Tafuta

Vatican News
Papa Francisko tarehe 17 Januari 2020 amekutana na Rais wa Jamhuri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC),Bwana Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo Papa Francisko tarehe 17 Januari 2020 amekutana na Rais wa Jamhuri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC),Bwana Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo  (ANSA)

Papa Francisko amekutana na Rais wa Congo DRC Bw. Tshisekedi!

Ijumaa tarehe 17 Januari 2020 katika ukumbi wa Kitume Papa Francisko amekutana mjini Vatican na Rais wa Jamhuri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC),Bwana Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo,na baadaye akukutana na Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican,akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Bwana Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Ijumaa tarehe 17 Januari 2020 katika ukumbi wa Kitume wa Vatican na baadaye akukutana na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.  Katika mazungumzo yao, wamepongezana juu ya ushirikiano na mahusiano mema yaliyopo baina ya nchi hizo mbili na hasa katika mkataba wa uhusiano wa nchi hizo. Aidha kwa kuona pia mchango mkubwa wa Kanisa Katoliki utolewao katika Jamii ya nchi hiyo kwenye hatua za mchakato wa maendeleo ya Taifa katika mantiki ya elimu na afya.

Baadaye wamezungumzia juu ya baadhi ya mada zinazohusiana na hali halisi kijamii na kisiasa nchini humo. Wamesisitizia juu ya mantiki zenye tabia ya kimataifa kama vile amani, usalama na ulazima wa mshikamano wa pamoja ili kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali za maisha. Katika mazungumzo hayo pia wametazama hali halisi ya sasa kwa namna ya pekee mateso ya watu wa mikoa ya Kaskazini kutokana na kuwepo wa migogoro ya kisilaha na kuenea kwa vurus vya Ebola. Dharura ya ushirikiano kwa ngazi ya kitaifa aa kimataifa katika kulinda hadhi ya kibinadamu na kuhamasisha kuishi kwa pamoja kuanzia na idadi kubwa ya wahamiaji na watu waliorundika na ambao wanakumbana na dharura kubwa ya kibinadamu, ni sehemu iliyoweza kuchukua nafasi ya mazungumzo yao.

Hata hivyo katika ukumbi wa Kitume Vatican Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, wamebadilisha zana za mkataba wao kati ya Vatican na Jamhuri ya DRC Rais wa Jamhuri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Bwana Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, na baadaye kukutana na Kardinali. Huu ni mkataba uliotiwa saini Mjini Vatican kunako tarehe 20 Mei 2016.  Katika afla hiyo walikuwpo pia Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican, Askofu Mkuu Ettore Balestrero Balozi wa Vatican nchini DRC, Askofu Maercel Utembi, Rais wa Baraza la Maaskofu DRC (CENCO), Monsinyo Mislav Hodzić, Mislav Hodzic, Mshauri wa Balozi katika Ofisi ya Ukatibu Mkuu Vatican, Padre Donatien Nshole Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu DRC. Kwa upande wa Jamhuri ya Kidemomrasia Congo alikuwapo; Bi Marie Tumba Nzeza, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya nchi za Nje Fortunat Biselele, Mshuri wa Rais Bwana Pacifique Kahasha,  Mhusika wa utume wa Mkuu wa nchi Bwana JeanPierre Hamuli Mupenda,ambaye ni Balozi wa Drc anayewakilisha Vatican.

17 January 2020, 13:53