Tafuta

Vatican News
Amani nchini Afrika ya Kati inawezekana lakini inahitaji utashi wa sehemu zote kunzia awali ya yote na raia kwa ujumla na pia kwa msada wa Jumuiya ya kimataifa! Amani nchini Afrika ya Kati inawezekana lakini inahitaji utashi wa sehemu zote kunzia awali ya yote na raia kwa ujumla na pia kwa msada wa Jumuiya ya kimataifa!  (AFP or licensors)

Afrika ya Kati:Amani na mapatano bado vinawezekana!

Kusaidiwa na Jumuiya ya kimataifa, juhudi za serikali na jibu la wazi kwa wazalendo wote bila ubaguzi katika utendaji kwa ajili ya ustawi wa pamoja, hasa kutafuta amani na mapatano.Ndiyo masuala ya Padre Mathieu Bondobo akibainisha juu ya uwezekano wa kuleta amani katika nchi mra baada ya tamko la maaskofu japokuwa anasema “Wakristo bado wanakabiliwa na jeuri na mateso”.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Kanisa ambalo ni hai na linalotaka kutembea laki nina laibiliwa na udhaifu na kutishiwa japokuwa linaalikwa kuzingatia hali halisi ya mantiki ngumu na janga ambalo linatokana na vita vya ndani ya nchi. Licha  kuwekwa kwa mikataba ya makubaliano ya kisiasa bado nchi imekabiliwa na matukio mengi ya kutisha, ya misuko misuko ya kutumia silaha. Ndivyo Padre  Mathieu Bondobo, Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Bangui katika Jamhuri ya chini Afrika ya Kati na Paroko wa Kanisa Kuu na ambaye alimsindikiza hata Papa Francisko wakati wa  ziara yake ya kitume nchini humo kunako mwaka 2015, akijaribu kuelezea jinis Kanisa lake la Afrika ya Kati linavyojikita katika harakati za kutafuta maridhiano ya amani.

Padre Bondobo, ambaye ameshiriki Mkutano wa Baraza maaskofu nchini Afrika ya Kati ulioanza tarehe 12 Januari 2020, amegusia hata ujumbe wa Maaskofu uliotolewa mara baada ya mkutano huo na hivyo kuwa msemaji mkuu katika hali ya upyaisho wa imani na matumaini. Hata hivyo Mkutano wa Maaskofu, umefanyika katika mantiki ya kuadhimisha miaka 125 tangu kuanzishwa kwa uinjilishaji nchini humo.

Padre Bondobo amethibitisha kwamba amani ya nchi ya Afrika ya Kati inawezekana lakini unahitajika mchakato wa kiufundi katika kujenga hatua moja baada ya nyingine kutoka kwa mchango wa watu wote wa taifa na kimataifa. Padre amesema Kanisa la Afrika ya Kati daima liko hai na linatenda shughuli yake ya kichugaji ya uinjilishaji kila siku. Na hiyo anaongeza “Wanaona daima Kanisa ni kijana, lakini hata kutokana na  tabia ya ushiriki wa waamini wengi katika maadhimisho ya Ekaristi. Vipo vyama vingi vya kidugu katoliki ambavyo vinajihusisha katika nchi hiyo na kutafuta kuishi roho ya mtakatifu wa kiume au kike kwa namna ya kila mmoja anavyojaliwa; maadhimisho ya sakramenti ya ubatizo ni mengi na maadhimisho ya lirutujia nyingi katika majimbo yote ,  hata wakati mwingine  ambao kila sehemu wanaonekana kuwa na  nguvu ya roho Mtakatifu inayowafanya kutafuta namna ya kupanda yaliyo mema. Lakini wakati huo huo kwa hakika Kanisa ni dhaifu ambapo leo hii kuna hali ya kukabiliana na hali hasi ya janga la vita na ghasia za kutisha .

Maaskofu wametuma ujumbe wao kwa wahudumu wa kichungaji, kwa jumuiya za Kikristo, kwa vijana, wasiasa, makundi ya kisilaha,na jumuiya za kimataia huku wakiomba kwa mara nyingine tena wote , kufanya kazi kwa ajili ya maridhiano  na amani  ya kitaifa kwa maana watu bado wanaishi katika mantiki ya ukosefu wa usalama na na hofu. Na hii ni kwa sababu maaskofu wamezungumza kwa wale ambao wamepokea ubatizo na kuwaomba wawe mashuhuda wa kweli, wawe mwanga wenye uwezo wa kuangaza katika kila mantiki. Hata wale ambao wako katika sekta za sera za kisiasa wanapaswa kushuhudia imani yao, kwa maana maaskofu wanabainisha kuwa ni hatari sana kuona  kwamba kati yao kuna wabatizwa ambao pamoja na taaluma yao waliyo nayo na maisha ya kikristo, wengi wanakimbilia katika uchawi, ushirikina, ufisadi, rushwa na mambo mengi yanayokwenda kinyume na kukiri kwao.

Wale ambao wanajitambua ni wa Kanisa, lazima wapeleke mwanga kwa njia ya matendo mema na siyo tu kwa sababu wanatambua vema kuwa hali halisi ya nchi ya Afrika ya Kati siyo rahisi. Wako mbele ya majanga haya kama anavyeleza: “Tunakabiliwa na pambano la mara kwa mara la silaha ambapo Wakristo wanakabiliwa na dhuluma na  mara nyingi, wengi wamepoteza maisha na lazima wawe na nguvu ili kuishi imani yao kwa sababu kila wakati wanatishiwa, kuuawa, na nyumba zao zinachomwa”. Pamoja na hayo yote “ ni dhahiri kwamba lazima kuishi imani yao japokuwa sio jambo rahisi. Kwa sababu wakati kuna vita, kama wanadamu wakati mwingine, tunaweza kuwa na msukumo wa kulipiza kisasi ikiwa wataua kaka yangu, mama yangu, baba yangu” amesema Padre. Na ndiyo hapa  maaskofu wanaingilia kati, na ujumbe wao, wakisema: “ kuweni makini ili mspoteze tumaini lililo ndani mwetu' na kwamba vita kamwe havitashinda. Ushindi uko kwa Kristo tu, ni yeye aliyeushinda ulimwengu na ambaye ameleta amani, kwa hivyo lazima tupeleke Kristo maishani mwetu na "usiogope wale wanaoua mwili".

16 January 2020, 11:38