka ya matibabu. Kwa upande wetu, tunaomba jamuiya zetu zote ziwe salama: makuhani, familia na jamuiya zote ziko kwenye mawazo na sala zetu katika kipindi hiki kigumu na cha changamoto”.

Baraza kuu la Kitaifa la Waasili na Visiwa vya Torres (NATSICC) ni kikundi cha ushauri cha juu kabisa cha Maaskofu wa Australia kuhusiana na masuala yanayohusu jamuiya asilia, ambayo ni zaidi ya Wakatoliki 130,000. Kati ya shughuli zilizo ndani ya uwezo wa Halmashauri kuna mchakato wa safari ya sakramenti na utunzaji wa kichungaji, msaada wa hisani kwa maskini na msaada kwa wagonjwa na wafungwa.

06 April 2020, 12:57