Tafuta

Vatican News
Jimbo kuu katoliki Chicago Marekani linawaalikwa waamini kujiundia katika sala mara tano kwa siku Jimbo kuu katoliki Chicago Marekani linawaalikwa waamini kujiundia katika sala mara tano kwa siku 

Marekani:Virusi vya Corona,COVID-19: kengele kulia mara tano!

Katika harakati za mapambano ya Virusi vya Corona, COVID-19,jimbo kuu katoliki Chicago Marekani linawaalikwa waamini kujiundia katika sala mara tano kwa siku.Kengele za maparokia yao zitalia mara tano kwa siku kuanzia asubuhi saa 3.00 majira ya huko hadi saa 3.00 usiku majira ya huko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hata Marekani kumeongezeka mara dufu shughuli za majimbo katika dharura hii ya Virusi vya corona. Kati ya majimbo hayo ni Jimbo kuu Chigaco mahali ambapo tangu tarehe 21 Machi  2020, kengele za makanisa zitakuwa zikilia mara tano kwa siku katika harakati za kuwaalika waamini waungane pamoja katika sala kwa ajili ya watu wote waliokumbwa na janga virusi vya corona. Kengele hizo zitakuwa zinaanzia saa 3.00 asubuhi majara ya huko na kufuata kila baada ya masaa matatu hadi saa tatu za usiku.

Kila wakati ni wakati wa sala muda huo umetolewa kwa ajili ya kundi maalum hasa waliokumbwa na Covid-19 kwa mfano walioambukizwa, wagonjwa; wahudumu wa afya ambao wanawashughulikia; wale ambao wanaendelea kufanya kazi kwa ajili ya huduma ya maisha ya watu; kwa ajili ya mataifa yote na vuongozi; na kwa ajili ya waliopoteza maisha yao. Ikiwa parokia haina kengele kama hiyo, basi waamini wanashauriwa kutumia saa zao kwa kuweka alarm ili iweze kuwakumbusha kuwa tayari kuacha kila kit una kusali katika muda huo uliopendekezwa.

 “Lengo letu ni kwamba watu wanaweza kuishi uzoefu wa umoja katika sala kwenye kipindi hiki cha upweke”, amesema Askofu Mkuu wa Chicago, Kardinali Blase Cupich wakati wa kutangaza jambo hili. Jimbo Kuu pia  katika tovuti yao na mitandao ya kijamii wameweza kuweka nia tano za sala katika lugha tatu: kingereza, Kispanyola na kipoland kwa kila kikundi. Nia maalum kila siku itakuwa inatangazwa wakati wa misa za kila siku ambazo zinatangawa mubashara kupitia tovuti hiyo na Twitter. Katika ukurasa maalum wa tovuti yao www.archchicago.org/coronavirus  wamewatangaza habari na kuwakumbusha juu ya liturujia na maadhimisho yatakayofuata wakati wa kipindi cha Pasaka kama ilivyo katika mataifa mengine ya kwamba vyote vitaendeshwa kwa njia ya vyombo vya habari.

Katika ukurasa pia wameunda kitengo cha waamini ambapo wanaweza kushirikia katika kutoa sadaka yao kupitia on-line kwa ajili ya kuwasaidia wenye kuhitaji katika maparokia ya jimbo na ambapo pia wako katika majaribu makubwa wakati huu wa janga la virusi. Vile vile Kardinali Cupich zaidi anawaalika waamini wachangie mfuko wa Jimbo Kuu kwa ajili ya watu wenye matatizo kiuchumi kwa sababu ya virusi vya corona.

21 March 2020, 14:48