Tafuta

Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama wa Jimbo Kuu Katoliki Abuja Nigeria Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama wa Jimbo Kuu Katoliki Abuja Nigeria 

Askofu Mkuu Kaigama:wanasiasa kuwa karibu na watu wenu kutambua mahitaji yao!

Wakati wa sherehe za kumkaribisha katika Jimbo kuu Katoliki la Abuja,Askofu Mkuu Kaigama amewageukia wanasiasa ili wawe karibu na watu wao huku wakitambuahali ya mahitaji yao na matatizo ya kijamii kwa ujumla.Haikubaliki viongozi kutumia jet na elkopta za kusafiria kwa kuepuka barabara mbovu zilizoharibika amesisitiza.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama, wakati wa sherehe za kupokelewa katika  Jimbo Kuu jipya Katoliki la  Abuja  nchini Nigeria hivi karibuni mwezi huu  ametoa hotuba yake akiwawaangazia wanasiasa kwamba: “mnazuia kuwasiliana na watu ambao hamjuhi hata matatizo na mahitaji yao. Ni lazima kuzuia tabia ya viongozi kuzungukwa na walinzi wa usalama huku wakiwa na silaha na mbwa wa ulinzi na kugeuka watu wasiokaribiwa na hata kuguswa na mahitaji ya watu wa Kawaida; badala yake wahakikishie masikini, watoto wadogo, wajoli, vijana, wajane na watu wakaao pembezoni wanapata mambo msingi ya maisha katika jamii na kuwawekea umakini zaidi.” Amesisitiza Askofu Mkuu Kaigama. Vilevile Askofu Mkuu Kaigama amelaani vikali kuhusu baadhi ya viongozi wanaotumia madaraka yao na wanajificha ndani ya maofisi yenye viyoyozi na kusafiri vizuri kwenye Jet au Elicopta, wakepuka kupita barabara mbovu sana kutokana na ukosefu wa matengenezo na miundo mbinu mbaya.

Umakini kwa ajili ya hali ya vijana

Askofu Mkuu Kaigama kadhalika katika hotuba yake kwa namna ya pekee  ametaka kutoa hoja kwa wahusika wa kisiasa juu ya kuwa na umakini wa  hali halisi ya vijana na ambao  wanawakilisha sehemu kubwa ya watu wa Jimbo Kuu Katoliki na nchi yote ya Nigeria kwa ujumla. “ Nitasali na wanasiasa na kufanya majadiliama nao juu ya kuweza kuona ni kwa jinis gani ya kuwasaidia vijana wetu. Nitaendelea kusisitizia ulazima wa kulinda maisha na mali ya watu wa Nigeria na kwa ajili ya kutoa kazi ya vijana wetu, kuwaonya kwa sababu wasiweze kuangukìa katika mitego ya mivutano ya kikabila, kidini, kisiasa, ghasia na matendo mengine dhidi ya maisha ya kijamii”. Ameisitiza Askofu Kaigama.

Ulazima wa kiroho na kichungaji kwa viongozi wa kidini

Askofu Mkuu Kaigama akiendelea na hotuba yake amelaani vikali juu ya tabia ya baadhi ya viongozi wa kidini ambao wanajifanya kuhubiri matarajio mema huku wakijilimbikizia utajiri kwa njia kuwalaghai maskini ambao  ndiyo sehemu kubwa ya watu wa Nigeria. “Haiwezekani kuona sehemu yangu ya  kama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katika mwelekeo kupewa heshima na huku inatokea kuhamasisha malimwengu, hadi kufikia kukabiliana na hali halisi ya Meya wa mji au Waziri wa nguvu na mwenye utajiri. Kazi yangu ni ya kiroho na kichungaji”, amesisitiza na kongeza kumshukuru Rais wa nchi Bwana Muhammadu Buhari na Makamu wake profesa Yemi Osibanjo, kwa ujumbe wao walio mtumia wa matashi mema ya kupewa mamlaka hayo mapya kama Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Abuja nchini Nigeria.

13 December 2019, 15:42