Tafuta

Vatican News
Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia linasikitika kutangaza kifo cha Askofu Justin Mulenga wa Jimbo Katoliki la Mpika kilichotokea tarehe 20 Machi 2020 huko Lusaka, Zambia. Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia linasikitika kutangaza kifo cha Askofu Justin Mulenga wa Jimbo Katoliki la Mpika kilichotokea tarehe 20 Machi 2020 huko Lusaka, Zambia.  (AFP or licensors)

Askofu Justin Mulenga wa Jimbo la Mpika, Zambia, Amefariki dunia!

Marehemu Askofu Mulenga alizaliwa tarehe 28 Februari 1955 huko Kabwe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 18 Julai 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 12 Machi 2016 akawekwa wakfu kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpika, Zambia. Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia linapenda kutoa salam zake za rambi rambi kwa watu wa Mungu Jimbo Katoliki la Mpika.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia linasikitika kutangaza kifo cha Askofu Justin Mulenga wa Jimbo Katoliki Mpika, kilichotokea, Ijumaa, tarehe 20 Machi 2020 huko Lusaka, Zambia. Hivi karibuni, Askofu Mulenga alikuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo na mipango ilikuwa inaendelea ili aweze kupelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi, lakini jitihada zote hizi zilizonga mwamba kutokana na maambukizi makubwa ya Virusi vya Corona, COVID-19.

Itakumbukwa kwamba, Marehemu Askofu Mulenga alizaliwa tarehe 28 Februari 1955 huko Kabwe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 18 Julai 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 12 Machi 2016 akawekwa wakfu kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpika, Zambia. Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia linapenda kutoa salam zake za rambi rambi kwa watu wa Mungu Jimbo Katoliki la Mpika pamoja na ndugu, jamaa, marafiki na wale wote walioguswa na msiba huu mzito wa Askofu Justin Mulenga wa Jimbo Katoliki Mpika, Zambia.

Kifo: Zambia

 

21 March 2020, 15:44