Tafuta

Mpango wa maaskofu wa Papua Guiena mpya kwa 2020 unataka kupeleka mbele kazi ya ubunifu na ujenzi kuanzia na ushirikishwana binafsi na tafakari juu ya Maandiko Matakatifu Mpango wa maaskofu wa Papua Guiena mpya kwa 2020 unataka kupeleka mbele kazi ya ubunifu na ujenzi kuanzia na ushirikishwana binafsi na tafakari juu ya Maandiko Matakatifu 

Papua Guinea Mpya:Mpango wa kichungaji 2020 kwa ajili walei na utume wa kimisionari

Kila mmoja wetu anaweza kutafuta kuelewa kwa kina imani yake katoliki,ikiwa na maana ya Sakramenti na namna ya kuziishi na kizifafanua katika maisha ya kila siku kwenye matendo hai.Ndiyo ufupisho wa tafakari ya Baraza la Maaskofu nchini Papua Guinea Mpya na Visiwa vya Salomoni walioutoa kwa ajili ya mwaka 2020.Mpango wao wa kichungaji, unaongozwa nakaulimbiu:Walei wakatoliki:wamefundwa kwa ajili ya utume.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila mmoja wetu anaweza kutafuta kuelewa kwa kina imani yake katoliki,ikiwa na  maana ya Sakramenti na namna ya kuziishi na  kizifafanua katika maisha ya kila siku kwenye matendo hai. Ndiyo ufupisho wa tafakari ya Baraza la Maaskofu nchini Papua Guinea Mpya na Visiwa vya Salomoni walioutoa kwa ajili ya mwaka 2020 katika mpango wao wa kichungaji, ambao wameupatia kaulimbiu:“Walei wakatoliki:wamefundwa kwa ajili ya utume”.

Mpango huo unataka kupeleka mbele kazi ya ubunifu na ujenzi” kuanzia na ushirikishwana binafsi na tafakari juu ya Maandiko Matakatifu kwa namna kwamba Neno la Mungu ligeuke kuwa uhai wa kuishi. Ushuhuda wa kikristo unajieleza awali ya yote katika upendo na umakini kwa jirani. Na ndiyo maana ya kutoa ili kuweza kupokea. Lengo lao kuu  ni kufikia hawa waliobaguliwa kama maskini, wafungwa, wakimbizi, wenye kuathirika na madwa ya kulevya na watoto wa mitaani.

Kwa maana hiyo katika ujumbe wao, maaskofu wanakazia kwa waamini kuwa: Tunapaswa kufungua mioyo yetu, kuguswa na kuhamasisha wengine katika kuelekea kwa wale ambao wanahitaji zaidi yetu sisi na ili waweze kufanya uzoefu  nao wa furaha ya pamoja na kupeleka tabasama katika nyuso zao.

Zaidi Maaskofu wa Papua Guinea Mpya kwa mwaka 2020 utakuwa ni wa kujikita kutafakari kwa kina na kuhamasisha waamini walei juu ya mada ua utunzaji wa mazingira, katika mwanga wa Wosia wa Laudato Si kuhusu utunzaji wa mazingira na viumbe vyote. Hata hivyo kwa dhati Umoja wa Mataifa mwaka 2020 umewekwa  katika mada ya “Afya ya mimea “  (IYPH) kwa  madhumuni ya kutaka kukuza na uhamasishaji juu ya umuhimu wa afya ya asili katika kushughulikia maswala ya ulimwengu, kama vile njaa, umaskini, vitisho kwa mazingira na maendeleo ya kiuchumi.

Hatimaye Kanisa katoliki nchini Papua Guinea Mpya linahamasisha baadhiya semina zenye kauli mbiu: “Geuka kuwa kijani na hakikisha usafi”, kwa  lengo la kufundisha kila mmoja awez sehemu ya kulinda sayaeiyetu na kuhifadhi kwa ajili ya kizazi kijacho. Amethibitisha hayo Padre Ambrose Pereira, Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu nchini Papua Guinea mpya na Visiwa vya Salomon.

04 January 2020, 12:31