Tafuta

Virusi vya corona nchini Bangladesh Virusi vya corona nchini Bangladesh 

Bangladesh:Kard.D’Rozario ushirikiano na serikali ni muhimu!

Kardinali Patrick D’Rozario,askofu Mkuu wa Dacca,Bangladesh ambaye ametoa ujumbe wake kwa njia ya video akiwaalika waamini kukabiliana na janga la virusi vya corona lakini kwa kufuata miongozo iliyotolewa na serikali na Kanisa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuwa waaminifu katika kushirikishana na serikali ili kuweza kushinda  janga la virusi vya corona ndiyo wito wa Kardinali Patrick D’Rozario, askofu Mkuu wa Dacca, nchini Bangladesh ambaye ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kupitia Shirika la habari za Kimisionari Fides. “Kardinali amesema: “wapendwa waamini, tunajikita kukabiliana na moto wa virusi vya corona. Mbaki nyumbani na kufikiria wengine. Tunapitia wakati mgumu sana. Katika hali kama hii inawezekana kujitokeza maswali mengi ni kwa nini janga hili la virusi vya corona?”

Kardinali D’Rozario ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu Katoliki nchini Bangladesh (CBCP), amebainisha kwamba,“sisi siyo binadamu tu, tunaamini katika Kristo, kwa maana hiyo katika kipindi kigumu zaidi, tutafute zaidi kuwa wana wa Mungu. Serikali inatupatia miongozi ya kufuata katika hali hii ngumu ya virusi vya corona. Ninawaomba kwa unyenyekevu waamini wote, kufuata miongozo iliyotolewa na serikali pamoja na Kanisa”.

Hata hivyo waziri mkuu Sheikh Hasina alihutubia taifa ambalo tayari kuweka kukabiliana na kila hali ngumu kwa mtazamo wa janga la virusi kidunia na kuwaomba wazalendo wote kusaidia kujidhibiti na virusi vya corona, kwa kufuata miongozo iliyotolewa.   Sheikh Hasina amerudia kutoa mwaliko pia wa kubaki nyumbani na akiwalekeza kila mzalendo wa Bangladesh amesema, “ utambuzi na uwajibikaji binafsi utajilinda binafsi, familia yako na watu wote. Kuzuia maambukizi ni sasa na yanapaswa kupewa kipaumbele.

29 March 2020, 15:06