Tafuta

Vatican News
Baraza la Umoja wa Maaskofu wa Ulaya(Comece)katika mahojiano na Vatican News linatoa wito wa nguvu kuhusu majadiliano kama zana ya kuokoa ubinadamu dhidi ya tishio la kivita nchin Iraq, Libia na kwingineko Baraza la Umoja wa Maaskofu wa Ulaya(Comece)katika mahojiano na Vatican News linatoa wito wa nguvu kuhusu majadiliano kama zana ya kuokoa ubinadamu dhidi ya tishio la kivita nchin Iraq, Libia na kwingineko  (AFP or licensors)

Askofu Youssefu Soueif atoa wito wa amani kwa Iran na Iraq

Askofu mkuu Youssef Soueif,Mkuu wa Kanisa la Maroniti huko Cipro na Mwakilishi wa Baraza la Umoja wa Maaskofu wa Ulaya(Comece)katika mahojiano na Vatican News anatoa wito wa nguvu kuhusu majadiliano kama zana ya kuokoa ubinadamu dhidi ya tishio la kivita katika kipindi hiki nyeti cha kimataifa ambacho ni vita vya tatu vya dunia vinavyobish tayari mlangoni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maaskofu wa Ulaya wanafanya uchambuzi juu ya kuongezeka kwa wasiwasi mkubwa unaotokana na kipeo kati ya Iran na Marekani. Na huu  ni ukatili wa vurugu nchini Iraq na kudumu kwa vita nchini Libia kwa  maana hiyo wanatoa wito wa nguvu ili majadilaino  yaweze kuwapo kwa ajili ya amani. Haya yamezungumzwa na Askofu Mkuu Youssef Soueif, wa Kanisa la Kimaronito huko Cipro ambaye pia ni Mwakilishi wa Baraza la Umoja wa Maaskofu Ulaya. Tume ya Baraza la Maaskofu wa Jumuiya ya Ulaya, kwa dhati wanaomba kwa haraka uwepo mkataba wa makubaliano ili kuweza kuepuka vita vya dunia ambayo wanaolipa gharama yake ni watu wasio kuwa na hatia, watu wasio na silaha yaani watu rahisi tu na dhaifu katika sayari hii.

Majadiliano ndiyo chombo cha kuepusha janga la kipeo cha kivita duniani

Katika mahojiano  Askofu Soueif, anasisitiza kwamba, Kanisa la Ulaya linaunga mkono kuhusu wito wa Papa Francisko kwa ajili ya amani ambao amerudia kuutoa wakati wa  hotuba yake alipokutana  na mabalozi wawakilishi wa nchi zao Vatican, katika fursa ya kutakiana heri na na baraka za Mwaka mpya 2020. Akisisitiza Askofu Mkuu Soueif,  amesema kwa hakika majadiliano ndiyo yanabaki kuwa zana msingi ya kuweza kuondokana na janga la kipeo hiki  kinachoitazama sayari nzima.

Awali ya yote hawa wanapaswa kuweka matakwa ya watu kuliko yao binafsi

Viongozi hawa wanapaswa kuweka matakwa ya watu kwanza kabla ya mipango yao na ndilo  jukumu msingi. Kinyume chake ni wazi vita ya tatu dunia inaingia hata kama mwa mtazamo wa haraka ni kuonekana kubisha hodi tayari katika milango. Jambo hili ni la kufanywa kwa makini ambalo linahitaji kuwa na hekima na tafakari amebainisha na ili kuweza kuondoa hatari inayoweza kuikabili dunia nzima. Kanisa la Ulaya, amesisitiza Askofu Mkuu kwamba litaendelea na msimamo wake thabiti wa hitaji kubwa la kuendeleza mchakato wa kutafuta amani kwa njia ya matendo yake yake ya kila siku katika mabara na katika hali halisi ya ushuhuda wa makanisa mahalia.

11 January 2020, 15:56