Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akiwa anatoa hotuba yake katika mnara wa kumbu kumbu kwa waliouwawa kwa bomu la atomiki kunbako mwaka 1945 Baba Mtakatifu Francisko akiwa anatoa hotuba yake katika mnara wa kumbu kumbu kwa waliouwawa kwa bomu la atomiki kunbako mwaka 1945  (AFP or licensors)

Marekani:Maaskofu waunga mkono Papa kuhusu dunia bila silaha za kinyuklia!

Akiwa huko huko Nagasaki na Hiroshima Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake ya kitume kwa hotuba yake ametoa ushuhuda wa nguvu juu ya hatua kubwa ambayo imekuwapo dhidi ya silaha za kinyukilia kwa ajili ya maisha ya kibinadamu.Kufuatia hiyo hata Maaskofu nchini Marekani wanaunga mkono tamko hilo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maasakofu nchini Marekani wanaunga mkono kwa pamoja juu ya wito wa Baba Mtakatifu Francisko alioutoa nchini Japan kwa ajili ya dunia isiyo kuwa na silaha za kinyuklia na wanathibitisha juhudi zao za kuhamasisha dunia ambayo isiwe na salaha za kinyuklia. Amethibitisha hayo Askofu David J. Malloy, Rais wa Tume ya Haki na Amani kimataifa ya Baraza la Maaskofu nchini Marekani (Usccb).  Akiwa huko huko Nagasaki na Hiroshima Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake na hotuba yake ametoa ushuhuda wa nguvu juu ya hatua  kubwa ambayo imekuwapo dhidi ya silaha za kinyukilia kwa ajili ya maisha ya kibinadamu, na kwa maana yakufuata nyayo za watangulizi wake kama Papa, amezidi kuomba ili kweli dunia iweze kuondokana na silaha za kiatomiki amesisitiza hayo Askofu Malloy.

Mkataba wa kusitisha silaha za kinyuklia

Askofu Malloy anasema kwamba , kwa upande wao maaskofu wa Marekani wanaungana kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha kwamba dunia inaishi bila silaha za kinyuklia na ambapo inadhihirisha katika sahini ya mktaba wa kusitisha kunako mwaka 1993 na ndiyo wazo kuu zaidi la kimaadili linalotakiwa hasa kuwa kwa dhati lengo la kisiasa. Rais wa Tume ya Haki na Amani kimataifa kwa maana hiyo ameitisha mwendelezo mpya wa Mkataba wa START kati ya Urusi na Marekani ambao bado wanashikilia  asilimia 90 ya silaha za kinyuklia katika dunia. Kwa maana hiyo  inaweza kuwa na busara kwa ajili ya hatua ya kwenda mbele  zaidi.  Mkataba mpya  wa START, ulianza kutumika kunako mwaka 2011 unataka kupunguza idadi ya makombora ya kupigania yaliyowekwa ndani, makombora yaliyozinduliwa na manowari yaliyo na mabomu ya atomiki na vichwa vya nyuklia. Mkataba huo unadumu kwa  kipindi cha miaka kumi napia unao  uwezekano wa kuongeza zaidi kwa miaka mitano. Kutokana na hiyo basi Mkataba huo utamalizika kunako mwaka 2021 lakini  kwa sasa Washington haijaamua ikiwa wataongeza zaidi muda.

26 November 2019, 17:12