Tafuta

Vatican News
Matatizo ya virusi vya corona ni makubwa nchini Afrika Kusini hasa kwa upande wa maskini zaidi na wahamiaji na wakimbizi ambao hawana chakula. Matatizo ya virusi vya corona ni makubwa nchini Afrika Kusini hasa kwa upande wa maskini zaidi na wahamiaji na wakimbizi ambao hawana chakula.  (AFP or licensors)

Afrika Kusini#coronavirus:Jitihada za Kanisa dhidi ya umaskini

Katika kitongoji cha pembeni mwa jiji la Johannesburg,Afrika Kusini Mapadre Wascabrini wa Parokia ya Mtakatifu Patrick wanasaidia maelfu ya maskini na wahamiaji waliobaguliwa na msaada wa serikali.Hata hivyo kazi kubwa ipo kwa sababu hawezi kusaidiwa na watu wa kujitolea kwa sababu watu wanaogopa na wanaparokia wao wanaogopa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila siku mama wengi, Watoto, wanaume vijana na wazee wanajipanga katika mstari usioisha mbele ya Kanisa wakilia na kulalamika kutokana na njaa. Polisi pia ameaogopesha na kuwaomba wafunge kila kitu lakini je inawezekanaje kuwaacha wenye kuhitako msaada katika kipindi hiki kigumu? Haya yamethibitishwa na adre Velasquez katika mtaa wa La Rochelle jijini  Johannesburg, nchini Sudan Kusini. Katika maelezo yake Padre Pablo Velasquez, anabainisha jinsi walivyosimamisha maadhimisho asubuhi katika Kanisa lao milango ikiwa imefungwa baada ya kusikia malalamiko ya vilio vya uchungu usioisha vya watu walio kuwa nje.

Tendo la kutoka nje waliona msululu mkubwa sana wa watu ambao walikuwa wanaomba chakula. Ameeleza Padre Pablo Velasquez mmisionari wa Shirika la Wascabrini akionesha majonzi makubwa kwa kizuizi cha kijamii na kiuchumi kilichotokana na janga hili la corona nchini kote na ambacho kina athari kubwa kwa watu hasa walio katika madaraja ya umasikini zaidi, kwa wahamiaji na wakimbizi, na mara nyingi wanapuuzwa na kusahauliwa. Aidha amebanisha kuwa kwa muda mfupi idadi ya wale ambao wanaomba msaada katika utume wao wa kiscalabrini imeongezeka sana. Kuna maelfu ya wahamiaji wasio na kazi ambao wanajitahidi kwa ugumu kuwasaidia.

Katika Parokia ya Mtakatifu Patrick katika kipindi hiki cha janga la corona imegeuka kuwa moja ya sehemu ya kukimbilia kwa wale wasiokuwa na kitu au wamepoteza kila kitu. Katika kitongoji cha La Rochelle, eneo la kutoa huduma kwa Mapadre wa kimisionari Wascalabrini, kuna jamuiya kadhaa za wahamiaji kutoka katika nchi ishirini tofauti. Hata hivyo Programu za misaada zilizotolewa na serikali kwa raia wa Afrika Kusini ili kupambana na athari za virusi haziwahusu wahamiaji,ambapo mealaani vikali Padre  Baba Velasquez. Kwa mujibu wake anabanisha kuwa waliotengwa hawawezi kufanya chochote isipokuwa kuwaelekea makuhani wa Parokia ya Mtakatifu Patrick. Mara ya kwanza kulikuwa ni mia tano lakini kesho yake watakuwa zaidi kwa sababu uvumi wa sauti ambao umekwisha eneoa maana umasikini ni mkubwa sana amesisitiza.

Anaye saidia Parokia ili kusaidia  masikini ni yule mwenye moyo mzuri tu kwa watu binafsi. Padre  Velasquez analitaja kampuni moja la uwekezaji huko Johannesburg, ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa sana na baadhi ya maparokia  wengine wao tu. Vile vile masikini wengi waliitwa na taasisi lakini walipogundua kuwa ni wahamiaji waliawambiwa wao ni wageni na hawana haki ya kupata  ruzuku hizo.  Na kadri ya kizuizi kikiendelea nchini kote, kiwango cha umaskini kitaongezeka sana.Amebainisha Padre. Kuna pia hatari ya maambukizi ambapo Padre Velasquez anafahamu hili, kiasi kwamba  anakubali kuwa katika msululu wa mstari wanaojipanga mbele ya parokia yao, wachache wanaheshimu sheria za kupambana na maambukizi. Hii ni kutokana kwamba ni wachache waliovaa barakoa na wengine hawana kwa sababu hawawezi kumudu gharama. Halafu wengine wengi wanasema ni bora ya hatari ya kufa na virusi  badala ya kufa kwa njaa.

Hatua za kuzuia  hata hivyo zinakuwa ni shida kubwa kwa wamisionari hawa. Parokia ya Padre Velasquez iko kati ya vizuizi vya maambukizi ya corona na wakati huo huo kuna hukosefu wa nyundo na msumari katika hatua za kisheria ili kusaidia wale ambao wamepoteza kazi na mkate. “Kwa jina la Mungu na Kanisa sote tunasaidia. Lakini sasa sisi wenyewe hatuwezi kusaidiwa na watu wa kujitolea kwa sababu watu wanaogopa, wanaparokia wetu wanaogopa”.

Lakini kwa upande wa Padre Velasquez hofu sio sababu ya kukata tamaa kwa mfano Wiki iliyopita polisi walifika parokiani na kuona kwamba wananasaidia masikini, waliwapigia  kelele kwana hawana  vibali, lazima wafunge kila kitu! Ndiyo anasema walikuwa wanajua kuwa wanakiuka sheria lakini hawawezi kuacha watu wafe kwa njaa. Tunajua tunakiuka sheria, lakini hatuwezi kuwaacha watu wafe. " Kufuatia na ujasiri huo, Parokia ya Mtakatifu Patrick kwa sasa imepata ruhusa ya kusaidia maskini huko Johannesburg. Kiukweli siyo kwa kanisa, ambalo lazima libaki limefungwa, lakini kwa umoja wa upendo na hisani ambayo Mtakatifu Vincenti wa Pauli, ndiyo umekuwa ujanja mdogo wa kujaribu kuendeleza kuokoa maisha kwa jina la Mungu na Kanisa.

 

24 April 2020, 13:25