Tafuta

Vatican News
Maaskofu wa Zambia, Malawi,Zimbabwe wakiwa na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Zambia Maaskofu wa Zambia, Malawi,Zimbabwe wakiwa na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Zambia 

Papa:Ni kutafakari juu ya utume wa Kanisa barani Afrika kwa ajili ya Habari Njema!

Katika ujumbe wa Papa Francisko unafungua siku ya kwanza ya mkutano wa maaskofu wa Malawi,Zambia na Zimbabwe.Maaskofu wameanzisha mchakato wa ushirikiano na kutoa wito wa pamoja ili kutaoa suluhisho la migogoro na juu ya kipeo cha uchumi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ili kuhamasisha mshikamano wa kichungaji kati ya makuhani, walei na watawa nchini Malawi, Zambia na Zimbabwe ndiyo lengo kuu na mkutano uliofanyika jijini Lusaka Zambia kuanzia tarehe 3-5 Februari 2020, ukiwa ni Mkutano wa kwanza wa ushauri wa maaskofu Katoliki katika nchi hizo tatu za Afrika na ambapo wamepokea hata ujumbe kutoka kwa  Papa Francisko.

Papa Francisko: kusali na kutafakari utume wa Afrika Kusini

Katika salam zake Papa anawatia moyo maaskofu kusali na kutafakari juu ya utume wa Kanisa Afrika ya kusini, na zaidi katika kujikita kwa shauku kubwa ya kutanza na kdumisha shughuli za kichungaji ambazo hatimaye ziweze kuzaa matunda kwa watu wa Mungu.

Katika taarifa yao ya hitimisho la mkutano wao, Maaskofu wanabainisha mapendekezo yao  ya kufikiria tena malengo, miundo, mtindo na njia za uinjilishai katika kila Nchi, kwa kuondoana na tabia  msemo “ tumezoea kufanya hivyo”, suala ambalo linagusiwa hata Papa Francisko katika Wosia wa kitume wa  “Evangelii gadium” (n. 33), na ambapo  anashauri kwa dhati kuachana na tabia hizo. Katika mtazamo huo, kufikiria mfanano wa kihistoria  na utamaduni kati ya mataifa hayo matatu yanayopakana. Maaskofu wameamua kuweka mambo muhimu ya ushirikiano wa dhati katika mada zinazowaunganisha kama vile mafunzo ya makuhani, elimu kwa walei; kuweka utaratibu wa kutembeleana kwa mshikamano, iwe katika kipindi cha matatizo au kile cha utulivu na furaha, kwa ajili ya kukuza roho ya udugu; matumizi ya miundo ya majengo ambayo tayari yao kama Sekretarieri ili kupunguza gharama za kila Kanisa; kuandaa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mabaraza hayo matatu.

Pendekezo la Baraza la Maaskofu wa Kanda  ya nchi tatu

Aidha wamependekea juu ya kuunda Baraza ka Maaskofu wa nchi tatu hizi za kanda ya Kusini. Hata hivyo chombo  hicho wanabainisha kwamba  hakiondoa ule  ushiriki ulio tayari wa maaskofu wa Malawi na  Zambia kuwa katika Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki (Amecea) na hata ile ya maaskofu wa Zimbabwe kuwa katika shirikisho la  Kanda ya Maaskofu wa Afrika ya  Kusini (Imbisa).

Tamko la amani na mapatano

Katika roho ya mshikamano, hatimaye Maaskofu Katoliki wa nchi hizo tatu , wametoa tamko la pamoja la amani, mapatano na majadiliano katika kanisa nzima ya Afrika ya Kusini, ili migongano na mikwaruzo ya kisiasa ambayo inaendelea  ipate kusitishwa pia kutafuta suhuhisho la kipeo cha uchumi unaokumba sehemu nyingi katika nchi hizo na zaidi zenye hatari ya ukame. Ushauri wa nguvu pia umetolewa ili wajikite katika mantendo ya dhati kuweza kukomesha matokeo hasi ya mabadiliko ya tabia nchi  na sababy ta  asili ya mafuriko na pia ukame. Ujumbe wa maaskofu hao unahitimishwa kwa kumwomba Bikira Maria.

07 February 2020, 12:30