Tafuta

Vatican News
Ukanda wa Sahel  barani Afrika  watu wanazidi kushambuliwa na magaidi na kuwawa kinyama. Ukanda wa Sahel barani Afrika watu wanazidi kushambuliwa na magaidi na kuwawa kinyama.  (SESAME PICTURES)

Burkina Faso:majadiliano ya kidini yawe chombo cha mapambano ya kigaidi!

Katika mahojiano tarehe 5 Machi 2020 kandoni mwa mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki na Madagascar( SECAM)Kardinali Phillip Ouedraogo,Askofu Mkuu wa Ouagadougou, nchini Burkina Faso,amethibitisha kuwa majadiliano ya kidini ni muafaka katika mapambano ya kigaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kardinali Phillip Ouedraogo, Askofu Mkuu wa  Ouagadougou, nchini  Burkina Faso, amesema majadiliano ya kidini ni chombo madhubuti kwa ajili ya mapambano ya ugaidi. Amesema hayo katika mahojiano tarehe 5 Machi 2020 kandoni mwa mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki na madagascar ( SECAM) kwa mujibu wa Tovuti ya Recowa-Cerao (mabaraza ya Maaskofu wa Kanisa ya Afrika Magharibi). Kardinali Oueadraogo anasema kuwa ili kuweza  kukabiliana kwa amani kati ya dini zote majadiliano ndiyo njia muafaka wa kuweza kupambana na wenye itikadi kali kwa namna ya pekee juu ya kipeo ambacho kwa sasa wanakiishi katika Ukanda wa Sahel huko Afrika mahali ambapo mashambulizi ya kigaidi yamezidi kuwa ya nguvu yanayoikumba nchi ya Burkina Faso, Mali, Niger na Chad.

Mazungumzo ya kidini ndiyo kiini cha kazi yao ya kichungaji  anasisitiza na kwamba wanatafuta namna ya kufanya kazi pamoja ili kuishi pamoja, katika kuheshimu na kusikilizana kwa pamoja. Hata hivyo kiini cha maneno ya Askofu Mkuu  wa Ouagadougou  ni ule wito wa kuweza kuweka umuhimu wa mshikamano wa ndani na nje, yaani uwe kwa ngazi mahalia au uwe wa kimataifa, kwa sababu anatoa mfano kwamba wasemavyo wahenga wa kiafrika kwamba “kidole kimoja hakivunji chawa, au hakikusanyi unga”,  kwa maana kuna haja ya kuwa na vidole vingi. Kwa maana hiyo ni lazima kuunganisha nguvu ziwe za ndani na je kwa kila nchi husika.

Kwa kutazama pia katika hali halisi ya nchi yake Burkina Faso, Kardinali  amesema nchi yao sasa  inakabiliana na changamoto za mashambulizi ya kigaidi tangu mwaka 2015. Kwa miaka mitano watu wasio kuwa na hatia wameuwawa kinyama bila huruma; Kanisa katoliki limelipa gharama nzito na wakristo wengi wameuwawa. Hata waprotestanti hawakuweza kukwepa janga hili na zaidi  watu 600elfu wamerundikana kwa sababu ya ukosefu wa usalama na kutumia nguvu na tukio hili limezuia watoto wengi wasiweze kwenda shule.

Rais wa Secam  kwa maana ya tukio hili anaomba wenye nguvu wa nchi za  Magharibi kuweza kusitisha kabisa biashara ya silaha barani Afrika kwani “ silaha hizi zimeruhusu makundi mengi ya kijihadi kuuwa watu wasio kuwa na hatia” Vile vile Kardinali  Oueadraogo  pia anakemea watendaji mahalia ambao wanahusika na ushiriki wa kununua silaha, “serikali haribifu ambayo inatenda kinyume na kwa kununua silaha na kusasabisha hatari ya amani na usalama wa watu wa Afrika”. Kwa mujibu wake anasema, Kanisa litabaki kidete ili upeleka mbele matumaini kwa watu wenye matatizo na  hatimaye katika matumaini ya kuona kuwa vitendo viovu vya kigaidi  vinasimamishwa.

Kwa  mujibu Askofu Mkuu kufuatana na hiyo anatoa mwaliko kumwomba Bwana mfalme wa amani na mpambanaji kwa ajili ya amani na wakati huo huo anawanashauri waamini wote na wenye mapenzi mema kuendeleza ishara za dhati za mshikamano kwa ajili ya kuwasaidia watu na kuwapatia msaada wa chakula, nguo na mafunzo kwa ajili ya watoto. Hatimaye wito wake unawandea waandishi wa habari, vyombo vya habari kwamba wanapaswa kuwajibika kwa maana wao kweli wawe "sauti ya wasio kuwa na sauti", watu wasio kuwa na hatia ambao wanauawa bila sababu zozote.

 

10 March 2020, 15:02