Tafuta

Vatican News
Kwaresima ni safari ya upendo na mabadiliko ya undani anasema Kardinali Nzapalainga na kutoa ushauri wa kusikiliza Neno kwamba hakuna lolote lifanyike bila kuwa na Neno la Mungu Kwaresima ni safari ya upendo na mabadiliko ya undani anasema Kardinali Nzapalainga na kutoa ushauri wa kusikiliza Neno kwamba hakuna lolote lifanyike bila kuwa na Neno la Mungu 

Kard.Nzapalainga:mwaliko wa majadiliano ya kidini na maono ya wema wa nchi!

Katika ujumbe wa Kwaresima wa Kardinali Nzapalainga wa Jamhuri ya Afrika ya Kati anatoa mwaliko wa kuwa na majadiliano ya kidini na kuwa na mtazamo wa wema wa nchi yao.Ili kufikia hilo ni kwa njia ya kisikiliza na kutafakari Neno la Mungu.Hakuna lolote lifanyike pasipo Neno la Mungu!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Umuhimu wa Neno la Mungu katika maisha ya kila siku una tazama hata  safari ya uekumene na majadiliano ya kidini. Ndiyo mantiki iliyokita katika ujumbe wa Kwaresima wa Kardinali Dieudonné Nzapalainga, Askofu Mkuu wa Bangui  katika  Jamhuri ya watu wa Afrika ya Kati. Katika ujumbe wake, Kardinali Nzapalainga anatazama hata juu ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka huu katika nchi yake, kwa maana hiyo anatoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wapiga kura ili kipindi hiki kiwe na matazamio mema ya uchaguzi na kuwashauri wapambane ili waweze kuondoa vizingiti vya kikanda na kikabila katika kutazamia mema na ustawi wa pamoja wa nchi hiyo. Kwa dhati anawaalika kukita matumaini yao, maamuzi yao na jitihada zao, ziwe za kibinafsi na zile za kijumuiya katika kusikiliza na kuweka kwenye matendo Neno la Mungu. “ Yote ni kwa njia ya Neno la Mungu na hakuna lolote lifanyike bila kuwa na Neno la Mungu” anaandika Kardinali Nzapalainga.

Kupokea Neno la Mungu na kuacha liweze kukita ndani ya roho ndiyo hali ya kuweza kuishi Kwaresima kama mchakato wa safari ya upendo na mabadiliko ya undani, anasisitiza Kardinali Nzapalainga ambaye pia anatoa ushauri wa kusikiliza Neno kama uhakika wa kuweza kuleta maana ya kweli ya neema, katika sala, sadaka na kufunga. Aidha amesisitiza kwamba: "ikiwa Neno lipo katika mazungumzo na Mungu kuna hata majadiliano mengine ya kuweza kukuza. Kufuatiana na suala la uekumene Kardinali amekumbuka juu ya  pendekezo la uzoefu wa tarehe 25 Januari 2020 katika Parokia ya Mtakatifu Antonio wa Padua huko Damara ambao uliwaunganisha wakristo, wakatoliki, waprotestanti na waislam katika maombi na kusikiliza Neno la Mungu. Kwa kuweka msisitizo amesema, " ni wakati wa sasa wa kiekumene na majadiliano ya kidini”. Katika kuweka suala hili katika matendo, Kardinali Nzapalainga anawaalika maparoko kwenda kwa wachungaji wa madhehebu mengine na maimam wa maeneo mengine ili kuweza kuuishi uzoefu wa kiekumene na kidini wakiwa wamezungukwa na Neno la Mungu. Kwa kufanya hivyo anasema: “inawezekana kutufanya tuwe na utambuzi zaidi wa dhambi zetu na vizingiti vyote vinavyotukumba kama ndugu”.

Kwa mtazamo wa uchaguzi wa urais katika nchi yao Kardinali Nzapalainga  anasisitiza kuwa “kwaresima ni kipindi muafaka cha kumkabidhi Bwana na kufanya maamuzi angavu ambayo yanapelekea maisha, maelewano na mshikamano. Kwa mujibu wake anasema maelezo kuhusu vishawishi vya Yesu, vinaweza kufundisha jambo kwani anasisitiza kwamba kwa viongozi  wasilazimishwe watu, kama ibilisi, ubatili mtupu na siyo kupendekeza njia ambazo siyo muhimu kwa watu; kwa wapiga kura wafuate  nyayo za Kristo, wasidanganyike na maneno ya uwongo, na waachie nuru ya Neno la Mungu.  Katika mkutano wa Bwana na Msamaria mwema, ni kuonesha kwamba katika matukiko hayo kuna uwezekanano wa kuvunja uadui na kuachilia mbali uchaguzi binafsi ambao unaweza kujitokeza katika kanda na kikabilia, mambo ambayo kwa hakika haleti tija na wala maendeleo ya kitaifa.

Ni mwaliko kwa wote kufa ndani mwao zile tabia zenye  tamaa na matendo ambayo hayasaidii kuleta wema na  ambayo yanaweza kusasabisha ukosefu wa maendeleo ya nchi. Katika kipindi hiki, Kardinali Nzapalainga anasema ni muafaka wa kushirikiana kwa pamoja ili waondokane na kipeo  walicho nacho na kutoa mwamko hai wa maendeleo fungamani ya Taifa. Ujumbe wa Kwaresima 2020 unahitimishwa kwa kukazia hata katika kupokea na kusikiliza Neno la Mungu ambalo linaweza kweli kuwa chachu ya majadiliano ya kweli na mabadiliko ya kina katika jamii nzima ya Jamhuri ya watu wa Afrika ya Kati.

05 March 2020, 14:27