Tafuta

Vatican News
Ongezeko la asilimia 50 ya wakatoliki nchini Korea Kusini kwa miongo miwili imekolezwa hata kutokana na ziara ya Papa Francisko kwa miaka ya hivi karibuni Ongezeko la asilimia 50 ya wakatoliki nchini Korea Kusini kwa miongo miwili imekolezwa hata kutokana na ziara ya Papa Francisko kwa miaka ya hivi karibuni  (ANSA)

Korea Kusini:ongezeko la wakatoliki ni karibia 50% kwa miongo miwili!

Idadi ya wakatoliki nchini Korea ya Kusini imeongezeka kwa karibia asilimia 50 katika miongo miwili iliyopita.Shukrani kubwa kutokana na chachu iliyokolezwa na ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini humo ya miaka ya hivi karibuni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Idadi ya Wakatoliki nchini Korea Kusini imeongezeka kwa karibu asilimia 50 katika miongo miwili iliyopita, ingawa kiwango hiki cha ukuaji kimepungua katika miaka ya hivi karibuni, inaripoti gazeti la Herald, nchini Korea Kusini, likionyesha ripoti hiyo mpya kutoka Taasisi ya Kichungaji Katoliki ya Korea. Mnamo 2018 kulikuwa na Wakatoliki wa Korea Kusini 5,866,510, ikilinganishwa na 3,946,844 kwa mwaka 1999, kwa ongezeko la 48.6%. Katika kipindi hicho, asilimia ya Wakatoliki nchini imepita  kutoka asilimia 8.3 hadi 11.1%.

Ongezeko la Wakatoliki kwa miaka ya hivi karibuni ni baada ya ziara ya Papa Francisko

Ripoti hiyo, hata hivyo, inabaini kuwa kiwango cha ukuaji halisi kimepungua chini ya asilimia 1 katika miaka ya hivi karibuni. Kinyume chake kwa kulinganisha, kunako  2000 na 2001, idadi ya Wakatoliki iliongezeka kwa asilimia 3.2 na 3.9 kwa mtiririko huo huo. Kiwango cha ukuaji zaidi kilishuka hadi chini ya asilimia 2 mwaka 2009, na kufikia asilimia 1.7 kunako 2010, kabla ya kuongezeka kwa asilimia 2.2 mnamo 2014.  Hata hivyo ukuaji huu umetokana na ziara ya Papa Francisko nchini  Korea Kusini katika mwaka huo.

Ni wakati wa kutafakari juu ya utendaji wao wa kimisionari

Wakati huo huo, idadi halisi ya Wakatoliki ikiwa imeongezeka, lakini maudhurio ya watu wengi yamepungua kanisani kutoka asilimia 29,5 hadi asilimia 18.3 katika kipindi kama hicho cha 1999-2018. Majimbo yote yamefanya juhudi mbali mbali za kuwarudishia Wakristo lile vuguvugu na ari katika Kanisa na kuiboresha namna ya utendaji wa utume, lakini mabadiliko makubwa bado yanapaswa kufika. Na tatizo hili linajirudia kila mwaka. Na kwa maana hiyo, ripoti imebainisha kuwa: “Ni wakati wa sasa wa kutafakari juu ya kazi yetu utume wa umisionari na kufikiria tena mwelekeo wa uinjilishaji mpya wa kitaifa kwa ajili ya watu wa Mungu katika kukiri imani yao kwa dhati.

14 January 2020, 10:22