Tafuta

Vatican News
Baraza la Maaskofu Italia wametangaza toleo Jipya la Misale ya waamini iliyo badilishwa sala ya Baba Yetu na sala ya Utukufu Baraza la Maaskofu Italia wametangaza toleo Jipya la Misale ya waamini iliyo badilishwa sala ya Baba Yetu na sala ya Utukufu   (© 2018 Catholic News Service)

Toleo jipya la CEI kuhusu Baba Yetu kuanzia 29 Novemba 2020!

Askofu Mkuu Bruno Forte wa Jimbo Kuu katoliki Chieti-Vasto na Mtaalimungu ametangaza tarehe za kutolewa kwa Misale mya ya waamini iliyobadilishwa sala ya Baba Yetu na Utukufu na kuelezea sababu zilizotoa msukumo wa maaskofu wa Italia kubadili neno Usitutie kishiwishi” kwamba Mungu anatupenda hawezi kutuwekea mitego ili tuangukie dhambini.

Askofu Mkuu Bruno Forte wa Jimbo Kuu katoliki Chieti-Vasto, Mtaalimungu  na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Mkoa wa Abruzzo –Molise ametangaza tarehe za kutolewa kwa Misale kwa toleo jipya litakalo kuwa na sala ya  Baba Yetu kwa mujibu wa Baraza la Maakofu Katoliki Italia ambayo itatolewa siku moja baada ya Pasaka. Katika maelezo zaidi wanasema katika sala iliyokuwa inatumika  kumwomba Mungu asitutie majaribuni imebadilishwa kwa tafsiri inayofaa kabisa isemayo usituachie majaribu. Hii itaanza kutumika katika liturujia kuanzia Misa za tarehe 29 Novemba 2020 kwa maana ya Dominika ya kwanza ya Majilio.

Askofu Forte akijibu ni kwanini maaskofu wa Italia wameamua kubadilisha sala hiyo ya kizamani naijulikanyo kwa wakristo anasema ni kubaki katika uaminifu kwa  malengo yanayo fafanulia na sala ya Yesu na asili ya kigiriki. Kwa hakika katika asili ya kigiriki, neno hili katika kuandika ‘portarci’,  ‘condurci’ yaani 'kutuchukua', 'kutuongoza'. Tafisri ya lugha ya kilatino, ‘inducere’ ikiwa na maana kututia, ilikuwa inaangazia neno la kigiriki. Lakini katika lugha ya kiitaliano,  ‘indurre’ ikiwa na maana ya ‘kusukuma’  kwamba iwezekane. Kwa njia hiyo inakwenda kinyume kuwa Mungu hawezi kamwe kutusukuma kuanguka katika majaribu. Kwa njia hiyo tafisri ya usitutie majaribuni, siyo sahihi.

Hoja hii pia imewekwa hata katika katika mabaraza yote  ya maaskofu katoliki  duniani. Kwa mfano nchini Uhispania, lugha inayotumiwa na wakatoliki wengi katika sayari hii wanasali :usituache  tuanguke katika majaribu. Wafaransa baada ya majadala mkubwa, walipata tafsiri yao tayari inayotumika  sasa kwamba usituache tuingie katika majaribu. Kutona na maelezo hayo, ni wazi kwamba Mungu ambaye ni Mungu mwema, mwenye upendo mkuu, anafanya kila njia ili watoto wake wasianguke katika majaribu.

Kutokana na sababu hizo maaskofu wa Italia wameamua kwenda sambamba na maandiko matakatifu  ya Biblia rasmi na lugha ambaye inapendelewa ya toleo la mwisho lisemalo:usituache tuanguke majaribuni. Na hii ni tafsiri ni nzuri kwa maana  ya kuondoa kitu chochote au mtu yoyote anayetaka kutuingiza tufanye ubaya au kututengenisha na muungano na Mungu. Ndiyo maana kielelezo cha majaribu ni tafsiri sahihi ya neno ambalo lazima liweze kutufanye tuelewe kwamba Mungu wetu anayetukimbilia na anayetusaidia, hawezi kutufanya tuingie majaribuni; na siyo Mungu ambaye  anaweka mitego. Hili ni wazo lisilokubalika. “Kimsingi, mabadiliko ni mdogo. Sidhani kama kuna shida yoyote kubwa ya kutoeleweka. Lazima tuwasaidie watu kuelewa kuwa siyo suala la kutaka mabadiliko yenyewe, bali ya kubadili namna ya kusali kwa uangalifu zaidi na karibu na nia ya Yesu”. Amesisitiza hayo Askofu Bruno Forte.

29 January 2020, 15:35