Tafuta

Vatican News
Tarehe 20 Desemba ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya mshikamano Tarehe 20 Desemba ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya mshikamano 

Siku ya kimataifa ya mshikamano wa kibinadamu!

Katika siku ya kimataifa ya mshikamano wa kibinadamu,Umoja wa Mtaifa unasisitiza juu ya kutoa thamani hii katika ulimweng na kutoa pendekezo kama misingi ya mahusiano kati ya watu ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa ajili ya wema wa binadamu wote.Kanisa liko mstari wa mbele na ndiyo ishara ya upendo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mshikamano ni neno linalotoa mbiu katika dhamiri ya watu lakini hawa uwajibikaji wa Mataifa yote, katika taasisi za serikali na zile siziso za serika, mashirika ya umma na binafsi. Ndiyo hasa roho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano kibinadamu ambayo ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kunako mwaka 2005 ili kuadhimisha duniani kote kila ifikapo tarehe 20 Desemba ya kila mwaka, ambapo inaangukia katika maandalizi ya siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Hata hivyo kufuatia na tukio hili, ni sambamba na mwaliko kwa wakristo na binadamu wote kuwa na mtazamo makini wa watu hasa wenye kuhitaji msaada wa zana na hata kutia moyo kiroho, kwa kila mahali na hali yoyote ya kibinadamu.

Ni siku ya kuadhimisha umoja wa familia ya mwanadamu

Ni siku ambayo unaadhimisha umoja wa familia ya mwanadamu katika utofauti wake, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ili kukumbusha serikali zote kuhusu kuheshimu jitihada zilizowekwa na mikataba ya kimataifa, kwa ajili ya kuhamasisha maoni ya umma kuhusu umuhimu wa mshikamano na kwa ajili ya kunzisha mambo mengi ambayo yanajikita katika kuondoa umaskini. Amesisitiza hay Mkuu wa Caritas ya Italia alipojihana na Vatican News. Hata hivyo tunapozungumza juu ya mshikamano ni kama vile tunahimiza roho na kwamba iweze kujifafanua katika matendo hai, amesisitiza  Bwana Paolo Beccegato, Makamu rais na mhusika wa kitengo cha eneo la Kimataifa katika Caritas ya Italia. Hii inahusu kutafakari kwa kina juu ya tabia binafsi hadi kufikia zile za siasa kimataifa na hali zake zote za kila mmoja, mikakati na maelekezo ya mambo ya dhati, ya maendeleo na  kwa urahisi wa kila siku. Kwa maana hiyo ni kama njia mbili kuanza ile ndogo hadi kufikia ile kubwa na nyingne kuanzia chini  hadi juu lakini ambayo inatengenezwa na mshikamano ambao una lengo la ukamilifu wa kibinadamu.

Mshikamano kwa nchi zilizo sahaulika

Aidha Mkuu wa Caritas Italia ameelezea juu ya maeneo ambayo kwa namna moja kuna umaskini, vita, ukosefu wa usawa na mahali ambapo kama Caritas wameweze kupanda miradi na mipango ya kidharura au ya maendeleo na daima yenye kuwa na ushirikishwaji mkubwa ambao unawasadia kujifunza mengi kutoka katika makanisa mahalia na ushirikiana kidugu kati ya Makabusa, ambayo inakuwa ni mtindo wa uwepo, ushirikishwaji na mabadilishano ya pamoja na mahali ambapo wao pia wamejifunza kuelewa zaidi na kukabiliana kwa namna ya ujenzi mzuri wa ushirikiano. Nchi hizi wamenzia na zile hasa zilizo sahulika kama vile Sudan Kusini, Kenya na katika Pembe ya Afrika: kwa upande wa bara Asia  huko Ufilippini, Indonesia, Sri Lanka na Nepal; Mcha za Mashairiki kwa hakika kama vile  Siria;  Na Afrika ya Kaskazini. Kwa njia hiyo neno mshikamano katika mjadala wa umma kwa miaka hii ya mwisho umekuwa ni neno haya linalitumiwa vibaya, limebadilishwa au kuwekwa pemebeni katika kipidni cha kipeo cha uchumi na ubinafsi wa kijamii.. Kwa maana hiyo Siku ya Kimataifa ya mshikamano, inataka kusisitizia hili kwamba ni muhimu kupambana na kuangusha zile hofu na kasumba, ujuu juu ambao hauleti maana na wala mshiko. Ni lazima kufanya uzoefu wa elimu dunia dhidi ya malimwengu katika Jumuiya zetu ambazo mara kwa mara zinajionesha katika mioyo ya vijana na hivyo waweze kufunguka na kujitambua kwa kina mada kuu ya maisha.

 

20 December 2019, 14:38