Tafuta

Vatican News
Liam Neeson anaomba msaada kwa ajili ya watoto na wazazi wao wahamiaji walioko mpakani mwa Brazil wakitoke nchini Venezuela Liam Neeson anaomba msaada kwa ajili ya watoto na wazazi wao wahamiaji walioko mpakani mwa Brazil wakitoke nchini Venezuela   (ANSA)

Venezuela:dunia isikilize kilio cha watu waathirika!

Baraza la Maaskofu nchini Venezuela wanarudia kwa upya kutoa tamko la wito ili viongozi wajibu kwa dhati juu ya mahitaji ya watu ambao wamejaribiwa na kipeo cha umaskini na ukosefu wa msimamo.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema maelfu ya watoto bado wanaendelea kuwa waathirika wa hali mbaya nchini na kulazimika na familia zao kukimbia na kuingia nchini Brazil

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Watu wa Mungu wa Venezuela wako mstari wa mbele wa kutaka mabadiliko ambayo Venezuela inahitaji. Ndiyo maandishi yaliyomo ya Maaskofu wa Venezuela mara baada ya Mkutano wao wa Mwaka uliofunguliwa tarehe 8 Januari 2020 huko Caracas. Kanisa linataka kuendelea kutoka msahada wa lazima kwa wote hasa wale  waathirika. Maaskofu pia wanasisitiza hata kile ambacho walibainisha kwenye Wosi wao wa kichungaji wa tarehe 12 Julai 2019 kwamba “ Mbele ya hali halisi ya kukubiliwa na serikali isiyo halali, Venezuela inataka mabadiliko ya kweli, ya mapambania ili kurudi Katiba” . “Mabadiliko haya yanahitaji kufukuzwa kwa wale wanaotumia madaraka kwa njia isiyo halali na uchaguzi wa Rais mpya wa Jamhuri katika muda mfupi iwezekanavyo.”

Viongozi waheshimu hadhi ya watu wote

Kwa washiriki wa Vikosi vya Wanajeshi, maaskofu wanaombaa hasa kuwa na viongozi wanaoongozwa na dhamiri njema na kwamba waheshimu hadhi na haki ya watu wote. Wale ambao wana jukumu la kisiasa, na pia wote serikalini na katika upinzaji, lazima wawe makini na watu, wakiangalia mahitaji yao na sio fursa na maslahi fulani.

Wahamiaji wawe mabalozi wa upendo katika kutoa hisani

Katika ujumbe huo, maaskofu wa Venezuela pia wanageukia  watu  wa Mungu wa Venezuela waliolazimishwa kuondoka katika nchi yao. Maaskofu wanawatia moyo kufungamana katika tamaduni mpya, kama ilivyotokea kwa wahamiaji kutoka kanda  tofauti za ulimwengu ambao wamekaribishwa nchini Venezuela. Wanawasihi wasiache kuonyesha imani yao na upendo hasa wa hisani kwa kushiriki katika kazi za jamii na Kanisa.  Wasisite kamwe kuwa mabalozi wa urithi uliopokelewa kutoka kwa mababu zao.

Nchi imasikitishwa na kuwekwa kwa mfumo wa kiitikadi

Katika ujumbe huo, maaskofu pia wanawasihi watu wa Amerika na ulimwengu wasikilize kilio cha idadi ya watu wa Venezuela. Na wanaomba mataifa ambayo yanawakaribisha wahamiaji wa Venezuela kuwapa umakini wanaohitaji kuishi kwa heshima. Huko Venezuela tunaishi katika serikali ya kiimla na ya kinyama ambamo upinzani wa kisiasa unateswa na mateso, kukandamizwa”. Haikubaliki, wanaongeza, kwamba nchi yenye utajiri mkubwa wa nyenzo imekuwa maskini na kuwekwa mfumo wa kiitikadi. Mfumo ambao mbali na kukuza ustawi wa kweli, umetelekeza raia wake. Kwa wale ambao wanasimamia serikali, mambo muhimu sio jambo ustawi wa jamnii tu lakini  nguvu ya oamoja na yenye uwezo wa kuvunja kila jaribio lolote la kuishi katika demokrasia halisi”.

Maelfu ya watoto wanaendelea kuwathirika na hali mbaya kwa mujibu wa Unicef

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema maelfu ya watoto bado wanaendelea kuwa waathirika wa hali mbaya nchini Venezuela na kulazimika na familia zao kufungasha virago na kuingia nchi jirani ya Brazil. Katika ziara ya siku nne iliyofanywa na balozi mwema wa shirika la UNICEF Liam Neeson kwenye mji wa Brazil ulioko mpakani na Venezuela ameshuhudia hali halisi baada ya kukutana na Watoto na familia zao lakini pia jamii zinazowahifadhi. Katika ziara hiyo ya siku tatu iliyomalizika mwishoni mwa wiki Neeson ametembele eneo la Rondon 3, moja ya makazi makubwa zaidi yanayohifadhi wahamiaji wa Venezuela nchini Brazili. Watu Zaidi ya 1000 wakiwemo Watoto 550 wanaishi katika makazi haya hivi sasa. Kama hatua za kukabiliaka na wimbi kubwa la wahamiaji wa Venezuela kuingia Brazil , UNICEF na washirika wake wamechukua hatua mbalimbali hasa katika masuala ya elimu na ulinzi kwa Watoto, afya na lishe, pamoja na masuala ya maji na usafi.

Vituo vinakutanisha watoto 

Moja ya vitu walivyofanya ni kufungua mahali pa kukutanisha watoto kituo kiitwacho Super Panas ambacho kinatoa huduma za elimu, michezo na msaada wa kisaikolojia ili kuandaa watotona vijana barubaru kujumika katika shule za kawaida au kuwasaidia ambao tayari wameingia shuleni. Balozi mwema alishiriki katika shughuli mbalimbali na Watoto hao na vijana barubaru na pia kuhudhuria huduma za afya za upimaji kwa ajili ya Watoto hao wahamiaji. Kwa kushirikiana na mamlaka na mashirika ya Umoja wa Mataifa Ecuador, Peru, Brazil, Colombia, Guyana na Trinidad na Tobago, UNICEF pia inaongeza hatua zake katika maeneo ya mijini na kusaidia kujumuishwaji wa Watoto kutoka Venezuela katika jamii zinazowahifadhi.

Nchi za Amerika ya kusini na Caribbean zinahifadhi wakimbizi wengi

Nchi za Amerika Kusini na Caribbea tayari zinahifadhi wahamiaji na wakimbizi milioni 3.9 kutoka Venezuela katika moja ya kinachojulikana kama wimbi kubwa zaidi la wahamiaji. Na idadi ya familia zinazoondoka Venezuela inazidi kuongezeka . Mwaka huu watoto zaidi ya milioni 1.9 wakiwemo wahamiaji toka Venezuela na jamii zinazowahifadhi wanatarajiwa kuhitaji msaada. Na hadi kufikia Desemba 2019 ni asilimia 41 pekee ya dola milioni 69.5 zizilizohitajika mwaka jana ndio zimepatikana na mwaka huu UNICEF inahitaji dola milioni 64 ili kukidhi mahitaji ya takriban watoto 633,000 walioathirika na uhamiaji toka Venezuela, wakiwemo ambao wako safarini na jamii zinazowahifadhi katika nchi sita za Amerika ya Kusini ikiwemo Brazil.

 

13 January 2020, 13:31