Tafuta

Uwanja wa Mtakatifu Petro Ujumaa 27 Machi 2020 ulionekana wazi lakini ukweli ulikuwa umejazwa na roho za wa waamini wote duniani! Uwanja wa Mtakatifu Petro Ujumaa 27 Machi 2020 ulionekana wazi lakini ukweli ulikuwa umejazwa na roho za wa waamini wote duniani! 

Askofu Crociata:uwanja wa Mtakatifu Petro ulionekana mtupu kiukweli ulijazwa kiroho!

Askofu wa Latina na Makamu wa Comece akitafakari kuhusu sala maalum na baraka ya Urbi et Orbi ya Papa Francisko anasema ulimwengu ulitikiswa sana na maneno,Baba Mtakatifu ambaye anatualikwa kugundua kwa upya ukuu wa kina wa katika uchaguzi wa maisha yetu kufuatia na janga hili.

Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Askofu Mariano Crociata, wa jimbo katoliki la Latina, Sezze na Priverno, Italia  mmoja wa makamu Rais wa  Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (Comece), katika maelezo yake na Vatican News bado anawaza na kuona  machoni pake ule uwanja wa Mtakatifu Petro ukiwa mtupu na kulowanishwa kwa mvua, ambapo Papa Francisko tarehe 27 Machi 2020 aliweza kuinua sala yake maalum kwa Mungu ili kuomba msaada janga la kutisha liishe na ambapo alitoa baraka ya Urbi et Orbi. Kwa mtazamo wa kijujuu amesema Asofu Crociata uwanja ulionekana kuwa mtupu, lakini kiukweli ulikuwa umejazwa na nguvu ya kiroho ambayo iliweza kuvuka kila kikwazo, kila mipaka, kufuatana na ishara kubwa hiyo iliyotingisha dunia nzima.

Ujumbe uliogusa dhamiri zetu ni upi?

Papa Franciso ametushauri kuendelea na kupambana bila kupoteza maana ya kiroho katika mambo ambayo yanatukia kwa sasa. Sisi sote tunaalikwa kuwa na mshikamano kwa wale wote ambao wanahitaji msaada, kuanzia wagonjwa. Lakini pia Papa Francisko anaomba kutafakari juu ya maisha yetu. Tunapaswa kutambua jinsi gani tulikuwa kwanza kabla ya uzoefu wa janga la kutisha na jinsi gani tumeanza kubadilishwa taratibu na janga hili. Na ndiyo hilo Papa Francisko amependekeza katika ujumbe wake hasa kwa kutukumbusha kuwa “sisi sote tuko katika mtumwi mmoja tukiwa na Bwana”. Ikiwa Bwana yuko pamoja nasi, basi tutashinda kila tatizo.

Papa akitafakari Injili ya Marko inayosimulia mitume waliopata hofu kutokana na dhoruba kali, alirudia kuuliza imani yetu iko wapi kama vile Yesu alivyo wauliza wafuasi wake…

Askofu Crociata amesema kuwa “ ni swali ambalo linawahusu watu wote .Ni kwa jinsi gani imani imekuwa haba. Ni shauku gani na ari tuliyo nayo katika imani? Kuna tatizo la kushuka, kupoteza umakini, ambao unagusa uzoefu wa kikristo. Lakini pia kuna swali ambalo linakwenda zaidi ya ukuu wa kikristo, unaogusa hata wale wote ambao wanaishi kwa ajili yao binafsi na ambao  wanatambua maana ya maisha katika hali ya kuwa na mali. Je inawezekana kuishi kwa ajili ya hilo? Ni maswasli ambayo yanamkumba mwanadamu wa leo. Uzoefu wa mlipuko wa janga unatuweka mbele ya kutazama sisi na kutafakari kwamba ni nani kiukweli na kutufanya tugundue kwa upya kile ambacho ni msingi wa maisha kweli.

Ni dhoruba kali ambayo imefunua wazi ule udhaifu wetu?

Ndiyo, anajibu Askofu  kwa maana hapa unaingia mchezo unaosukana pamoja  kati ya mwelekeo wa kiroho wa maisha na mantiki ya mali. Leo hii tunatazama namna ya janga hili lilivyo katika hali ya ugawanaji wa mali. Ni tatizo la msaada katika mazingira, katika kutibu nyumba yetu ya pamoja. Ni tabia ya imani tuliyo nayo ambayo matokeo yake yanauhusiano wake. Ni kipindi cha kufanya uchaguzi katika kambi kwa sababu uchagusi msingi ndiyo unatoa mwelekeo katika hatma ya maisha ya ubinadamu wetu.

29 March 2020, 13:44