Tafuta

Tarehe 26 Februari ni mwanzo wa Kwaresima kwa kuanza na liturujia ya kupakwa majivu Tarehe 26 Februari ni mwanzo wa Kwaresima kwa kuanza na liturujia ya kupakwa majivu 

Nigeria:mshikamano wa sala ili kudhibiti ghasia nchini Nigeria!

Wakatoliki wanaitwa kuwa na mshikamno kwa watu wengi ambao wametekwa nyara na kuuwawa kwa kufanya ishala ya uvaaji wa nguo nyeusi ikiwa ni lengo la kutaka kupinga kila mtindo wa hali hizo.Majimbo yote katoliki kitaifa wameombwa pia kusali kwa ajili ya kuomba amani nchini Nigeria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Fursa ya siku ya Jumatano tarehe 26 Februari 2020 wakati mama Kanisa anaanza kipindi cha Kwaresima kwa ibada maalum ya kupakwa majivu, wakatoliki wanaitwa kuwa na mshikamano kwa watu wengi ambao wametekwa nyara na kuuwawa. Watafanya hivyo kwa kuvaa nguo nyeusi, katika ishala ya kupinga kila aina ya hali hizo na kwa majimbo yote ya taifa wataweza kusali kwa ajili ya kuomba amani. Haya yamesemwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Baraza la Wakatoliki Nigeria (CSN), Padre Zacharia Nyantiso Samjumi. Katika taarifa yake amesema kwa waandishi wa habari kuwa “nimepewa jukumu la Baraza la Maaskofu wa Nigeria  (CBCN) kuwapa taarifa kuwa Kanisa linapaswa kuzungumza na kutenda kwa dhati hasa kuhusiana na suala la ngazi za ulinzi na usalama wa Nchi.

Katika ujumbe uliofuata kwa maparoko wa maparokia yote,  Baraza la maaskofu Nigeria limeamua kuwa Dominika tarehe Mosi Machi 2020, hapatakuwapo na misa yoyote ya jioni katika maprokia yote. Badala yake watafanya maandamano ya  sala katika  kupinga kila aina ya mauaji yanayoendelea na ukosefu wa usalama katika nchi ya Nigeria . Katika ujumbe wa Kwaresima uliotangazwa kwa umma tarehe 21 Februari 2020, Maaskofu wa Nigeria wanawaalika Kanisa la ulimwengi na waktristo wote kuungana kwa pamoja katika sala zao kwa ajili ya kaka na dada waliouwawa na kwa ajili ya kuombea amani na usalama katika nchi ya Nigeria.

“Tuna huzuni. Tunaishi kwa uchungu, lakini kwa matumaini ya kwamba mwanga wa Kristo, ambao unatuangazia katika mioyo yetu, utaangaza hata katika kona zenye  giza la jamii ya Nigeria”, wamethibitisha maaskofu. Aidha kwa ngazi ya usalama wa Nigeria wanasema leo hii sehemu kubwa ya wanaigeria wanaishi na hofu, iwe nyumbani, barabarani hata katika maeneo mengi ya nchini. Uwezo wa  kutesa wakristo kwa upande wa Boko haramu na kuendelea kuteka watu kwa malengo ya kutaka fidia kwa upande wa makaundi hayo na ugaidi wa kila aina unaogopesha wazalendo, wamsisitiza maaskofu.

Kufuatia na hilondipo maaskofu wanatoa mwaliko wa serikali katika  kufanya michakato ya kisheria dhidi ya waalifu, wapewe adhabu kali na zaidi  hasa juu ya uwezo na utashi kwa serikali katika  kulinda na kutetea maisha ya wanaigeria. Kwa utambuzi wa uwajibikaji wao kimaadili na mbele ya waamini, maaskofu pia wanakumbusha kuwa bila usalama hawawezi kuwa na amani na bila amani hawawezi kuwa na maendeleo au kukua kitaifa. Katika muktadha huo, Baraza la Maakofu wa Nigeria, wametoa ushauri kwa serikali kusitisha kwa haraka bila kusubiri matukio haya ya kutumia nguvu na ukatili hasa unawaokusudia wakristo, waweke mbaloni wale ambao wako nyuma yamatukio hayo ya mauaji yasiyo na kikomo na ambao wanazidi kupanda mbegu ya  hatari ya chuki na ukosefu wa kuaminiana kati ya sekta za jamii nchini Nigeria.

Wito wa maaskofu  pia wamegeukia jumuiya ya kimataifa ili waweze kwa dhati kutoa msaada kwa serikali ya Nigeria katika mapambano dhidi ya magaidi kwani matokeo ya uhalifu huo unaangukia si tu katika nchi ya Nigeria lakini pia  hata kwa afrika nzima. Na hatimaye kwa wanaamini wa Kanisa Katoliki nchini Nigeria wanawaalika wasikubali kukata tamaa badala yake kuwa mashuhuda wa dhati wa Injili na kujikita katika matendo ya kweli ya fadhila za kikristo.

25 February 2020, 14:43