Tafuta

Vatican News
Tarehe 20 Machi 2020 Nchini Pakistan ripoti inasema maambukizi ya virusi kwa sasa yameongezeka hadi kufika watu 467 Tarehe 20 Machi 2020 Nchini Pakistan ripoti inasema maambukizi ya virusi kwa sasa yameongezeka hadi kufika watu 467  (ANSA)

Pakistan:Sala ya waamini katika mapambano ya corona!

Katika janga ambalo limekuwa ni la kimataifa na hatarishi,viongozi wa Makanisa wanatoa ushauri wa kusali na kufunga. Askofu Mkuu Joseph Arshad nchini Pakistan ameomba waamini wa Islamabad-Rawalpindi, kuungana pamoja katika maombi na kufunga tarehe 20 Machi 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kipindi cha uchungu na mateso umetolewa mwaliko kwa waamini wa jimbo Katoliki la Islamabad-Rawalpindi nchini Pakistan kufanya siku ya sala na kufunga Ijumaa tarehe 20 Machi  2020 katika harakati za kupambana na hatari ya Virusi COVID-19”. Katika janga ambalo limekuwa ni la kimataifa na hatarishi kwa maana hiyo  wito huo ulitolewa katika barua na kutangazwa na shirika la habari za kimisonari (Fides) kutoka kwa Askofu Mkuu Joseph Arshad kwa waamini wa jimbo  kuu Islamabad-Rawalpindi.

Katika barua hiyo Askofu Mkuu Joseph Arshad anathibitisha kuwa “ tusali kwa namna ya pekee kwa ajili ya wale walioambukizwa, kwa ajili ya jitihada zilizo kwisha tekelezwa na mamlaka, kwa ajili ya wale wote katika kambi ya afya na sayansi inayoendelea kutafiti virusi hivi ili hatimaye kuweza kugundua kinga na  kwa wale wote ambao wanahisi kuwa na wasiwasi mkubwa ili Mwenyezi Mungu mwenye huruma aweze kutoa nguvu ya lazima na kuwaponyesha wote.” Askofu Mkuu Arshad aidha ameongeza kuandika “wakati duniani inajikuta mbele ya mapambano ya hatari ya virusi hivi ambavyo vimekumba sehemu mbali mbali, duniani ninapendelea kuonesha ukaribu wangu kwa wale ambao wanateseka na corona na wahudumu wa afya ambao wanashughulikia wagonjwa”.

Askofu Mkuu amesema“Historia ni ushuhuda ambao unatuonesha kila mara kwamba binadamu anachangamotishwa na kila aina ya janga la asili au la kusababishwa na mwanadamu na wakati huo Kanisa limekuwa mstari wa mbele katika kusaidia wenye mateso na binadamu wahitaji. Huduma ya ubinadamu unaoteseka ni hali halisi ya wito wa kikristo.  Hiki ni kipindi maalum cha Kwaresima, na ambacho kwa kwa mara nyingine tena kimejihsisha na wasi wasi mkubwa na ni wa kibinadamu katika hali halisi ya sasa. Kufuatia na hili  ninawatia moyo watu wote ili kusali, kujikita katika matedno ya huduma ya watu wanaoteseka kwa sababu ya magonjwa.” Askofu Mkuu Arshad aidha amewaalika waamini washirikiane na serikali ya Pakistan na kuwa makini katika kuchukua hatua muhimu zinazoelekezwa na serikali za kuweza kuzuia maambukizi zaidi.

Naye Kardinali Joseph Coutts, Askofu Mkuu wa Karach ametangaza kusitishwa kwa misa zote huko Jimbo Kuu Karach nchini Pakistan na maadhimisho mengine, mkutano ya sala katika kipindi cha kwaresima kwa wiki tatu zijazo. Katika ujumbe wake kwa njia ya video kwa waamini, anawashauri waamini na raia wote nchini Pakistan kushirikiana vema na Kitengo cha Afya nchini  humo na kufuata maelekezo yote yaliyotolewa kwa ajili ya ulinzi wa wote. Kardinali Coutts amesema:” watu wote wa imani zote, kwa kuungana pamoja na kusali ili Mwenyezi Mungu aweze kulinda  binadamu na ulimwengu katika janga hili la COVID 19".

 

20 March 2020, 14:00