Tafuta

Vatican News
Rais Emmerson Mnangagwa akihutubia taifa kuhusu virusi vya Corona Rais Emmerson Mnangagwa akihutubia taifa kuhusu virusi vya Corona  (ANSA)

Zimbabwe:Makanisa ya Zimbabwe yahimiza majadiliano ya pamoja!

Katika mahojiano na mchungaji Kenneth Mtata,kiongozi wa Kanisa la Kiluteri na Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa nchini Zimbabwe (ZCC),amelezea juu ya hali halisi nchini humo kuwa ni ngumu.Inahitajika kuwa na matendo ya dhati ya pamoja katika majadiliano kwani baada ya ushindi wa Rais Mnangagwa matarajio ya demokrasia ya kweli imekuwa kinyume.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Makanisa Katoliki wako katika hali ngumu hasa katika kujikia kwenye  matendo ya pamoja ya majadadiliano.Baada ya uchaguzi sisi sote tulikuwa tunafikiri tumekabiliana na ukiukwaji wa haki na kuanza upya kupitia njia ambazo zinaelekeza wakati ujao wa kidemokrasia ya kweli. Kwa hali halisi, utafikiri kwamba kabla ya miaka miwili kila kitu kimetawanywa na upepo. Ukiukwaji unaendelea, kuna vifo, kukamatwa ovyo na mateso mengi. Katiba mpya, iliyopitishwa kunako 2013, bado inangojea kutekelezwa, kwa maana kuna ucheleweshaji kwa nia  ya kuisubirisha ili kuongezea nguvu ya serikali. Ndiyo ufafanuzi katika  mahojiano na shirika la habari za Kimisionari (Fides) na Mchungaji  Kenneth Mtata, kiongozi wa kikristo katika kanisa la Kiluteri na Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa nchini Zimbabwe (ZCC). Yeye kama mwakilishi katika  Jukwaa la Makanisa ya Waprotestanti ambayo yanatoa mchango wa kujikwamua katika majadiliano na raia katika awamu muhimu ya historia ya kitaifa nchini Zimbabwe..

Safari ya mchakato wa Zimbabwe kuelekea demokrasia, karibu kwa miaka miwili baada ya uchaguzi wa kihistoria ambao ulifunga kipindi kisicho na mwisho cha utawala wa Robert Mugabe kwa aliyeshika  madaraka kwa miaka 38, bado kuna matata sana! Takwimu mbaya  zinaoneshwa na ripoti ya “Granaio Afrika”, ambayo inaonesha hali hiyo kuondoa miaka ya udikteta kwa kuharibiwa kwa suala la haki, na kusababisha ubaya katika nchi hiyo. Karibu milioni 17 ya wakazi ambao walikuwa wametelemka  katika kiwanja kwa wingi huku wakiadhimisha mwisho wa utawala  mgumu na mategemeo ya kuwa mshindi  Emmerson Mnangagwa, Kiongozi wa chama cha Zanu-Pf  ambacho ndicho kilikuwa cha Mugabe katika uchaguzi wa Julai 2018, walitegemea uwe ndiyo mwanzo mpya wa demokrasia na matumaini, lakini kwa bahati mbaya wanajikuta wanakabiliana na hali ngumu, ya ukosefu wa ajira ikiwa ni asilimia 95%, mfumko wa bei zaidi ya 500%; zaidi ya asilimia  70% ya idadi ya watu wakiwa  chini ya umaskini wa kukithiri, au kutokuwa na utulivu mkubwa wa kisiasa na haki za zilizokanyagwa.

Takwimu za kijamii na kiuchumi zinabainisha  juu ya hali iliyo karibu na kulala chini kabisa . “Kila mtu alitarajia kufufua uchumi kwa kuzingatia rasilimali za nchi yetu, lakini vigezo vya uchumi vimezidi kuwa vibaya katika miaka miwili iliyopita na mfumko uko karibu na 600%. Zaidi ya hayo, vyama viwili vilivyowakilishwa havishirikiani na hali inakuwa ya wasiwasi kila siku, na viwango kuwa vya juu vya ufisadi “ amesisitiza mchungaji” Kenneth Mtata.

Ili kuzindua tena majadiliano ya kitaifa na kujaribu kuondokana na athari hizo, Makanisa pia yamechukua hatua ya kuingia katika uwanja  ambao walikuwa ni  waandamanaji wa mipango mikubwa ya kijamii na kisiasa: “Kunako Desemba tulizindua Mfumo Kamili wa Kitaifa wa kuweka jukwaa  ambalo linaleta pamoja   jamii ya umma, wafanyakazi na wawakilishi wa mashirika. Lengo lake ni kuongeza uelewa wa hatua za pamoja na kushawishi vyama vya siasa ili kuingia katika majadiliano ya pamoja. Ngazi ya urais wa Jukwaa hili unatoka katika Baraza la Maaskofu Katoliki, wakati Sekretarieti imekabidhiwa Baraza la Makanisa na tunapendekeza mkutano wa kitaifa na watendaji wote wa kisiasa. Katika siku hizi tunaweza  ujikita katika  awamu ya operesheni na tunaamini kuwa itakuwa chombo  bora cha kuondoka kutoka katika  tundu hili kubwa sana”. Amehitimisha Mchungaji Kenedy.

20 March 2020, 14:22