Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Kaigama wa Jimbo Kuu katoliki anasema kuwa haki na amani ni dada pacha hivyo, anatoa ushauri wa kufanya jitihada hai katika majadiliano ya kidini na imani na uadilifu viambatane Askofu Mkuu Kaigama wa Jimbo Kuu katoliki anasema kuwa haki na amani ni dada pacha hivyo, anatoa ushauri wa kufanya jitihada hai katika majadiliano ya kidini na imani na uadilifu viambatane 

Nigeria:majadiliano ya kidini ni zana msingi wa amani na haki!

Askofu Mkuu Kaigama nchini Nigeria wakati wa hotuba yake kwenye Jukwa la majadiliano ya kidini lilofanyika Jimbo kuu Abuja ametoa mfano kuwa haki na amani ni kama dada pacha hivyo,anatoa ushauri wa kufanya jitihada katika majadilianoili iwe ndiyo njia ya kufuata na kuonya dhidi ya kutumia dini kama silaha ya uchochezi,migogoro,vurugu,ubaguzi na ukorofi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Haki na amani ni dada pacha. Kwa msemo huo Askofu Mkuu Ignatius Kaigama, wa Jimbo Kuu katoliki la Abuja, nchini  Nigeria, ameutumia wakati anatoa hotuba yake katika Jukwa la Tatu kwa  2020 la majadiliano ya kidini kwa ajili ya amani, uliofanyika katika jimbo kuu lake kuanzia tarehe 21-23 Januari 2020. Tukio la jukwa hili limeongozwa na kauli mbiu Majadiliano ya kidini: kuongeza jitihada za utamaduni wa amani  haki na mapatano”

Katika hotuba ya Askofu Mkuu Kaigama, anatoa ushauri wa kufanya jitihada hai katika majadiliano ili iwe ndiyo njia ya kufuata na kutoa wito makosa ya  kufanya dini kama silaha ya chochezi, migogoro, vurugu, ubaguzi na ukorofi, aidha kutoa onyo dhidi ushabiki wa dini. Askofu Mkuu Kaigama amesema: “Hatupaswi kutoa ruhusa, ya tamaa ya mafundisho ya uongo, madaraka na ukuu wa kikundi kimoja cha kidini dhidi ya kingine, pia kupitia vyombo vya kisiasa au rasilimali za kiuchumi”.  Aidha anaongeza kusema: “Kinyume chake, inahitaji kuelewa kwamba imani na uadilifu lazima viambatane katika mazoezi ya kidini, vinginevyo dini inakuwa dhihirisho la hisia na hisia mbaya”.

Katika hili ndipo anatoa wito wa nguvu  kuwa: “Hatuwezi kuruhusu dini kutumiwa kuvuruga jamii, kusababisha machafuko ya kijamii au hata kuua”.”Nchini Nigeria, hasa, “Wakristo na Waislamu wanapaswa kuungana kwa nguvu kwa jina  la wema wa pamoja, badala ya kuumizana mmoja na mwingine  na hivyo kupinga  ubaguzi”.  Katika muktadha huo, mazungumzo yanayohusiana na yanayoeleweka amesema kama: “uelewa na kuheshimiana ambao unaruhusu sisi kuishi na kushirikiana licha ya tofauti zetu tulizo nazo, unakuwa muhimu kwa kukuza amani, kwa sababu tunashukuru kwamba kuta zinazogawanya ambazo ziko kati, kati chanzo chake ni migogoro mingi”. Amesisitiza Askofu Kaigama.

Hatimaye, Askofu Mkuu wa Abuja amewaalika  viongozi wa dini, huku akiwahimiza kujikita katika kupinga  moyo wa ushabiki kupitia uundaji wa vituo vya majadiliano  katika jamii zote na kwa maana hiyo anasema “ na ikiwezekana, ni kuanzisha Wizara ya Shirikisho la majadiliano na mapatano”. “Tunahitaji kwa dharura ule utamaduni wa majadiliano halisi ya uhusiano, na ambayo haki, amani na maridhiano vinapatikana” amesisitiza.

Jukwaa la majadiliano ya kidini kwa ajili ya amani (IDFP liliundwa kunako februari ya 2016,) ambalo  ni shirika lisilo la kiserikali la mazungumzo,  kiutendaji na ya kitamaduni ambayo kama lengo lake kuu ni kufanya umoja wa amani kati ya dini za Nigeria; kuondoa fikra, kupunguza vurugu, kujenga uelewa na kuruhusu ushirikiano, wakati huo huo kudumisha na  kuheshimiana baina ya vikundi tofauti vya dini, na ambazo  ni zana zinazotumiwa na Baraza kila siku kutekeleza jukumu lake.

28 January 2020, 15:16