Tafuta

Makanisa ya kiorthodox wameadhimisha Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana tarehe 7 Januari Makanisa ya kiorthodox wameadhimisha Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana tarehe 7 Januari 

Makanisa ya nchi za Mashari waadhimisha Noeli!

Ni wakristo wengi na sehemu kubwa wa Kiorthodoz ambao wanaadhimisha Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana tarehe 7 Januari 2020.Katika mahojiano na Padre Boules Garas anazungumzia juu ya mantiki ya mivutano ya kijamii huku akitoa heri na matashi mema ya kuweza kuwa na amani nchini Misri na kwingineko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican City

Tarehe 7 Januari 2020 ni Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa makanisa yote  katoliki ya Mashariki na Makanisa ya Kiorthodox ambayo yanafuata kalenda ya Kiujualini. Makanisa hayo ya ni ya  Mashariki pia Katoliki-Kigiriki ya Ukrain na kwa ajili ya wakristo wa kiothodox wanaoishi Urusi, Bielorusi, Serbia, Kroazia, Macedonia na nchi nyingine. Kwa namna ya pekee nchini Misri wakatoliki Jijini Cairo na Alessandria na wilaya zake wameadhimisha tayari siku ya tarehe 25 Desemba wakati wale wanaoishi Misri ya Kaskazini wanaadhimisha tarehe 7 Januari 2020 pamoja na waorthodox wengine. Katika wilua ya Minya nchini Misri wakoptiki- waorthodox mwaka huu wamekuwa na sababu ya furaha hasa ya uzinduzi, wa Kanisa la Anba Moussa al-Asswad, tarehe 5 Januari 2020  lililokarabatiwa hivi karibuni. Ni moja ya makanisa 84 ambayo yaliharibiwa kunako mwaka 2013 baada ya mapindizu ya Serikali ya kijeshi tarehe 3 Julai  na kumweka rais wa udugu Mohamed Morsi. Ukarabati wake na kurudishwa kwa ibada, unajenga ndani ya mioyo ya wakristo wote ile ishara ya matumaini.

Naye Padre Boules Garas, Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa nchini Misri ni padre mkatoliki ambaye anaishi Cairo akizungumza kwa simu katika studio za Vatican News  ameelezea hali halisi ambayo imewaongoza katika maadhimisho ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ,na matumaini kwa ajili ya tarehe 7 Januari 2020 katika kwa ndugu waorthodox  na hali halisi ilivyo ya nchi yao. Padre amesema kuwa katika maadhimisho ya usiku  wa kuzaliwa kwa Bwana alijiuliza kwa nini kumekuwapo na ulinzi mkali namna hii ukizunguka Kanisa lao katika parokia yao. Alitoka nje na kukutana na polisi wengi ambao walimwomba awatume skout wawe pamoja na polisi kwa maana aliambiwa wanwafaha,u watu na ili kuweza kushirikiana nao wakati wa ukaguzi wa mikoba ya wanawake. Padre alijiuliza kwa nini kuwa na hofu bamna hii? Tunaishi nchi ya utulivu. Lakini wao walimwambia kuna mivutano mingi sana inayowazunguka na ilikuwa ni lazima kukaa makini. Lakini wao waliweza kuadhimisha kwa utulivu misa yao na Kanisa lilikuwa limejaa  na sikukuu ilikuwa nzuri. Ni matarajio kwamba kila kitu sasa kinaweza kwenda  vizuri hata sherehe za tarehe 7 Januari katika Misri ya Kaskazini.

Yeye kama Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa nchini Misiri , uhusiano uliopo kati ya wakatoliki na waorthodox anasema, wanafanya mchakato wa hatua mbele ya pamoja na kuheshimiana. Yeye alitembelewa na Patriaki wa Kiorthodox yaani Papa Tawadros II, tarehe 25 Desemba alipofika kuwatakia matashi memna na heri za Sikukuu akiwa na Patriaki Katoliki Ibrahim Isaac Sidrak  na maaskofu wengine,na hivyo Yeye binafsi anataweza kwenda tarehe 7 Januari kuwatakia matashi mema Papa Tawadros. Hii yote ni kuonesha uhusiano mwema uliopo na wakaristo ambao unazidi kuwa bora na hatua ya mbele madhubuti. Hata hivyo akibainisha ni kwa jinsi gani wakatoliki wakati wanaadhimisha tarehe mbili tofauti kwa mujibu wa Kanisa, amesema , kwa urahisi ni kwamba wakaristo walioko Misri Kaskazini ni wachache. Na ndiyo  uchache huo pia kuna wakatoliki. Ndani ya familia moja unaweza kukuta mjumbe mmoja mkatoliki na muorthodox. Na kwa maana hiyo wanaadhimisha pamoja ili wakatoliki wasiadhimisha peke yao huko Kaskazini mwa Misri, na bila hivyo wasingeweza kujihisi katika hali ya kuwa katikati ya watoto na kati ya watu. Kwa kuungana pamoja, wakatoliki, waorthodox na waprotestani wanaadhimisha kwa pamoja tarehe 7 na sikukuu inakuwa nzuri kwa pamoja.

Katika Bibalia, Misri inatajwa kama mahali pa ukarimu na hata  katika Agano Jipya ambapo wanataja Maria na Yosefu walipokimbiza mtoto kufuatia na mateso ya Herode. Utambuzi huu katika dhamiri ya Kanisa la Kikopti ikoje? Padre anasema katika fursa ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Familia Takatifu, aliandika kuwa makaribisho ni sehemu muhimu ya utamaduni wao wa nchi za Mashariki. Wao wamekaribisha zaidi ya milioni 3 za watu kutpka Sudan ambao hadi sasa wanaishi nchini Misri. Wamewapokea watu kutoka Siria, na Palestina, na hawajawahi kutengeneza kambi za wakimbizi, kwa maana wao wanawaona kuwa ni ndugu na wanapata kazi na kufanya nao kwa pamoja na kufanya biashara katika barabara na hawahisi kuwa wageni au wakimbizi nchini Misri.

Na zaidi amesema ipo mitaa katika miji mingi ambayo unakuta karibu ni watu kutoka Siria au Iraq, wote hao wamekirimiwa, na kwa maana hiyo kile ambacho Biblia inasema ni ishara kwao ya kuendeleza msimamo huo kwa maana, kwanza walimakaribisha Yosefu, Yakobo na koo 12 za Israeli. Kukaribisha kwa upande wao ni ishara ya kikristo na ya Injili ya kina. Kwa kuhitimisha mahojiano, Padre Boules Garas, anatoa matashi mema ya mwaka mpya ili uwe wa amani na matumaini. Katika nchi za Mashariki kuna hali ya hewa ya wasiwasi mkubwa; nchini Libia, ukanda wa Ghaza mashariki, Sudan Kusini, Uturuki, Iraq, Iran  na kwa njia hiyo,kuomba utulivu na amani ndiyo jambo msingi kwa wakati huu na daima.

07 January 2020, 16:12