Tafuta

Vatican News
Shirika la wajesuit Kanda ya Afrika wanatoa wito kwa Serikali ya Camerun kufanya majadiliano ya dhati ili kuleta amani ya kudumu nchini humo. Shirika la wajesuit Kanda ya Afrika wanatoa wito kwa Serikali ya Camerun kufanya majadiliano ya dhati ili kuleta amani ya kudumu nchini humo.  (AFP or licensors)

Camerun:Wajesuit Afrika watoa wito kuhusu suluhisho la mchakato wa amani!

Kufuatia na mzozo unaoendelea kwa miaka minne sasa nchini Kameruni kati ya Kanda za Kingereza na Kifaransa,Baraza la Shirika la Wajesuit wa Afrika wanaungana na wengine kutoa wito wa Serikali ya Biya kufanya mchakato wa majadiliano ambayo yanaweza kufikia suluhisho la amani ya kudumu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Majadiliano ya dhati kwa ajili ya kanda ya lugha ya kingereza ndiyo moja ya suluhisho endelevu dhidi ya mzozo ambao umesababisha kupoteza maisha ya kibinadamu tendo ambalo halikubariki katika Mkoa wa Kaskazini magharibi na Kusini mwa Camerun. Hayo ni kwa mujibu wa  Baraza la Wajesuit wa Afrika na Madagascar (Jcam) ambao wanaunga mkono kwa pamoja katika tamko ambalo limetolewa wiki mbili zilizopita  kutoka katika Makanisa ya nchi tofauti ulimwenguni kote kwa ajili ya  suluhisho la amani dhidi ya  mzozo huo kwa karibu miaka minne wakipinga serikali kuu inayoongozwa na Rais Paul Biya kwa wanamgambo wa kujitenga wa Kingereza.

Uhusiano kati ya kundi kubwa la wanao zungumza kifaransa na wale wachache wanaozungumza kingereza ni mgumu sana tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kunako mwaka 1961, uliozaliwa kutokana na muungano wa Camerun ya Kifaransa na ile ya  Kameruni ya Waingereza, lakini tangu mwaka 2016 kumezuka mzozo mkubwa hadi umwagaji dumu kwa njia ya silaha baada ya maandamano makali dhidi ya uamuzi wa Younde kulazimisha kuzungumza lugha moja tu ya kifaransa katika mahakama na katika shule za lugha ya kingereza.

Ukandamizaji  huo uliwasukuma waasi wanaozungumza Kiingereza kujitangazia uhuru. Tangu wakati huo, mzunguko wa vurugu umeanza, ambao umetumia fursa ya wahalifu na ambao umesababisha vifo vya zaidi ya elfu 2 na kulazimisha watu wengi kutoroka, hata kwenda nchi jirani ya Nigeria kwa zaidi ya watu 700,000 na watoto 800,000 wasiende shuleni. Katika muktadha huo katikati ya mwezi Februari, barua ya Maaskofu wa Camerun na wa Nchi tofauti kumi za Bara waliandika wakiomba kuwepo suluhisho la amani kwa njia ya majadiliano ambayo ndiyo njia muafaka na zaidi katika kuhamasisha serikali ya Biya ili  ashiriki majadiliano yaliyoanzishwa na shirika moja lisilo la kiserikali huko Uswis.

Wito huo pia unajumuishwa sasa  na wa Shirika la Yesu kwa upande wa bara la Afrika na Madagascar ambao wanalaani vikali iwe “ kuendelea kutumia nguvu kwa upande wa Serikali ya Camerun, hata vurugu za wanamgambo. Wanashirika hawa wanasema: “Tunaomba Rais Biya na serikali yake wachukue hatua zaidi dhidi ya kukandamiza na kuchukua jukumu la kupata suluhisho la kudumu kupitia majadiliano ya upatanisho na kuhakikisha heshima ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza na udhihirisho”.

Kwa mujibu wa Baraza la Wajesuit wa Afrika na Madagascar (Jcam) wanasema wako tayari kutoa mchango dhabiti kwa juhudi zilizowekwa na Umoja wa Afrika (UA ili kuleta amani katika mkoa huo na bara lote  hasa kwenye kampeni ya “Silencing Arms in 2020' yaani “kusitisha silaha Afrika 2020” iliyoanzishwa mnamo 2013 na kurudiwa tena katika mkutano wa hivi karibuni wa Addis Ababa wa wakuu wa Nchi na serikali.

03 March 2020, 11:27