Tafuta

Vatican News
Kuzaliwa kwa Yesu kwa hakika kunaonesha kuwa Mungu anapenda sana mtu hadi kufikia kugeuka kuwa mmoja kati yetu kwa ajili ya wema wetu.Amesema hayo askofu Mkuu wa Sdney nchini Australia Kuzaliwa kwa Yesu kwa hakika kunaonesha kuwa Mungu anapenda sana mtu hadi kufikia kugeuka kuwa mmoja kati yetu kwa ajili ya wema wetu.Amesema hayo askofu Mkuu wa Sdney nchini Australia 

Noeli ni kuonesha kwamba kila mtu ni mwenye thamani!

Katika Ujumbe kwa waamini katika fursa ya Noeli Askofu Mkuu Anthony Fisher wa Jimbo katoliki la Sydney nchini Australia anasema kuzaliwa kwa Yesu kwa hakika kunaonesha kuwa Mungu anapenda sana mtu hadi kufikia kugeuka kuwa mmoja kati yetu kwa ajili ya wema wetu.Hiyo ndiyo Habari Njema ambayo wakristo hawachoki kamwe kutangaza. Na ndiyo hicho kinatoa thamani katika familia,parokia,shuleni,hospitalini na katika utume.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila mmoja wetu ni mwenye thamani na isiyoweza kubadilishiwa ndiyo wito unaoonekana katika Ujumbe wake wa  Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana wa kwa waamini na awenye mapenzi mema wa Askofu Mkuu Anthony Fisher wa Sydney, nchini Australia. Siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana inaeleza kuwa sisi tunathamaniwa na tumependwa.Inawezekana kusema kuwa ni kuweka chumvi nyingi lakini ndiyo maana yake anathibitisha Askofu Mkuu Fisher Kuzaliwa kwa Yesu kwa hakika kunaonesha kuwa Mungu anapenda sana mtu hadi kufikia  kugeuka kuwa mmoja kati yetu kwa ajili ya wema wetu. Hiyo ndiyo Habari  Njema ambayo wakristo hawachoki kamwe kutangaza. Na ndiyo hicho kinachotamaniwa kwa ajili ya wema ambao unafanyika ndani ya familia, ya parokia, shuleni, hospitalini na katika utume wa umisionari wowote ule. Hiyo ndiyo Habari  Njema ambayo wakristo wa nyakati zote hawachoki kamwe kutangaza. Na ndiyo hicho kinachotamaniwa kwa ajili ya wema ambao unafanyika ndani ya familia, ya parokia, shuleni, hospitalini na katika utume wa umisionari wowote ule.

Uharibifu wa misitu na vichaka nchini Australia

Hata hivyo katika ujumbe wake, Askofu Mkuu Fisher hakukosa kuenesha janga la na idadi kubwa ya moto ambao unaendelea kuangamiza sehemu kubwa ya Australia kwa kipindi sasa ambacho  hadi sasa imeharibu karibia ekari elfu 200 za misitu na vichaka. Injili inahamasisha kuwa na jitihada zetu kwa ajili ya kuweza kusaidia kilimo na wale wote waliokumbwa na baa hili la ukame, amesisitiza; Injili inatia moyo na ujasiri wa kukesha dhidi ya moto naili kuweza kuwatunza wale ambao wanapambana mbele ya majanga haya. Mtoto Yesu kwa hakika anazungumza na kila mwanadamu kwa maana yeye alikuja kwa ajili ya mtu mwenyewe binadamu.

Kama ilivyokuwa kipindi cha Erode hata leo hii bado kuna watoto wasio na hatia

Askofu Mkuu wa  Sydney katika ujumbe wake anatoa mwaliko pia wa  kutosahau mauaji ya wale wasio kuwa na hatia ambao anasema kama ilivyokuwa kipindi cha Erode, hata leo hii bado watoto wanauwawa ambao hawajazaliwa. Leo hii ni hatari zaidi kuliko awali hasa baada ya uamuzi wa hivi karibuni wa utoaji wa mimba huko Wales Mpya ya Kusini; “Watoto wasio na hatia, walemavu na wasiohitajika; wanaokandamizwa bila hatia, kutiwa kwa ndani kwa Wakristo,  wanaoteswa na kuwatia kizuizini wale wanaotafuta hifadhi; wazee wasio na hatia na kutunzwa vibaya huku wakitishiwa na euthanasia au kifo laini. Mbele ya mambo yote hayo, sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana zinatoa fursa kwa mara nyingine tena kufanya uchaguzi kwa maana ya kutenda kama Erode yaani  kuona kuwa kuna wale wanaostahili, au kutenda kama  Malaika na wachungaji katika hori, waliotoa sifa kwa Mungu na kusali kwa ajili ya amani duniani kwa kuonesha kuwa kila maisha ya binadamu ni muhimu.

 

 

23 December 2019, 13:39