Tafuta

Vatican News
Ufanisi wa kichungaji hauna msaada wowote ikiwa mtu hafanyi kama walivyofanya Mamajusi yaani haondoi ubinafsi wake na kuamua kumwabudu Mungu katika ukweli. Ufanisi wa kichungaji hauna msaada wowote ikiwa mtu hafanyi kama walivyofanya Mamajusi yaani haondoi ubinafsi wake na kuamua kumwabudu Mungu katika ukweli.   (ANSA)

Kuabudu ni kujiachia mwenyewe kupendwa na Yesu!

Katika mahojiano na Askofu mkuu Bruno Forte wa jimbo kuu katolili la Chieti-Vasto Italia, amekazia juu ya tafakari ya Papa Francisko aliyoitoa Siku ya Tokeo la Bwana tarehe 6 Januari 2020 iliyokuwa inakazia juu ya mada kuabudu hasa kwa kufuata nyayo za mamajusi ili kugundua tena umuhimu wa kuabudu.

Na Richard Kashinje - Vatican

Wakati wa Misa, iliyofanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Vatican, Papa Francisko alitoa mwaliko wa kujiuliza swali hili muhimu: Je! Mimi ni mwabudu Kristo? Katika kujibu amesisitiza kwamba nadharia ya uchungaji na ufanisi ni kidogo au “hakuna kabisa ikiwa haifanyiki kama walivyofanya Mamajusi. Papa Francisko anaelezea “Kwa kuabudu tunagundua kuwa maisha ya Kikristo ni hadithi ya upendo na Mungu”. Aidha alihimiza kugundua hitaji hili la imani ili kanisa liweze kukua katika sala na kuabudu. Papa Francisko alisema kuwa ili kujua uso wa Yesu tunapaswa kukaa mbele ya uso wake. Kwa kuabudu, tunagundua kuwa maisha ya Kikristo ni hadithi ya upendo na Mungu, ambapo maoni mazuri hayatoshi, kinachotakiwa ni kumweka Kristo katika nafasi ya kwanza maishani mwetu. Wanaoabudu wako kwenye kizingiti cha umilele. Akinukuu maneno ya Papa Francisko, Askofu mkuu Bruno Forte amesisitiza kwamba kuabudu ni kujiachia kupendwa na Mungu.

Wale wanaoabudu wako kwenye kizingiti cha umilele

Wale wanaoabudu wanaishi uhusiano wa upendo na Mungu unaobadilisha maisha yao yote. TaaliMungu, ufanisi wa kichungaji hauna msaada wowote kama mtu hafanyi kama walivyofanya Mamajusi, ikiwa mtu hajifunui mwenyewe ili aweze kukutana na Mungu. Askofu Mkuu Forte pia anasema kwamba "hali ya mwelekeo wa maisha yote ya Kikristo ni kwenda kwa Bwana". Kwa hali hiyo wale wanaoabudu wamesimama kwenye kizingiti cha umilele, ambao ni, kujiweka mbele za Mungu. Wao wanakubali kukaribishwa katika uhusiano wa kimungu; wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Askofu mkuu anaongeza kuwa, kupoteza maana ya kuabudu, inamaanisha kupoteza hali ya mwelekeo wa maisha yote ya Kikristo ambayo yanakwenda kwa Bwana na sio vinginevyo. Ni maisha ambayo kwa kizingiti kila siku huenda kwa Bwana na inakaribisha kuja kwake mioyoni mwetu na katika maisha yetu.

Wale wanaoabudu hujifunza kukataa Mungu asiye wa kweli

Papa Francisko pia alikazia kuwa kwa kuabudu mtu hujifunza kukataa kile kisichopaswa kuabudiwa kama vile "Mungu wa pesa, Mungu wa matumizi, Mungu wa raha, Mungu wa mafanikio, pamoja na ubinafsi wetu. Papa Francisko alimtaja Herode ambaye anatumia kitenzi "kuabudu" na kumbe ndani mwake alikuwa na nia ya kumwangamiza mtoto, jambo ambalo ni ibada ya udanganyifu. Badala ya kuabudu Mungu, mtu hujiabudu mwenyewe ama kitu kingine. Hali hii ni kumtumia Mungu badala ya kumtumikia. Aidha Papa anasisitiza kwamba bila kuondoa ubinafsi wetu, kurudia nia ya upendo, huruma na bila kweli kukutana na Mungu na kukutana naye katika sala na kwa wengine, basi maisha ya Kikristo hayatimizwi. Kwa maneno mengine, taaliMungu, ufanisi wa kichungaji hauna msaada wowote ikiwa mtu hafanyi kama walivyofanya Mamajusi yaani haondoi ubinafsi wake na kuamua kumwabudu Mungu katika ukweli.

Kuna wakristo wasiojua kuabudu

Akitoa mwito kwa wakristo wengi ambao hawajui jinsi ya kuabudu, Papa anakazia kuwa kuabudu ni kujiachia mwenyewe kupendwa na Mungu na wakati tunajiruhusu kupendwa na Mungu, Bwana anatimiza kile alichonuia ndani mwetu. Wale wanaoabudu wanaishi uhusiano wa upendo na Mungu ambao hubadilisha maisha yao yote. Hivi ndivyo mamajusi walipata uzoefu. Ikiwa wewe sio mwabudu Mungu, wewe sio mwanafunzi wa Yesu ambaye alikuwa mwabudu wa ubora, mtu anayeshikilia kizingiti kati ya wakati na umilele, kati ya Mungu na mwanadamu.

ASK.FORTE
08 January 2020, 12:18